ukweli kuhusu ufaulu kidato cha sita kuwa juu na 0 kupungua

young j

Member
Joined
Dec 22, 2012
Posts
58
Reaction score
17
Kulingana na matokeo ya kidato cha sita kuwa juu na zero kupungua ukweli ni huu ambao bado hamjafaham
Daraja sasa daraja zamani
A 100-75 A 100-75
B+ 74-60 B 74-65
B 59-50 C 64-55
C 49-40 D 54-45
D 39-30 E 44-35
E 29-20 S 34-25
F 20- 0 F 25-0
Kwa kuangalia hapo tuu utaelewa ni kiasi gani mwaka huu wamependelewa mfano mwanafunzi wa mwaka huu amepata C mbili za marks 43 lakini mwanafunzi ambaye alimaliza miaka ya nyuma kama alipata marks kama hizo yaani 43 ingetambulika amepata E mbili, sasa kwa kuangalia mfano huo tu tutafakali wanaJF wenzangu ingetumika mfumo wa awali tungeshuhudia matokeo ya aina gani? asante
 

Kwa mtindo huu basi hata pcb mwenye C flat hana sifa ya kuchaguliwa medicine mana watatuletea madaktari feki........masikini elimu ya tanzania vilaza nao wanaonekana wako juu
 
Kutatokea mkanganyiko mkubwa sana kwenye sehemu yoyote inayofanya selection yoyote (academic or employment) pale ambapo kigezo cha ufaulu kitatumika, na maombi yakawa yanatoka kwa watahiniwa wa kabla ya 2014 na wale wa kuanzia 2014 onwards?
 
Kutatokea mkanganyiko mkubwa sana kwenye sehemu yoyote inayofanya selection yoyote (academic or employment) pale ambapo kigezo cha ufaulu kitatumika, na maombi yakawa yanatoka kwa watahiniwa wa kabla ya 2014 na wale wa kuanzia 2014 onwards?

Ndio hivyo yani ndugu yangu elimu yetu sijui wanaipeleka wapi
 
Kama hali ni hiyo kuna uhalali kweli wa kulinganisha na ufaulu wa mwaka 2013 wakati vigezo ni tofauti kabisa. Yaani alama za C mwaka 2013 sasa ni alama za B+ kisha NECTA wanatuammbia eti ufaulu umeimarika. Yaani huko ni kuimarika au ni kudhoofu? Kweli kuishi ni kuona mengi na ukistaajabu ya ----- utaona ya -------


E=young j;10085660]Kulingana na matokeo ya kidato cha sita kuwa juu na zero kupungua ukweli ni huu ambao bado hamjafaham
Daraja sasa daraja zamani
A 100-75 A 100-75
B+ 74-60 B 74-65
B 59-50 C 64-55
C 49-40 D 54-45
D 39-30 E 44-35
E 29-20 S 34-25
F 20- 0 F 25-0
Kwa kuangalia hapo tuu utaelewa ni kiasi gani mwaka huu wamependelewa mfano mwanafunzi wa mwaka huu amepata C mbili za marks 43 lakini mwanafunzi ambaye alimaliza miaka ya nyuma kama alipata marks kama hizo yaani 43 ingetambulika amepata E mbili, sasa kwa kuangalia mfano huo tu tutafakali wanaJF wenzangu ingetumika mfumo wa awali tungeshuhudia matokeo ya aina gani? asante[/QUOTE]
 
Yani hapo wenye sifa za kuingia chuo naona mwenye div 3 ya 10 ndo iwe ya mwisho kuchukuliwa, hao wengine waliobaki hawastahili kwakweli kuingia chuo.
 
Inanibidi nipeleke cheti changu wakakiapudeti nafikiri nitapata nafasi ya kuingia chuo.
 
Hii BRN imetupeleka pabaya sana [/QUOTE]
 
Kama viwango ni tofauti kihivyo hatuwezi kusema ufaulu umeimarika

 
MWAKA 2013: A = 80 – 100; B = 75 - 79;
C = 65 – 74; D = 55 – 64; E= 45 – 54; S =
40 – 44 na F =0 – 39.
Hivyo vilikuwa viwango vya ufaulu 2013
linganisha na vya sasa.
 
[/QUOTE]

So kweli kijana.. Viwango au madaraja ya zamani hayakuwa hayo..afu nectar walikuwa wanatumia flexible grade ranges ambayo huchange kutokana na mazingira.. Tukubali kuwa madogo wetu wamefaulu..miaka ya nyuma kwenda principal mark ni E but now ni C.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…