Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Mohamed Said,

..naelewa kwamba hoja ya Tanganyika kudai uhuru ililalia ktk ukweli kwamba tulikuwa ni trustee territory na siyo koloni la Muingereza. ukweli huo ndio uliomfanya Mwalimu aende kutoa kilio chetu UNO, na siyo mahali pengine popote.

..nilichokuwa najaribu kuuliza ni kama unamfahamu MWANDISHI wa hotuba ile aliyosoma Mwalimu UNO.

..pia ningependa kujua kama unamfahamu mwandishi aliyeandika maneno yale mazito ambayo mpaka leo bado yananukuliwa " sisi wananchi wa Tanganyika tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima kilimanjaro. umulike ndani na nje ya mipaka yetu. Ulete matumaini pale ambapo hakuna matumaini. Ulete upendo pale ambapo pamejaa chuki, na heshima pale ambapo pamejaa dharau."

..kama nilivyokueleza hapo awali, mwandishi aliyeandika hotuba ya John Kennedy yenye maneno "ask not what your country can do for you, but what you can do for your country" anajulikana na amepewa sifa zake anazostahili. uandishi wa hotuba ni taalamu, na hotuba nyingi wanazosoma viongozi wetu huwa zimeandikwa na wasaidizi wao. ingependeza sana kama hapa kwetu tungewajua waandishi wa hizi hotuba za viongozi wetu na kuwapa sifa zao.
 
Mag 3: Kwa hilo Kuwa mimi Muislam kwanza kisha Mtanzania wala hujakosea. Kama una marafiki wa Kiislam na wanasema hapana dhulma dhidi ya Waislam nchi hii nawakaribisha katika huu mnakasha na nina maswali nitawauliza na wana ukumbi wenyewe wataamua. Ili taifa lidumu katika umoja ni kuwa ipatikane haki kwa wote bila upendeleo. Kama unadhani amani itasimama kwa jamii moja kuwa juu ya nyingine unakosea. Soma historia. Asiyataka amani hatoi nasaha na kuwatahadharisha ndugu zake. Tulia, chunguza maneno yangu tafakari Insha Allah utanielewa. Nina wengi katika Wakubwa wanakubaliana na mimi kuwa nisemayo ni kweli. Bahati mbaya Mungu hajawapa ujasiri wa kusema kweli.

Huwezi kusema "mimi muislamu kwanza kisha Mtanzania" halafu ukaenda kusema "ili taifa lidumu katika umoja ni kuwa haki ipatikane kwa wote bila upendeleo". Kauli yako ya kwanza ishaligawa taifa katika misingi ya dini, huwezi kuanza kuligawa taifa kwa misingi ya dini halafu kuongelea kulihifadhi taifa hili hili lidumu kwa kutaka haki sawa kwa wote.

Sentensi zako zinajikanganya. Ya kwanza inaonyesha hujali utaifa kama unavyojali udini, na kama kuna mkwaruzano kati ya maadili ya kidini na maadili ya kitaifa utachagua ya kidini. Kauli ya pili inataka kutukuza (au angalau kuhifadhi) na kufaidika na utaifa na kudai kupata haki sawa chini ya utaifa huu huu unaoutelekeza chini ya udini.

Wewe ushalifanya taifa kama second priority, halafu unataka kulalamika kama taifa litakufanya wewe kuwa second priority (Sisemi kwamba taifa limekufanya second priority, nachanganua maneno yako).

Hivi unaona kuna haki hapo?

Katika kuwasema wanaume wakware wenye kupenda mabibi wengi, wanawake wa Kimarekani wamekuja na msemo wao wanaupenda sana siku hizi "Never make someone a priority if you are only an option to him". Wakimaanisha kwamba wanawake wasiwadekeze na kuwapa umuhimu wa kwanza wanaume ambao wana wanawake wengi na wala hawawapi umuhimu wa kwanza hawa wanawake. Sasa wewe mbona unataka kuwa kama huyu mwanamme mkware ambaye anamfanya mwanamke fulani kama option number mbili au chini zaidi, halafu anategemea mwanamke huyu awe amekaa nyumbani tu anamsubiri huyu mwanamme kama priority number one ?

Unalipa taifa second priority, halafu unasema wewe huwezi kuwa second class citizen (basically, unataka haki sawa kwa wote) katika taifa hilo, hivi kanuni ya reciprocity itakuhukumu vipi ? Kanuni ya Newton ya kwamba "every action has an equal and opposite reaction" ikija kuwekwa hapo itakuweka wapi?

Waswahili wamesema "Baniani mbaya, kiatu chake dawa". Utaifa si kitu, mimi muislamu kwanza, lakini katika haki za kitaifa zote nazitaka, ama sio ? Changu changu, chako changu. Unamsimanga mpishi hajui kupika huku ungali ukila ? Na unadai kuongezewa chakula zaidi uwe sawa na wenzako ? Huku unamaka, chakula hiki si lolote si chochote, mama yangu anapika vizuri zaidi. Nenda kwa mama yako basi ukale.

Kama dini ni priority kwako kuliko utaifa nenda Saudia kwenye nchi ya kiislamu ukaombe uraia, useme Tanzania waislamu wanaonewa.
 
Huwezi kusema "mimi muislamu kwanza kisha Mtanzania" halafu ukaenda kusema "ili taifa lidumu katika umoja ni kuwa haki ipatikane kwa wote bila upendeleo"

Sentensi zako zinajikanganya. Ya kwanza inaonyesha hujali utaifa kama unavyojali udini, na kama kuna mkwaruzano kati ya maadili ya kidini na maadili ya kitaifa utachagua ya kidini. Kauli ya pili inataka kutukuza (au angalau kuhifadhi) na kufaidika na utaifa na kudai kupata haki sawa chini ya utaifa huu huu unaoutelekeza chini ya udini.

