Ukweli mchungu ambao Pro NATO Huwa hawapendi kuusikia

Ukweli mchungu ambao Pro NATO Huwa hawapendi kuusikia

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Urusi kushindwa kutawala anga la Ukraine.
memba mmoja wa JF T14 Armata,hupenda sana kuelezea swala hili la kumiliki anga.
Yeye hupenda kusema Urusi haitumii mtindo wa kumiliki anga kama vile ifanyavyo USA.
Yeye huona kama huo ni udhaifu kwa Urusi na uwezo kwa USA.

Lakini Mimi Nina maoni tofauti na yeye.

Kwangu Mimi najiuliza je ni anga lipi ambalo USA anasifiwa kulimiliki?
Naomba tusizungumzie vita kati ya USA na Vietnam.

Ni vita Gani kubwa baada ya Vietnam USA alipigana?
Je alimiliki anga la nchi Gani ambayo tunaweza kumsifu kuwa kamiliki anga?.

Vita alizopigana baada ya Vietnam ni vita kati ya USA na Panama,Iraq na Afghanistan.

Sasa tuziangalie nchi hizo.
Je ni sahihi kwa Pro USA kujisifu kua USA kamiliki anga la Panama?
Anga la Afghanistan? Na anga la Iraq?
Je hizo nchi tatu nilizozitaja Zina vifaa vya kutosha kukabiliana na uwezo wa jeshi la anga la USA?
Je USA inaweza kujisifu kukamata anga la Iraq,ama la Afhanistan ama la Panama?.

Tutoke hapo.
Je USA ilikwenda peke yake kupigana na kukamata ma anga ya Afhanistan na Iraq?
Je wale waliokua wakiitwa USA na washirika wake waipiga Iraq au afghanistan ni akina nani?
Maana sio Siri USA alienda kuzipiga Iraq na Afghanistan akiwaalika wale wanaoitwa washirika wake,ambao wengi wao na wenye nguvu ni Wanachama wa NATO.
Mfano UK,France,German,Poland n.k.
Na kwa bahati nzuri wako vizuri kijeshi katika baadhi ya maeneo kuliko USA mwenyewe.
Yaani tuseme Kila mmoja wao ana uwezo Mzuri kuwashinda wenzake,mfano UK,France na germani Kuna vitu vya kimedani wanamshinda USA.na ushahidi uko wazi.
Sasa kwa point yangu naweza kusema kuwa USA ambae anasifiwa kumiliki anga,humuliki anga za nchi dhaifu sana kiulinzi wa anga kwa kusaidiwa na nchi kubwa kijeshi zenye uwezo mkubwa sana katika vifaa vita vya ardhini,majini na angani.uk,France na german.nk.
Je ndo wanaweza kujisifu kwa lipi?

Je Afhanistan ya Watalaban wakishirikiana na al qaida walikua wanaulinzingani wa anga ambao USA anasifiwa kuutawala?

Vivyo hivyo kwa Iraq ambayo angalau kidogo ilikua Ina uwezo mkubwa kijeshi kuliko Afghanistan.
Lakini je Iraq ilikua inaweza kuzisumbua ndegevita aina ya Rafale,Mirage, Jaguar,tonado na ndege nyinge za USA,UK na France kwa pamoja?
Iraq ilishambuliwa kwa ushirikiano
wa USA na nchi nyingi sana wakati yenyewe (Iraq ikiwa haisaidiwi na nchi yoyote hapa duniani.)hakuna hata nchi moja ya Ulaya wala Asia iliomsaidia iraq.hata kama ingekuwepo yenye Nia ya kumsaidia Sadam,ni mbali Sana kutoka ulaya kupeleka misaada Iraq.
Tutafakari hapa.

