Hivi hujawahi kuona au kusikia watu wanalipa hela kuangalia maigizo au mazingaombwe?
Kwenye Cinema Hall watu wanajua kabisa movie hazina uhalisia lakini wanalipia kabisa kuangalia, ni kawaida Mkuu.
Hata wacheza sinema wa Hollywood wanalipwa pesa ndefu, WWE(World Wrestling Entertainment) ni maigizo tu. Kuwa 'Entertainment' na si 'Sport' au si 'Competition' ina maana ni burudani tu na si mashindano halisi wala si sport.
[emoji116]
Finamu zimejisajiri Kama kazi za Sanaa za Maigizo.
Na waigizaji wake wanajulikana Kama
WASANII.
Mieleka ni Michezo halisi hata hapa Tanzania uliwahi kuchezwa na wachezaji Kama.
Power Mwanza
Power Bernardo
Power Shaka Zuru
Power Vuru Mroma
Power Ruvuma
Nk.
Na baadae mchezo wa Mieleka hapa TZ ukafungiwa kutokana na kukosa vigezo vya kimataifa vya kulinda usalama wa wachezaji.
Yaani
Palikosekana madaktari na matibabu ya uhakika ya wachezaji.
Palikosekana Jukwaa salama la kuchezwa Mieleka ambalo litawalinda wachezaji ( Jukwaa moja linakalibia TSH 1.bn)
Palikosekana mdhamini wa kuuendesha pambano katika viwango vinavyokubalika kimataifa.
(Kabla ya pambano la ngumi huwa mnaona mabondia wanakutanishwa ili kujitambulisha. tulio hilo linaweza kubeba mambo mengi na hata mabondia kuzichapa kavukavu kama hawazuiwa.
Katika mieleka tukio hili lipo pia, na ndipo hapo mnapoona kama Maigizo kwani katika utambulisho wachezaji wa Mieleka huwa wanakuja na wapambe wao na zinachapwa Kama kawaida na wapambe wanaingilia pambano Kama kawaida.
Au linapangwa pambano la kujitambulisha ambalo mchezaji mhusika mmoja anacheza na asiye husika, mhusika akikaribia kushinda ndipo mshindani sahihi anakuja kuingilia pambano na kumpinga mshindani mwenzake.)
Tazameni pambano la mieleka la mtu na kakake
Yaani Jeff Hard na Mark Hard lilivyoandaliwa mtaelewa.
Jeff hakutaka kucheza na kakake Hard.
Na Hard aliandaliwa pesa nyingi ili amchokoze kakake hadi wacheze kwa ahadi ya kulipwa pesa nyingi kwani wadau walitaka ndugu hao wacheze.
Mambo haya yanafanyika ili kuvutia watazamaji wengi kuingia mchezoni na kupata pesa.
MIELEKA SIO SANAA NA USANII NI MCHEZO HALISI NA WADAU WAKE TUPO
Asiyeelewa aende akaulize Baraza la Michezo Tanzania.
BMT.