Exactly, ndio maana mimi sipotezi muda kumbishia kuhusu historia anayoiandika kwani watu hawataona tofauti kati yangu na Mohamed Said. Mohamed Said hana tofauti na watu wanaozaliwa wakiwa jinsia fulani lakini wanakuja kudai kuwa pamoja na kuwa na maungo ya jinsia hiyo wanaikana na kujiita jinsia nyingine. Mimi ni Mtanzania kwanza halafu Mkristo kama walivyo Watanzania wengi pamoja na wale wenye dini tofauti na wasio na dini. Adui wa Tanzania atakuwa adui wa Watanzania wote na si wa Waislamu, Wakristo na wasio na dini peke yao.

Kinachonituma nichangie katika mada hii ni hofu yangu baada ya kugundua kuwa kuna kikundi cha watu wasiouenzi Utaifa wao kama Watanzania. Kwao kila kitu kinaangaliwa katika misingi ya kidini na potelea mbali hata kama kwa kufanya hivyo wanahatarisha umoja wetu kama taifa. Mfano ni huyu mpuuzi Mohamed ambaye ana jeuri ya kutaka kutumia udini wake kupandikiza mbegu ya chuki miongoni mwa jamii ya Watanzania. Kwa upofu wake anashindwa hata kuiona hatari iliyo mbele ya taifa letu iwapo lengo lake hili litafanikiwa kwani ametanguliza Uislamu kabla ya Utaifa, dini tuliyoletewa na Wageni sawa na Ukristo.
 
LG: Mimi silalamiki. Mimi naiweka historia ya wazee wangu katika ramani isije kamwe ikapotea. Kama unahisi mimi ninasema uongo basi eleza ukweli ni upi. Ukumbi huu ni kwa watu kueleweshana. Mimi nimejifunza mengi humu na sitachoka kusoma na kujifunza fikra mpya hata kama sizikubali. Ghitilafu katika dunia haziwezi kuisha. Nimeeleza katika historia ya Waislam juhudi zetu za kuung'oa ukoloni na juhudi zetu za kujiletea maendeleo baada ya uhuru kupatikana 1961 juhudi ambazo zilihujumiwa na Nyerere. Huu ndiyo ukweli. Mifano nimetoa mingi. Labda tatizo ni kuwa wewe hujui kuwa hivi ndivyo ilivyokuwa. Fanya uchunguzi kama niliofanya mimi na Wakubwa watoe maoni yao kuwa hawakuihujumu EAMWS kwa ajili ya kutaka kujenga chuo, hawakuhujumu miradi ya OIC, Darul Iman nk. Kwa wewe kujibu bila utafiti itakuwa tabu kupata ukweli. Tuendelee kujadiliana.

Ndugu Mohammed Said , Mwalimu Nyerere ndo kisha tutoka na hayupo hapa nasi, kwa hiyo sahau yale yote ya Mwalimu kama itakavyo kupendeza.
Nasema hivyo ili utafute sababu nyingine na mtu mwingine wa kumlaumu kwa jamaa zako kutopata maendeleo unayaoyahitaji.
Tumejaribu kukushawishi umoja wa kiTaifa baado umeng'ang'na na udini wako.
Sasa inabidi tuelewane kitu kimoja kama hatuendi pamoja , basi uende kivyako na wengine kivyao, umoja kwishnei, ndio maana nikakuita CUF usiye sikia la muadhini wala shekhe ateteae umoja.
Vile upendavyo fanya ndani ya Uislamu wako na narrow mindedness yako.
Mimi nikifikiri kuendelea kwako kutatokana na juhudi ya pamoja kama waTanzania, sasa kama wewe unataka kuifurahisha roho yako kwa kumlaumu Mwalimu , hiyo ni hiari yako isiyokuongezea kipato wala elimu ya ziada.
Kama nilivyo sema awali, inaelekea waumini wa siasa ya ubaguzi wa kidini ulionao wakiwa wengi basi na ushinde vita hiyo.
Lakini nchi hii inayoitwa Tanzania itabidi imegwe vipande vipande ili watu wa aina yako muwe na kwenu na wengine wae na kwao.
 
Huwezi kusema "mimi muislamu kwanza kisha Mtanzania" halafu ukaenda kusema "ili taifa lidumu katika umoja ni kuwa haki ipatikane kwa wote bila upendeleo". Kauli yako ya kwanza ishaligawa taifa katika misingi ya dini, huwezi kuanza kuligawa taifa kwa misingi ya dini halafu kuongelea kulihifadhi taifa hili hili lidumu kwa kutaka haki sawa kwa wote.

Sentensi zako zinajikanganya. Ya kwanza inaonyesha hujali utaifa kama unavyojali udini, na kama kuna mkwaruzano kati ya maadili ya kidini na maadili ya kitaifa utachagua ya kidini. Kauli ya pili inataka kutukuza (au angalau kuhifadhi) na kufaidika na utaifa na kudai kupata haki sawa chini ya utaifa huu huu unaoutelekeza chini ya udini.

Wewe ushalifanya taifa kama second priority, halafu unataka kulalamika kama taifa litakufanya wewe kuwa second priority (Sisemi kwamba taifa limekufanya second priority, nachanganua maneno yako).

Hivi unaona kuna haki hapo?

Mkuu kundi la hawa jamaa ingekuwa enzi za Mwalimu na Simba wa Vita tayari wangekuwa wamepewa miraba yao kupalilia huko Mafia, na wangerudi toka huko wajue Taifa ni kitu gani,
Na hata wakipewa Taifa kuliongoza, Mungu aepushie mbali, watu hawa hawakawii kuwa kama Al Shaabab, na kukata watu mikono , miguu na kupiga watu mawe hadi wafe.
Maono haya yanawezaligharimu Taifa hili.
 
Joka Kuu: Hebu soma hii hapo chini:

Tanganyika as a Mandate Territory

Britain was administering Tanganyika under articles 76 and 77 of the Charter of the United Nations. As the administering authority, Britain was expected to establish and promote political, economic and social advancement of Tanganyika until such time as its people were ready for self-rule. In spite of this international commitment, the British were more interested in safeguarding their own colonial interests and those of other minorities’ but-not those of the indigenous African majority. In order to pre-empt African reaction to this injustice, in 1949 Governor Twining invited proposals from prominent individuals, welfare societies and from Native Authorities, as to how Tanganyika should be governed. The TAA Political Sub-Committee formed in 1950 submitted a memorandum to the Constitutional Development Committee which was signed by the entire executive: Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando and Said Chaurembo.

