Ukweli mchungu: CHADEMA inapoteza Tena hili la Viti maalum

Threads zingine ni michosho tupu, hao covid 19 hata wakiwa wabunge wa mahakama kwa chadema sio tatizo, shida ya chadema ni kuonyesha supporters wake kuwa haihusiki na haijabariki uhuni huu full stop!
Huna sappoters wewe na Kama ungekuwa viongozi waliposema muandamane mngejitokeza
 
Thread sio michosho hapa chadema ndio michosho hivi chama hakina wachunguzi wake mpaka inafikua wanachama 19 wanajikusanya na kufika dodoma bila uongozi kuwa na taarifa hiki chama bure kabisa
Kwa akili ndogo unahisi chama kilikuwa hakifahamu, kama toka Nov 3 kigogo alilifahamu hili sembuse chama? Kitu kimoja usichokifahamu hata mie Leo nikifahamu kuwa wiki ijayo umedhamiria kuachana na mmeo, kitakochoweza kuzuia tukio hilo ni dhamira yako kughairi au Mimi nikuue, sasa ulitaka chadema iwauwe hao covid19 ili wasiende kuapa wkt nafsi zao zilidhamiria hivyo?
 

Tunataka tupoteze zaidi. Tuna uhakika na wananchi na wananchi wanauona upuuzi wote.
 
Huna sappoters wewe na Kama ungekuwa viongozi waliposema muandamane mngejitokeza

Huwezi kupima support kwa njia ya maandamano kwenye kundi la wananchi waoga. Support nzuri tumeiona wakati wa kampeni. Na kwenye box la kura tumeuona uhuni wote wa jiwe wa matumizi mabaya ya madaraka.
 
Huna sappoters wewe na Kama ungekuwa viongozi waliposema muandamane mngejitokeza
Sapotaz wapo wengi sana ila hakuna aliyetayari kwenda kwenye maandamano yanayotawanywa kwa risasi za moto, ni bora mkwere alitawanya kwa majiwasha na mabomu ya machozi sio huyu katili wa kihutu!
 
Inapendeza Sana kama Chama kitajiendesha kama taasisi huru....hakuna atakae kuwa mkubwa kuliko Chama.... katiba ndio itumike kuendesha chama...watu watakuja na kuondoka....yeyeto anaeenda kinyume cha katiba ahukumiwe kwa kufuata katiba.,...hii ya kukimbilia mahakamani waachiwe wawo...ni haki yao pia...cha msingi katiba na heshima ya chama ilindwe kwa nguvu zote.
 
Yaani ndugu Mimi nimesema tu ukweli mchungu kuwa hii mbugi chadema hawatoboi... Haina maana naunga mkono!
 
Halafu huwezi jua mdee 'iron' lady pamoja na wenzake wameahidiwa Nini!

Maana kutoka kuvunjwa mkono plus kuibiwa Kura halafu ghafla tu watu wanaibukia mjengoni huwezi jua,
Labda tusubiri sapraizi nyingine?
Hapa umenena kitu. Ni kweli hatuwezi jua walichoahidiwa
 
CHADEMA haina viongozi makini bali inaendeshwa na losers na negative minds waliojazana mitandaoni!
Si ajabu wakatoa uamuzi wa kuwafukuza akina Halima Mdee. Acha wakate mti walioukalia!

We ulitakaje? Wasaliti waachwe?
 
Thread sio michosho hapa chadema ndio michosho hivi chama hakina wachunguzi wake mpaka inafikua wanachama 19 wanajikusanya na kufika dodoma bila uongozi kuwa na taarifa hiki chama bure kabisa
kama movement ilipangwa na watu wa juu yao zaidi ? we unajuaje kwamba hawana intelijensia yao ?
 
Yaani ile tu kwamba serikali ya JPM imejikuta inafanya upuuzi wa aina hiyo na kiwango hicho, tayari ni ushindi mnono kwa CHADEMA. Kwa vipi?
1) ni ushahidi kwamba wamejikuta kwenye kona mbaya sana. Swali ni je, waliingiaje kona hiyo? Jibu ni kwamba magumashi ya uchaguzi yalikuwa kiwango cha kufa mtu. Kama wao wanaamini kwamba ushindi wao ulikuwa halali, kwa nini wahangaike? Basi kumbe hata nao hawaamini wameshinda kihalali.

2) badala ya kushangilia kwamba wamefaulu hatimaye kuondoa "uchafu" bungeni, kumbe sasa wanahangaika kuurejesha "uchafu" huo?

3) sasa hivi utamu wooote wa ushindi, kama ulikuwepo, sasa hakuna. Jumuiya ya kimataifa ndio kabisaaa hawatatuelewa. Najua wapo wanaodhani Magufuli hajali wengine wanasemaje. Kama ingekuwa hivyo, Magu asingeharakisha kuteua waziri wa mambo ya nje tena kwa kukiuka katiba. Macho yote nje wanasemaje
 
Yani CHADEMA nilikuwa nakiamini na kukipigania,but sasa ni chama cha hovyo kabisa.Nitakaa tu bila ufuasi wowote ule
 
Yaani kwa hili unajiona una akiliiiiiiiii
 
Muda ni mrefu sana (miaka mitano) Ndugai hawezi kuwalinda kama akina komu ila atawalinda kwa njia tofauti.Watakwenda Mahakamani na mahakama itaendesha hiyo kesi miaka mitano au mahakama itaamua wameshinda na warudishiwe uanachama na wakati kesi ikiendelea Ndugai atasema waendelee na ubunge.
 
Kuwaacha chadema itadharaulika na kufariki kama CUF ya Lipumba lakini wakifukuzwa chadema itaheshimika zaidi na kupata wafuasi wapya wazuri zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…