Ukweli mchungu.
Kinyume chake Ukraine inapigwa na Urusi huku ilipewa Kila aina ya misaada ya kijeshi na kivita kutoka nchi karibu zote za west na zaidi nchi za NATO.
Ukraine Iko karibu sana na nchi za west kwa mipaka.ni rahisi hata kusafiri kwa bodaboda kutoka Ukraine kwenda Poland na kwenda german.sio rahisi hivyo kutoka ulaya kwenda Iraq.
Wakati Ukraine ikipata silaha Bora kabisa ambazo kama Iraq angekua anazipata,huenda historia ingesomeka vingine Leo hii.

Wakati huohuo Ukraine ikiendelea kumiminiwa silaha Urusi haisaidiwi na nchi yoyote hapa duniani,
Urusi imewekewa Kila aina ya vikwazo ambavyo viliwekwa kwa makusudi kabisa ili adhoofike ili aweze kushindwa kugharamia vita ama wananchi wake walote ghasia huko kwao ili kuiangusha Serikali ya Putin.
Hivyo utaona kwamba Urusi inapigana na nchi iliyokua na uwezo mara kumi ya uwezo alipokua nao Iraq ya Sadam Hussein.
Kabla ya OP hii ya Urusi Ukraine alikua ana uwezo kijeshi mara kumi kuliko Iraq ya Sadam.
Ukraine Ina viwanda vya silaha,Ina wanasayansi Bora kabisa wa masuala ya silaha na Jeshi,in technolojia na silaha nyingi mno.

Ukiongeza na hizi zinazoingizwa na west NATO ambazo baadhi ya nchi za NATO zimelalamika kuwa Hadi zimeishiwa na akiba zao za silaha.

Kwa muktadha huo Urusi kwa kujua ukaribu wa mipaka kati ya Ukraine na nchi Wanachama wa NATO,nankwa kujua tabia za Wanachama wa NATO kama USA kuwa itaisaidia Ukraine silaha Bora kabisa za kuangusha ndege zake,Urusi ikaona Haina haja kupoteza ndege nyingi na marubani wengi,ikaamua kuja na mtindo mwingine wa kuivamia.
Hata hivyo,sio kwa kua USA huja na mtindo huo na Urusi nayo ije na mtindo huo na ndio tofauti za kimapigano kati ya nchi na nchi.
Na kwa kuwa Urusi ana uwezo kijeshi? Na ana uwezo wa kuingia kwa njia mbadala ndio maana kaja kivingine.

Urusi ikiwa imewekewa vikwazo,na ikiwa inapigana peke yake,inapigana na nchi inayosaidiwa na umoja mkubwa sana wa kijeshi hapa Duniani,na inawamudu vizuri tu.
Kwa ukaribu wa Ukraine kimipaka na nchi za NATO ni rahisi sana kuingiza silaha hata kwa njia za panya.silaha ambazo zitapunguza utawala wa anga la Ukraine.

Vipi Leo hii kama Ukraine isingekua inapata silaha kabisa kutoka west.

Na vipi kama Libya na Iraq zingepata silaha kutoka Urusi,china na nchi washirika kutoka Asia?
Kwa Nini hatutaki kukubali ukweli kuwa Urusi ni ngangari?

Nchi moja inapigana na nchi zaidi ya 30?hata kama ni indirect?

Kumbuka USA ilipigana na Vietnam,nayo Vietnam ikpewa misaada na akina china,Korea na Urusi, ni Nini kiliipata USA?

Kwa nini Ukraine inapata misaada mingi TU lakini bado inazidiwa?

Wala USA haikuwekewa vikwazo,lakini Urusi imewekewa.

Majasusi Bora kabisa wa USA UK Fr German n.k wakionesha Ukraine wapi pa kupiga na Nini Cha kufanya,lakini majasusi wa Urusi peke Yao wanaendesha Op hii.

Kwa mara ya kwanza tumeshihudia waumini wa uhuru wa habari USA na west wakiminya uhuru wa habari.
Vyombo vya habari vya Urusi vimedunviwa visioneshe matangazo Yao huko west na sehemu nyingine.
Sasa unajiuliza ni kwa sababu Gani.
Je walijua Urusi itakua inafanya vizuri vitani hawataki watu wao wauone uewzo wa Urusi kijeshi?