The author was for the first time informed of the existence of this document by one of Hamza Mwapachu's children, Juma Volter Mwapachu. He was informed that his father took great pride in having participated in the drafting of this document. In her book Listowel mentioned this document and its historical significance to the political history of Tanganyika. Cranford Pratt is the only researcher who analysed the document in detail. The document was first consulted by Pratt in 1959 in a file of the Committee on ‘Constitutional Development Report/and Despatches to the Secretary of State’ no. 1146-6, Dar es Salaam Secretariat Library. Although this file is available at the Tanzania National Archives, the document is missing. The author was informed that a microfilm of the document was available but that too could not be traced. (For more information on loss of historical documents see M. Said, ‘In Praise of Ancestors Revisited’ in Africa Events, London March, 1989, pp. 50-51).

In his annual report for 1950, Abdulwahid was to write:

"For the welfare of the Africans and to safeguard the interests of this Association and those of the African community as a whole, this Association has arranged for an advocate to stand by and to advise the Association on the technical side of the law. This advocate is Mr. E.E. Seaton of Moshi. He has from time to time written to the Association on various political subjects, and helped a great deal with his advices when this Association was compiling its memorandum on constitutional development. "

Abdulwahid realised that many of the problems in respect of the rights of Africans in the territory were legal issues which required the advice of legal experts. For the first time, with the help of Seaton, TAA was able to confront the colonial authority with facts and figures illustrating injustices in the colonial system which were contrary to the United Nations Charter.

In his analysis of the TAA memorandum to the Constitutional Development Committee, Pratt reported:

The most detailed African submission came from the Dar es Salaam branch of the Tanganyika African Association. It asked that the distribution of seats (i.e. an official majority and one-half of the unofficial to be African) should be held constant for the next twelve years and that in the thirteenth year a common electoral roll should be introduced with a majority of the council then being elected.

Governor Edward Twining’s committee ignored TAA’s recommendations. The government continued with its long-term plans of strengthening the positions of minority Europeans and Asians in the political development of the territory while pushing aside the indigenous Africans contrary to the United Nations Charter. Many learned Africans were of the opinion that the TAA submission should have rightly formed the basis of the future constitution of the territory as a multi-racial society. But the spirit of that document did not die. It surfaced at the TANU founding conference on 7 th July, 1954 and was to form the basis of Julius Nyerere’s speech before the Trusteeship Council of the United Nations in New York in March, 1955.
The key word here is that it "formed the basis of Julius Nyerere's speech before the Trusteeship Council of the UN in 1955." It formed the basis. Nyerere hakuisoma word for word.Tunaomjua Nyerere tunajua kuwa mkono wake pia ulikuwemo kwenye hiyo speech. Lakini Mohammed Said hakulisema hilo, alitaka tuamini kuwa ile hotuba iliyoandikwa na Walid Sykes aliisoma UN word for word. Thank you jokaKuu. Unasaidia sana kuchokonoa mambo.
 
You are at it again Maalim , Sheikh Mohammed Said.
Uongo unaporudiwa rudiwa hata facts zinapindishwa kwa ajili ya kuutukuza udini.
Udini ni ugonjwa unaojitokeza kama imani.
Ugonjwa wa udini ukimpata mtu hata yeye kujitambua inakuwa shida.Na huu ndio ugonjwa unaomsumbua mwenzetu huyu Mohammed Said.
Katika nchi yenye makabila mengi , imani tofauti na vile vile rangi tofauti ni ukosefu wa upeo wa yajayo kujikita katika utetezi wa udini, kwa luelemea dini moja.
Now lets get back to what has been said by our writer MS

1.Islam and ignorance, the two paradigms are mutually incompatible. To be a Muslim the prerequisite is to be knowledgeable.

How true!!
But what is the reality?
The writer goes back to blame the Church and government for his own under achievement.
It is not a secret that up to now as we speak,wherever you find a church , a school will be in the vicinity, but look at our mosques, it is as if madrassa schooling is incompatible with modern formal education.
If Islam was in East Africa well befaore the 16 th Century where are the formal Islamic school schools that one can brag about?
We should not shy away from the realisation that there was a serious lack of vision by our Arabic visitors and their Islamic converts, and even when the European colonisers came to Africa, they RESENTED formal education, much to their own undoing.

Uislamu nchini umerealise kuwa elimu ya kikoloni ni mali wakati jua limeshakuchwa na uhuru upo mkononi.
Kasumba ya kutothamini elimu hata leo ipo sehemu tofauti nchini palipo na imani kali. Kuoza na kuozwa baada tu ya kumaliza mafunzo ya madrassa hutawala badala ya juhudi kubwa ya ushindani wa kupata elimu ya darasani.
Sasa wenzetu hawa wanarudi nyuma kuulaumu ukristo na serikali kwa wao wenyewe kuchelewa kuchangamkia elimu kwa karne nyingi tu.
The question that the colonial govt and christianity thwarted the efforts of muslims to study higher education leaves much to desire and is complitely false. One wonders why the muslims did not send students to Arabic countries for that matter, through their mosques to circumvent these restrictions?
Lets face it, the interest for formal education in many Islamic communities was not there in the first place.

2. d. In mid 1990s Darul Iman from Saudi Arabia was refused permission by the government to build a technical secondary school in the Coast Region, Mainland.

Maalim Mohammed Said, usipoteze muda kuandika untruths about your own under achievements na machafuko mengi tu katika organisations zenu za Kiislamu.
Pale Chang'ombe (opposite Chan'ombe Pr School)kuna Chuo ambacho kingekuwa kwa taaluma ya kuwajenga waislamu,kimejengwa nafikiri 1968 kwa msaada kutoka serikali ya Misri.
Mpaka leo it is a white elephant, na wajanja miongoni mwenu sasa wanauza eneo hilo kwa wahindi. Unauza sehemu ambayo ingewafaa waislamu wenzio halafu lawama kwa watu wengine.
Jichunguzeni kwanza , you guys are totaly unamanagable within and between yourselves, that is a fact.

