Binafsi nimeangali hiki kipindi muda huu ITV nikajikuta nafika mbali sana na kuona kila kitu kinapita hapa tu katika hii duniani na hata haya madaraka na mambo mengine tunayohangaika nayo ni ya kupita tu.
Nimemuona Nyerere anakagua gwaride ila leo ni marehemu.
Nimemuona Raisi aliechukua madaraka ya kuiongoza Uganda baada ya Amini kuangushwa Bina Issa ambae nae leo hii ni marehemu.
Halikadhakika, nimemuona Kawawa kama waziri wa Ulinzi akikamkaribisha Nyerere kuhutubia wananchi ila nae leo ni marehemu.
Nimeona makamanda na wapiganaji wa kitanzania wakishangila ushindi pamoja na kuteka miji ila wengi wao leo nao ni marehemu.
Nimeona wananchi wa Uganda walioteswa na utawala wa Amini wakiyashangilia majeshi ya Tanzania lakini Amin huyu na wanachchi wake hao leo hii wengi wao watakuwa ni marehemu.
Kwakweli hii film imenifanya niwaze mbali sana na kuona hii dunia na mambo yake yote haina maana na tunahangaika bure tu katika hii dunia.
Miaka 30 au 40 ijayo haya yote tunayohangaika kuyafanya katika hii dunia yawe mazuri au mabaya yatakuwa ni historia tu.
Ni bora kutenda wema tu ili mungu atukumbuke katika ufalme wake kuliko kuhangaika na haya ya duniani ambayo hayana maana bali ni ya kupita tu.
Kila napoona film za aina hii huwa nafika mbali sana kimawazo kwa mfano ile ya kuwaua Wayahudi wakati wa Adolf Hitler n.k