Ukweli ni kwamba wanaoamini kuwa utawala huu utakuja kupendwa na Watanzania, wamenyimwa hekima kabisa.
Ebu fikiria, hivi ni nini unaweza kukifanya ambacho ni mbadala wa uhai wa binadamu? Mwanadamu mkamilifu, hata awe maskini kiasi gani, ukimpa chaguo, achague aendelee kuishi kwenye umaskini wake, lakini akiwa na wanawe, wazazi wake, ndugu zake na majirani, AU watoto wake au wazazi wake au majirani zake wauawe ili yeye apewe pesa nzuri na mali nyinginezo, ni dhahiri atachagua aendelee kwenye umaskini wake lakini wanawe, wazazi wake na majirani zake waendelee kuwa hai.
Huo ni uthibitisho kuwa hakuna kilicho mbadala wa uhai wa mwanadamu.
Fikiria mtu ambaye mtoto wake, kaka au dada yake, mama au baba yake, waliuawa na watawala mwakajana, wengine hata maiti za wapendwa wao hazijaonekana mpaka leo. Lakini pia wapo majirani wa waliopoteza wapendwa wao, lakini na watanzania kwa ujumla wanaothamini uhai wa wanadamu wenzao. Hivi hawa, utawafanyia nini hata wasahau mauaji ya wapendwa wao, halafu siku moja wageuka na kukushangilia wewe uliyewaua ndugu zao? Kwa mtu mwenye akili, hakika nasema, haitatokea wanafamilia, majirani na watanzania kwa ujumla eti kuna siku watawasahau ndugu zao waliouawa hovyo, halafu wakawashangilie watawala waliofanya mauaji yale ya mwaka 2025! Huko ni kujidanganya na kukosa akili ya tafakari.
Laiti watawala hawa wa sasa waliofanya mauaji yale wangeijiwa na hekima japo ndogo, ilikuwa ni vema wangekuwa wamejiondoa, wakaja wengine, ambao sasa wangefanya kazi ya kuponya majeraha. Lakini kwa hawa waliofanya mauaji, ni ngumu sana kuipoza mioyo ya watu iliyovunjika. Kadiri wanavyolazimisha na kung'ang'ania madaraka, wanazidisha chuki dhidi yao kutoka kwa wananchi, kwa kila siku ipitayo.
Mataifa yanayoongozwa na wenye hekima, kiongozi anaweza kufanya kosa dogo tu, wananchi wakalalamika, kiongozi anaamua kuachia nafasi na kukaa pembeni. Lakini huku kwetu, sijui kuna laana gani!! Watawala wanafanya uharamia wa kutisha kwa kiwango cha ajabu, kuua wananchi kwa maelfu, lakini wote wapo kimya wakisubiria na kuamini kuwa wananchi watahadaiwa na kuwasahau ndugu zao.
Tunaomba Mungu aturehemu, kama kuna mahali tulimkosea, naye akaamua kutuadhibu kwa kutupatia watawala katili, tunaomba atusamehe kwa mabaya yote tuliyoyatenda.