3. Dr. Hamza Njozi's has further evidence:

…Arabia (May, 1985) wrote under the heading "A Closed Door to the Corridors of Power": ‘The majority of pupils in Tanzanian primary schools are Muslim (80 percent), a percentage which dwindles to 15-20 percent in secondary schools, sinking to a mere five percent at University level'. Almost fifteen years later, on 2 February, 1999 the Member of Parliament for Kigamboni Hon. Kitwana Kondo told the parliament that out of every 100 students who sat for the standard seven examination in Dar es Salaam in the year 1998, 71 were Muslim and 29 Christian. But out of every 100 students selected to join government secondary schools only 21 were Muslim while 79 were Christian. The MP wanted to know whether Muslim children were inherently dull (An-Nuur, February 5-11, 1999).

Now this may be characterised as a writing from a learned person but complitely lacking in logical objectivity and falsified facts. What a shame for a person masquerading as a PhD holder.
When you propound that 80% of ALL primary school goers IN TANZANIA ARE MUSLIMS and put it as a fact, then I am sorry only fools will believe this!
And bigger fools have the audacity of putting it on paper!!
Like I said, I am sorry, but my intellect does not allow me to stomach this and I have no further comment on this. With a wrong opening assumption one ends up with an equally wrong conclusion.
Njozi's claims will remain to be dreams, as a credit to his name sake, unless he and many others of his ilk, work on actively to build more primary and secondary school in their home steads.
Kitwana Kondo(KK wa Dar), is your wrong bench mark my dear Mohammed Said. Those who know this gentleman will attest to the fact that he is a murky character, often operating in shadowy circumstances both in politics and in life.
We will be more that happy Mr Mohammed Said if you will give us KK's shadowy life history. Remember his case with Martha Wejja? well it is said that the Judge in that case died in mysterious circumstances at Muhimbili.
As for the secondary school statistics statistics presented, it does not take very rocket science to figure out the obscure logic behind KK's assertations.
If his statistics are based on students from Chamazi or Mbagala Rangi Tatu Primary school and comparing it with St Josephs Pr School the one has to doubt ones level of intellectual representation in the Bunge.

Mohammed Said you can place all the blame on the Church and the government for the under achievement and under development in all muslim areas, but if at all that is the best you can do then you are probably lost and will rot in a religious jail of your own making.
A religious jail ffrom which a nobody will help you out
Umesema:
Uislamu nchini umerealise kuwa elimu ya kikoloni ni mali wakati jua limeshakuchwa na uhuru upo mkononi.
Kasumba ya kutothamini elimu hata leo ipo sehemu tofauti nchini palipo na imani kali. Kuoza na kuozwa baada tu ya kumaliza mafunzo ya madrassa hutawala badala ya juhudi kubwa ya ushindani wa kupata elimu ya darasani.
Sasa wenzetu hawa wanarudi nyuma kuulaumu ukristo na serikali kwa wao wenyewe kuchelewa kuchangamkia elimu kwa karne nyingi tu.
................................................................................................................................................................
Tangu huu mjadala uanze na wewe kujiunga sijasikia hoja yenye mantiki kutoka kwako.Zaidi unazungumzia umoja wa kitaifa na kwamba waislamu wajione wako sawa na wakristo.Kama nilivyosema awali waislamu wa sasa hawadanganyiki.Ukweli kuhusu historia ya TANU umetufunza mengi.Usawa munaozungumzia nyinyi ni huu wa mdomoni tu ambao tukibweteka nao mutatumaliza.Tunataka usawa uonekane kivitendo katika utendaji serikalini....tutaendelea.
Hapa Lole umejionesha wazi kwamba wewe si mtu makini katika huu mjadala.Hilo ulilozungumza ndio limekushushia hadhi yako mpaka chini kabisa.Unapozungumzia kuchangamkia elimu wewe unatutazama waislamu sisi watanzania ambao ni wahanga wa dhulma katika elimu tangu enzi za mkoloni,ambao kama si rehma za Mungu basi ingekuwa mumeshauzika uislamu Tanzania kwa ugonjwa wa kuwanyima waislamu elimu.
Wewe kweli unafahamu maana ya karne nyingi tu?.Huna habari kuwa waislamu kwa kuelewa kwao umuhimu wa elimu ndio waliowazindua mababu zako wazungu walioleta ukoloni Tanzania.Uislamu kusambaza elimu ni ibada na mafunzo ambayo hayako kwenye ukristo.
Hivi huna habari kwamba tabia ya wakristo kurudisha nyuma maendeleo ya kielimu ya waislamu haikuanza leo na jana?.Umesahau kuwa wakristo ndio waliochoma moto vitabu katika maktaba kule Iraq ya leo na kutumbukiza majivu yake kwenye mto Dijjla mpaka mto wote ukawa rangi ya wino kwa weusi.
Vitabu vichache vilivyopatikana ndivyo vilivyofikishwa kwa wazungu wako (wakoloni) halafu wakapata jeuri hii.

Wewe nahisi ni mpenzi wa sayansi na Physics kama mimi.Mara nyingi umerudia Newton's third law of motion Every Action has an Equal and Opposite Reaction.Hujui kwamba baba wa Physics ni Al-Hasan Ibn Al-Haytham (Alhazen).Yeye ndiye mvumbuzi wa namna jicho linavyofanya kazi.Uvumbuzi uliofuatia kuhusu camera kufikia hata photocopy machine visingewezekana kama si uvumbuzi wake.Kitabu chake Al-Manazir kilikuwa rejea muhimu kwa miaka mingi kuhusiana na somo la mambo ya mwangaza.

Tuseme umepatwa na nini hata ukasahau jinsi kanisa lilivyomfanyia mwanasayansi Galileo!.

Ukija katika uwanja wa somo la hesabu majina kama aljebra ni kutokana na mvumbuzi wake Muhammed Aljabry.Ukija kwenye kemia ndio usiseme kabisa.