Je kama Urusi Ingekua inazidiwa kijeshi huko uwanja wa vita wangeendelea kuzuia?
Je isingekua sahihi kuachia matanagazo ili raia wa Urusi na wengine duniani waone jinsi Urusi ilivyo dahifu kijeshi mbele ya Ukraine?
Je Urusi kuzidiwa na kuonyeshwa kwenye TV zao si ndo Ingekua silaha muhimi kwa NATO dhidi ya Urusi?
Kuleta machafuko Urusi?
Lakini jibu ni kuwa ukiona wamezuia ujue maana yake wanaujua fika uwezo wa kijeshi wa Urusi hawataki Dunia iutambue na kuujua,kwani waliwaaminisha watu kua wao ni Bora na Urusi ni dhaifu kijeshi na kiuchumi.

Tumeshuhudia vita nyingi sana lkn hatujawahi kushuhudia mdororo wa kiuchumi namna hii kwa nchi za west na duniani.

Ukraine inapigania nchi yao ardhi Yao na watu wao.ni sahihi kabisa,ndio maana wanapigana kufa na kupona,ni halali kabisa kwao ndivyo ilivyo,lkn bahati mbaya wanapigana kwa kutegemea msaada wa silaha kutoka Kwa majirani na marafiki,bahati mbaya,wanapigana na mtu mwenye silaha zake asietegemea kutoka Kwa mtu yoyote,anabuni mwenyewe,anazalisha mwenyewe na anatumia mwenyewe.

Pro NATO USA haikuwahi kutawala anga,kama ilitawala,ni anga la nchi dhaifu sana Tena akiwa pamoja na marafiki zake wakubwa sana hapa duniani.
Anga la Ukraine na mabosi wake ni tofauti na anga la Afghanistan,Libya na Iraq.
Ni vitu viwili tofauti kabisa kujisifu kutawala anga la Libya, Afghanistan na Iraq.
 
Mkuu umekula ugali mapema sana maana umepata wapi nguvu ya kuandika malalamishi badala ya hoja,sasa hivi dunia inapitia kwenye hali mbaya ya uchumi embu tuache mambo ya kushabikia vita tujenge hija zenye tija ,dunia imekumbwa na misukosuko mingi sana kipindi cha 2021 had 2022 hivyo pambana ujikwamue kiuchumi ,yaani unaandika maandishi kitabu hakuna la maana uliloandika
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mkuu umekula ugali mapema sana maana umepata wapi nguvu ya kuandika malalamishi badala ya hoja,sasa hivi dunia inapitia kwenye hali mbaya ya uchumi embu tuache mambo ya kushabikia vita tujenge hija zenye tija ,dunia imekumbwa na misukosuko mingi sana kipindi cha 2021 had 2022 hivyo pambana ujikwamue kiuchumi ,yaani unaandika maandishi kitabu hakuna la maana uliloandika
 
Ukraine inapigania nchi yao ardhi Yao na watu wao.ni sahihi kabisa,ndio maana wanapigana kufa na kupona,ni halali kabisa kwao ndivyo ilivyo,lkn bahati mbaya wanapigana kwa kutegemea msaada wa silaha kutoka Kwa majirani na marafiki,bahati mbaya,wanapigana na mtu mwenye silaha zake asietegemea kutoka Kwa mtu yoyote,anabuni mwenyewe,anazalisha mwenyewe na anatumia mwenyewe.
... kwa hiyo ilitakiwa Ukraine afanyeje labda? Mngetamani kweli kuona Ukraine iki-surrender ili mu-justify supremacy ya dikteta Putin furaha zenu zitimie au sio? Kwa hakika kama Mungu aishivyo, Russia haitokaa iitawale Ukraine hupendi kanywe sumu!
 