Hii habari ni ndefu na kama ungekuwa makini ungewacha kutoa tusi hilo kwa waislamu.

Kuwa kwetu nyuma kielimu Tanzania ni kutokana na dhulma za mkoloni na Nyerere baada ya uhuru.
Zaidi kuhusu mchango wa uislamu katika elimu soma hapo chini kwa furaha.

1.Ushawishi wa Qur'an kuhusu elimu na uvumbuzi

2.Baadhi ya mifano ya michango wa waislamu katika kuipeleka mbele elimu.
 
Jasusi: Ahsante kwa mchango wako. Hakuna haja ya sisi kushindana katika hilo la nani kaandika nini na yupi kafanya lipi katika memorandum hiyo. Muhimu ni kuwa lile ambalo lilitaka kufichwa sasa liko hadharani na kila mtu ana uhuru wa kufanya tafsiri yake. Hapa unanikumbusha kitu kimoja. Wakati wa kuhariri kitabu nilipingana na mhariri katika neno "stolen" maana mimi niliandika kuwa hiyo memorandum imeibiwa yeye akasema hapana tusitumie neno hilo tuweke "missing." Sasa yule mhariri Kiingereza ndiyo lugha yake mimi sikijui kama anavyokijua yeye. Nikawa nimesimama kwa kumpa taarifa ambazo nilikuwanazo kuhusu ugomvi wa nyaraka za TAA na TANU nani ana haki nazo zaidi? Ni za akina Sykes, Nyerere au chama cha TANU? Ugomvi huu ulitokea baada ya uhuru. Kuna mengi najizuia siwezi kuyasema. Unapofanya utafiti unakutana na mengi. Mengine yanaandikika na mengine ni tabu kuyaandika. Ungependa kupata taarifa za upande wa pili lakini upande wa pili haufikiki. Hapo ndipo penye tatizo kubwa na utafiti una misingi na miko yake. Juu ya hayo yote nikaandika makala hiyo iliyochapwa na Africa Events kwa nia ya kuonyesha kuwa zipo nyaraka nyingi zimechomolewa katika majalada na watu kwa dhamira isiyokuwa nzuri. Nilipokuwa maktaba ya CCM Dodoma hili nililishuhudia. Nililetewa jalada la Abdulwahid Sykes ndani hakuna nyaraka hata moja na Hamza Mwapachu ni hivyohivyo. Kwanini iwe hivyo? Jibu nawaachia wanaukumbi walitafute. Ndiyo maana mpaka leo kila nipatapo nafasi humwambia Kleist (mtoto wa Abdu Sykes) kuwa ana dhima kwa historia ya nchi hii na kwa historia ya marehemu baba yake kuwa zile shajara za baba yake ziwe-transcribed ili tujue kuna taarifa gani mle ndani. Si bure kuwa kati ya 1950 - 1954 Abdulwahid Sykes alikuwa akiandika shajara zake kwa hati mkato. Kuna vitu alikuwa ameficha kwa kuhofia Special Branch. Hata taarifa yake kwa TAA ya mwaka 1950 ametaja safari ya Nairobi lakini hakusema kuwa alikwenda kufanya mazungumzo na Jomo Kenyatta. Habari kamili za mkutano ule nilikujazipata kutoka kwa rafiki yake Ahmed Rashad Ali. Kisa kizima cha safari hii nimekieleza katika kitabu. Wanaukumbi endeleeni kuchokonoa kama anavyochokonoa Joka Kuu kwani nami mnanipa nafasi ya kueleza mengi ambayo hayafahamiki katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
LG: Unakuza mambo bila sababu na siwezi kukulaumu kwa kuwa najua huujui Uislam unasema nini. Uislam wa kweli ni tofauti na huo uliozoeleka katika vyombo vya habari. Uislam wa kweli ni ule aliofundusha Allah katika Qur'an na Mtume (SAW) akatuonyesha kwa vitendo. Hilo la kusema mimi kwanza Muislam kisha Mtanzania ni kuwa kubwa kwangu ni Mungu kisha mengine yanafuatia. Na alofundisha Mungu ndilo lenye manufaa zaidi kwetu kuliko fikra za binadamu. Binadamu hutoweka lakini Mungu ni wa kubakia. Katika mafunzo ya Mungu moja ni kutuonya kuhusu dhulma akasema tusidhulumu na wala tusikubali kudhulumiwa. Sasa mimi nipewe miraba ya kupalilia kwa kosa lipi? Hebu nieleza ndugu yangu. Kwa kule kusema ndugu yangu unanikanyaga hebu ondoa mguu wako unaniumiza? Lugha ya vitisho si lugha nzuri na ya kiungwana. Hilo la kukata mikono unalisema bila ya kujua dhahiri yake na hilo la kupiga wazinifu mawe halikadhalika. Lakini hapa tunayojadili siyo hayo. Hapa tunajadili historia ya kudai uhuru wa Tanganyika na dhulma zinazofanywa dhidi ya Waislam. Tujishughulishe na hayo ili mjadala ustawi kwa faida yetu sote. Kama lipo niloandika katika historia ya TANU ambalo si kweli nifahamishe au kama wewe ulilipokea vingine halikadhalika tufahamishe. Namna hii faida kubwa itapatikana na wasomaji watakuwa na hamu ya kutusikiliza. Hapa tuko katika kuelimishana.
 
Yaya: Ahsante. Hapo Dar es Salaam University hali ilikuwa kama unavyoiona hapa ukumbini. Wahadhiri wameshikilia Nyerere, Nyerere kila kitu. Kaleta amani, umoja nk. Sasa mimi nikawa nawauliza kawaletea nani? Sisi wazee wetu ndiyo waliompokea yeye hawamjui tena kapokelewa kwa kauli ya marehemu Abdulwahid Sykes ndiye aliyekuwa rafiki yake. Ihsani imetoka kwa wazee wetu kwenda kwake yeye mgeni wao na hiyo ndiyo amani na umoja wenyewe. Huwezi kuamini mshtuko waliokuwa wakipata. Basi hapo nawaeleza hali ilivyokuwa Dar es Salaam niliyokulia mimi. Nikawa nawaeleza kuwa kwa kufundisha kwa namna hiyo historia iatakuwa inapotoshwa. Sasa tofauti na hapa kidogo pale katika semina au darasani wanafunzi wenzangu wakiniuliza maswali mazuri ya kujenga. Walikuwapo waliokuwa hawaamini nisemayo hata hivyo. Nilikuwa sioni aibu kuwaambia kuwa ile mtu kuwa Muislam peke yake ni ustaarabu tosha mengine yatakuja kujazia tu. Ni muhali mtu atoke atokako aje pwani kuwafunza Waswahili ustaarabu.
 
Ndugu Mohammed Said , Mwalimu Nyerere ndo kisha tutoka na hayupo hapa nasi, kwa hiyo sahau yale yote ya Mwalimu kama itakavyo kupendeza.
Nasema hivyo ili utafute sababu nyingine na mtu mwingine wa kumlaumu kwa jamaa zako kutopata maendeleo unayaoyahitaji.
Tumejaribu kukushawishi umoja wa kiTaifa baado umeng'ang'na na udini wako.
Sasa inabidi tuelewane kitu kimoja kama hatuendi pamoja , basi uende kivyako na wengine kivyao, umoja kwishnei, ndio maana nikakuita CUF usiye sikia la muadhini wala shekhe ateteae umoja.
Vile upendavyo fanya ndani ya Uislamu wako na narrow mindedness yako.
Mimi nikifikiri kuendelea kwako kutatokana na juhudi ya pamoja kama waTanzania, sasa kama wewe unataka kuifurahisha roho yako kwa kumlaumu Mwalimu , hiyo ni hiari yako isiyokuongezea kipato wala elimu ya ziada.

Kama nilivyo sema awali, inaelekea waumini wa siasa ya ubaguzi wa kidini ulionao wakiwa wengi basi na ushinde vita hiyo.
Lakini nchi hii inayoitwa Tanzania itabidi imegwe vipande vipande ili watu wa aina yako muwe na kwenu na wengine wae na kwao.

LG: Si hivyo ndugu yangu mimi nataka na nyie mvae viatu vyetu muone sisi tunahisi vipi. Juhudi ya pamoja ndiyo hiyo wazee wetu waliitekeleza kuleta uhuru wa nchi hii. Soma historia ya Tanganyika uone ni akina nani waliokuwa bega kwa bega na Nyerere.

Mwaka 1963 walimu Wakristo Bukoba wakiungwa mkono na Kanisa Katoliki, waliwapinga wagombea Waislam walioteuliwa na TANU katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Wagombea Waislam walishindwa katika uchaguzi ule. Kanisa lilikuwa limechanganya dini na siasa kwa kuwapinga Waislam wasichaguliwe kushiriki katika kuongoza nchi. Hakuna taarifa zozote zinazoonyesha kama serikali ya Nyerere ilichukua hatua yoyote dhidi ya Kanisa au dhidi ya wale wagombea Wakatoliki. Lakini Waislam walikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa kukataa utawala wa Kikristo katika TANU ñ chama ambacho Waislam walikiianzisha na kukijenga ili kiondoe dhulma. Halamshauri Kuu ya Taifa TANU ilifuta katika TANU Baraza la Wazee wa TANU lililokuwa na wajumbe Waislam watupu kwa kile kilichoitwa "kuchanganya dini na siasa."

Nguvu mpya dhidi ya Uislam na Waislam ilitumia ujanja na mbinu za hali ya juu na hivyo ikafanikiwa kuihujumu EAMWS na kuiweka BAKWATA kuwaongoza Waislam. Vipi serikali ambayo sifa yake ni kupinga ubaguzi wa rangi na kutetea umoja wa kitaifa, itawaruhusu kikundi kisichozidi watu watano kutumia magazeti ya TANU- The Nationalist, Uhuru, Radio Tanzania, polisi na Usalama wa Taifa , vyombo vilivyo chini ya vya dola kuamrisha utengano wa watu na kueneza siasa za ubaguzi wa rangi. Vipi itaundwa jumuiya ya Waislam ambayo licha kuwa haina ridhaa ya Waislam wenyewe vilevile haina ulamaa hata mmoja ndani ya uongozi wake. BAKWATA haikuundwa kwa maslahi ya kumtumikia Allah. Uongozi wa Kikristo uliokuwa madarakani ulikuwa na hofu ya hali yake ya baadae huku wakikabiliana na Waislam walio huru chini ya jumuiya yao wenyewe iliyo huru na mbali na serikali na Kanisa.

Kwa kuwa serikali haikuonyesha dalili zozote za kutaka kuleta fursa sawa kwa wote katika elimu na kugawana madaraka, ikijizatiti katika kuiacha dhulma ya kikoloni iendelee, ilikuwa wazi awamu ya pili ya harakati itaanzishwa dhidi ya serikali iliyohodhiwa na Wakristo kama vile Waislam walivyopambana na udhalimu wa Kikristo ndani ya ukoloni wa Waingereza. Dalili zilikuwa wazi kuwa harakati zilikuwa zimeenza na hazitakuwa kupitia TANU kwa sababu ndani ya TANU Waislam walikuwa wameshaanza kupigwa vita. Harakati hizi za pili zilikuwa ziwe chini ya umoja wa Waislam wote. Hii ilisababisha hofu kuu kwa serikali na kwa ajili ya woga ule ikawa imejiweka tayari kujikinga na jambo kama hilo lisitokee. Kwa ajili hii serikali ikawa inavamia kila Muislam aliyedhaniwa ni tishio kwa Kanisa. Ni katika hofu hii ndiyo maana hata historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika inaogopwa kuandikwa. Hii ni moja ya njia ambayo serikali inadhani inaweza kujikinga dhidi ya hisia za Waislam.