Ndio tatizo la kuhamasisha ushoga hadi jeshini, leo hii hata US US akiingia vitani na Somalia ataomba msaada kwa washirika wake. Nguvu ya US ipo kwenye "ushirikiano" wao binafsi ni waoga mno, ila wana mbwembwe balaa.

Vita ya US na Vietnam iliwafunza akili, kamwe hawatarudia kuingia nchini kwa watu wakiwa alone, sasa pale Ukraine Nato wote wanapeleka silaha, kuna maajabu gani? Us ni jina kubwa kwenye vyombo vyao vya habari.. ila uhalisia ni wepesi kama manyoya.
 
Ukweli mchungu
 
Mkuu umekula ugali mapema sana maana umepata wapi nguvu ya kuandika malalamishi badala ya hoja,sasa hivi dunia inapitia kwenye hali mbaya ya uchumi embu tuache mambo ya kushabikia vita tujenge hija zenye tija ,dunia imekumbwa na misukosuko mingi sana kipindi cha 2021 had 2022 hivyo pambana ujikwamue kiuchumi ,yaani unaandika maandishi kitabu hakuna la maana uliloandika
Kwako wewe unaona sio ya maana,lkn Mimi hayo ndio maoni yangu.
Dunia nzima watu wanafatilia mgogoro huu,na wanatoa maoni Yao kama nitoavyo.
Wachambuzi mablimbali wanachambua juu ya mgogoro huu.
Dunia inapitia kipindi kigumu kwa hiyo tuacha kutazama ama kusikiliza ama kusoma habari kutoka vyombo vya habari kwa sababu tutaonekana tunashabikia vita.
Unajua maana ya kushabikia?
Unasema nitafute kujiongezea kipato,kwa hiyo unakijua kipato changu Cha Sasa?
Ungekua una akili na maarifa kama unavyojinasibu nadhani wala usingekua katika jukwaa hili ukisoma michango mbalimbali,huo muda umeutoa wapi.
Kwa hiyo kwa sababu Dunia inapitia kipindi kigumu,tujifungie ndani tuomboleze?
Majenerali wakubwa duniani,wasomi na wanasiasa maarufu wanaizungumzia vita hii kwa mitazamo tofauti,wewe ni nani Hadi uzuie watu wasitoe maoni Yao.
Huna lolote,huna mbele wala nyuma,huna msaada kwa taifa wala familia unayotoka unajifanya una akili ilhali umeshindwa hata kutokomeza umasikini katika ukoo wako.
Jifunze kujibu hoja kwa hoja na kuheshimu mawazo ya wenzako.
 
Achana na uwezo wa anga wa marekani, Kitu F-35, B-52, Ni vitu hatari sana
Waserbia walitandikwa non-stop kutoka angani hawawezi kusahau zile mvua
 
Binafsi naamini Kuna mambo Yako planned ktk vita na matokeo yake Huwa yanajulikana.
Siamini kama hawa viumbe ni maadui kwani wana ushirika mkubwa ktk mambo nyeti.
Huenda baadhi ya jamii kama Africa na Arabs zitapumbazika huku wao wakisonga mbele.
 
Achana na uwezo wa anga wa marekani, Kitu F-35, B-52, Ni vitu hatari sana
Waserbia walitandikwa non-stop kutoka angani hawawezi kusahau zile mvua
Wanashindwa nini kufanya hivyo Ukraine.. Wakati mwingine natamani sana kujua bongo za watu. Maana nashindwa kuelewa wengine huwa wanawaza Kwa kutumia nini?
 
Wanashindwa nini kufanya hivyo Ukraine.. Wakati mwingine natamani sana kujua bongo za watu. Maana nashindwa kuelewa wengine huwa wanawaza Kwa kutumia nini?
Vita ni hatua, joto linapandishwa taratibu taratibu.
Sasa hivi Waukraine wanatreiniwa kutumia F-16, kadri vita itakavyoendelea ndo madude yatakapoanza kutolewa kimoha baada ya kingine
 
[emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji635][emoji1787]
GridArt_20220717_114245399.jpg
 
Back
Top Bottom