Wakati kundi lililojitenga kutoka EAMWS huku likiungwa mkono na serikali, likimshutumu Aga Khan kwa kuwa Muasia, hakuna aliyethubutu kuonyesha kidole kwa taasisi za Kikristo katika Tanzania zinazoongozwa na Wazungu na kufadhiliwa na mataifa kadhaa ya Ulaya. Hakuna aliyethubutu kuonyesha kidole kuelekeza kwa Kanisa Katoliki ambalo lina uwakilishi wa kibalozi wa Papa nchini Tanzania. Kwa kuwa inafahamika kuwa Kanisa Katoliki linalazimisha utiifu kwa Kanisa kutoka kwa waumini wake, na kwa kuwa Kanisa lina mawakala wake katika TANU na utumishi wa serikali, ingelikuwa ni Ukristo ambao ungehatarisha usalama wa nchi na wala si Uislam. Wakati Nyerere anawadhoofisha Waislam kwa hila za wagawe uwatawale, Wakristo walikuwa wanazidi kupata nguvu kila kukicha.

Hadi ilipofika mwaka wa 1970 vumbi la ëmgogoroí wa EAMWS likawa limetulia. Mwaka huo Nyerere alihudhuria semina kwa ajili ya dini na viongozi wa siasa. Semina hii kwa ujanja ilitayarishwa na Tanzania Episcopal Conference kamati ya juu kabisa ya Kanisa Katoliki inayotunga sera zote za Kanisa. Katika semina ile kwa mara ya kwanza hadharani Nyerere alizungumza kuhusu TANU na sura yake ya dini. Nyerere alisema ëChama chetu, TANU, hakina dini. Ni chama cha siasa tu na hakuna mipango au makubaliano na dini maalumí.[1] Maneno haya yanaweza kuwa na maana moja tu, nayo ni kuwa TANU jinsi miaka ilivyokuwa inapita, imepoteza taswira yake ya Uislam. Kuanzia mwaka 1954 TANU ilikuwa na dini na dini ya TANU ilikuwa Uislam. Historia ya TANU na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika ndiyo shahidi wa ukweli huu. Juu ya haya yote, Waislam wanakataa kudhalilishwa na serikali na Kanisa. Waislam hawajaacha harakati za kupambana na serikali na Kanisa kwa njia mbalimbali ambazo serikali inadai ni ëkashfa na matusií kwa Ukristo. Serikali imeshindwa kutuliza hasira za Waislam dhidi yake na dhidi ya Kanisa. Sababu ni kuwa wakati umebadilika. Waislam wamepoteza imani na serikali. Waislam hawaamini kuwa serikali haina dini. Waislam wametambua kuwa wanadhalilishwa na kunyimwa haki kwa kuwa serikali ni ya Wakristo. Salama yao na dini yao kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni, ipo katika kuondoa dhulma inayotawala nchi kwa kuwa hivi sasa Ukristo umechukua nafasi ya ukoloni.

Kusalitiwa kwa Maadili

Tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais, Nyerere aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam. Hotuba hii ilijaa simanzi, Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo. Wazee hawa wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono Nyerere wakati wa kudai uhuru. Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru. Nyerere alisema kuwa upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake:

"Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo. Sasa nipo katika hali ya kufarahisha kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama Mbunge mpya, Waziri, au Katibu Mkuu katika wizara zetu za serikali, ni Muislam au Mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho. Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna Wakristo wenye majina ya Kiislam, na Waislam wenye majina ya Kikristo. Kuvumiliana huku nyie ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu."

Hotuba hii ilikuwa ya ulaghai. Ukweli ni kuwa miongo mitatu baada ya uhuru Waislam hawajanufaika chochote wako katika hali ile ile aliyowaacha wakoloni au mbaya zaidi. Sivalon amefichua kuwa Kanisa limeweza kujenga himaya yake ambayo inahodhi asilimia sabini na tano za viti katika Bunge la Tanzania. Kati ya viti hivyo asilimia sabini vipo mikononi mwa Wakatoliki na vilivyobaki vimegawika kati ya Waislam na Wakristo wa madhehebu nyingine.[1] Baada ya kupatikana uhuru, Kanisa lilipohisi wasiwasi, limeweza kwa urahisi kabisa kuwazuia na kuwadhibiti Waislam. Serikali imeweza kutumia nguvu iliyokuwanayo katika kudhibiti siasa kuzuia harakati za Waislam kudai fursa sawa na Wakristo katika kugawana madaraka katika serikali. Kanisa limehakikisha kuwa kupinduliwa kwa ukoloni si kizingiti kwa Ukristo, ingawa ingetegemewa kuwa Kanisa lingedhirika kwa kuanguka kwa ukoloni. Katika miaka yake zaidi ya mia moja, Kanisa lilikuwa limestarehe kama muokozi wa nafsi na watu wenyewe. Kanisa lilikuwa salama na halikupambana na msukosuko wowote kutoka kwa serikali kwa kuwa lilikuwa Kanisa ndilo lilishika hatamu ya serikali.
 
LG: Si hivyo ndugu yangu mimi nataka na nyie mvae viatu vyetu muone sisi tunahisi vipi. Juhudi ya pamoja ndiyo hiyo wazee wetu waliitekeleza kuleta uhuru wa nchi hii. Soma historia ya Tanganyika uone ni akina nani waliokuwa bega kwa bega na Nyerere.

Hapa ndipo unapokosea. Sisi tukisoma hiyo historia tunawaona waislamu, wakristu, wahindi na hata wazungu. Wewe unawaona waislamu peke yao! Mtazamo kama huo sisi tunaona umeelemea zaidi kwenye udini kuliko kutafuta ukweli wa historia yetu.

Amandla.......
 
Umesema:
Uislamu nchini umerealise kuwa elimu ya kikoloni ni mali wakati jua limeshakuchwa na uhuru upo mkononi.
Kasumba ya kutothamini elimu hata leo ipo sehemu tofauti nchini palipo na imani kali. Kuoza na kuozwa baada tu ya kumaliza mafunzo ya madrassa hutawala badala ya juhudi kubwa ya ushindani wa kupata elimu ya darasani.
Sasa wenzetu hawa wanarudi nyuma kuulaumu ukristo na serikali kwa wao wenyewe kuchelewa kuchangamkia elimu kwa karne nyingi tu.
................................................................................................................................................................
Tangu huu mjadala uanze na wewe kujiunga sijasikia hoja yenye mantiki kutoka kwako.Zaidi unazungumzia umoja wa kitaifa na kwamba waislamu wajione wako sawa na wakristo.Kama nilivyosema awali waislamu wa sasa hawadanganyiki.Ukweli kuhusu historia ya TANU umetufunza mengi.Usawa munaozungumzia nyinyi ni huu wa mdomoni tu ambao tukibweteka nao mutatumaliza.Tunataka usawa uonekane kivitendo katika utendaji serikalini....tutaendelea.
Hapa Lole umejionesha wazi kwamba wewe si mtu makini katika huu mjadala.Hilo ulilozungumza ndio limekushushia hadhi yako mpaka chini kabisa.Unapozungumzia kuchangamkia elimu wewe unatutazama waislamu sisi watanzania ambao ni wahanga wa dhulma katika elimu tangu enzi za mkoloni,ambao kama si rehma za Mungu basi ingekuwa mumeshauzika uislamu Tanzania kwa ugonjwa wa kuwanyima waislamu elimu.
Wewe kweli unafahamu maana ya karne nyingi tu?.Huna habari kuwa waislamu kwa kuelewa kwao umuhimu wa elimu ndio waliowazindua mababu zako wazungu walioleta ukoloni Tanzania.Uislamu kusambaza elimu ni ibada na mafunzo ambayo hayako kwenye ukristo.
Hivi huna habari kwamba tabia ya wakristo kurudisha nyuma maendeleo ya kielimu ya waislamu haikuanza leo na jana?.Umesahau kuwa wakristo ndio waliochoma moto vitabu katika maktaba kule Iraq ya leo na kutumbukiza majivu yake kwenye mto Dijjla mpaka mto wote ukawa rangi ya wino kwa weusi.
Vitabu vichache vilivyopatikana ndivyo vilivyofikishwa kwa wazungu wako (wakoloni) halafu wakapata jeuri hii.

Wewe nahisi ni mpenzi wa sayansi na Physics kama mimi.Mara nyingi umerudia Newton's third law of motion Every Action has an Equal and Opposite Reaction.Hujui kwamba baba wa Physics ni Al-Hasan Ibn Al-Haytham (Alhazen).Yeye ndiye mvumbuzi wa namna jicho linavyofanya kazi.Uvumbuzi uliofuatia kuhusu camera kufikia hata photocopy machine visingewezekana kama si uvumbuzi wake.Kitabu chake Al-Manazir kilikuwa rejea muhimu kwa miaka mingi kuhusiana na somo la mambo ya mwangaza.

Tuseme umepatwa na nini hata ukasahau jinsi kanisa lilivyomfanyia mwanasayansi Galileo!.

Ukija katika uwanja wa somo la hesabu majina kama aljebra ni kutokana na mvumbuzi wake Muhammed Aljabry.Ukija kwenye kemia ndio usiseme kabisa.

Hii habari ni ndefu na kama ungekuwa makini ungewacha kutoa tusi hilo kwa waislamu.

Kuwa kwetu nyuma kielimu Tanzania ni kutokana na dhulma za mkoloni na Nyerere baada ya uhuru.
Zaidi kuhusu mchango wa uislamu katika elimu soma hapo chini kwa furaha.

1.Ushawishi wa Qur'an kuhusu elimu na uvumbuzi

2.Baadhi ya mifano ya michango wa waislamu katika kuipeleka mbele elimu.
Mkuu wewe saizi yako vijana wa madrasaa na primary kubishana nao.
My allegations still stand, period.
 
LG: Si hivyo ndugu yangu mimi nataka na nyie mvae viatu vyetu muone sisi tunahisi vipi. Juhudi ya pamoja ndiyo hiyo wazee wetu waliitekeleza kuleta uhuru wa nchi hii. Soma historia ya Tanganyika uone ni akina nani waliokuwa bega kwa bega na Nyerere.

Mkuu viatu vyenu tumevivaa kwa miongo mingi sana na ndio maana tunalilia uTaifa kama kitu pekee kinachotuunganisha, vinginevyo hatuna chochote cha kujadiliana hapa.
Kama si hivyo inabidi turudishiwe vyama vyetu vilivyohujumiwa vya Ushirika, Shule nyingi tu na vyuo vingi tu pamoja na mahospitali.
Hivi vyote vilitaifishwa ili kuleta uomoja.
Kama MS hulitambui hili basi inabidi uvikose na virudi kwa wenyewe na wewe uanze na vya kiislamu tu.
Kwa ujumla wazo lenyewe linalokuwa floated halina mantiki kwa Tanzania ya leo ya kutaka tu kuwafurahisha Islamic zealots wachache
 
LG: Ahsante sna kwa fikra zako kwa kweli kila kuchao unanielimisha. Nakushukuru kwa hili kulikuwa na mengi nilikuwa siyajui.
 
LG: Kauli yako ya kuwa mimi saizi yangu vijana wa madrasa na primary umenikumbusha sheikh wangu Maalim Haruna (Mungu amrehemu) akitufunza umuhimu wa tabia njema na kauli nzuri na vipi uwe unapokutana na kujadiliana na watu. Alikuwa anasema wewe silaha yako ni huo unyenyekevu na elimu kwa lile unalojadili. Akasema tabia njema ni hazina kwani itakufaa duniani na akhera.
 
Sawa kabisa Mkuu Mohammed Said , lakini na mimi nimeweka msimamo kuwa hapa hatujadili dini bali udini, au kwa lugha nyepesi hatujadili Uislamu bali mazingira yaliyotawala kihistoria wakati wa Uhuru kama mada inavyosema.Sasa mtu akileta quote toka Quran tukufu ambayo mimi sisubscribe ingawaje naiheshimu , basi hapo si saizi yangu wala muelekeo wa mjadala.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom