The Six Triple Eight
New Member
- Dec 29, 2024
- 2
- 80
Majina yangu ni Johannes Ignatius Rwebangira, mzaliwa wa kijiji cha Bisheke, Kata ya Mubunda, Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera. Baba na Mama yangu wote wakiwa wazawa wa kijiji hiki pia, hivyo hapa ni nyumbani.
Mwaka 1994, nikiwa na umri wa miaka miwili (2), ndipo safari ya hadithi ya maisha yangu ilipoanza ambayo ni tamu kuisikia lakini chungu kuiiishi. (NITARUDI HAPA)
Nyumbani kwetu tumezaliwa watoto watano (5), wawili wa kiume na watatu (3) wa kike, mimi nikiwa mzaliwa wa nne (4), na bahati nzuri Mungu ametuweka wote hai. Baba na Mama yetu walikuwa ni wakulima na wafugaji wadogo kikijini, waliishi maisha ya kawaida sana, yasiyo na fahari. Maisha hayo waliyaambukiza kwa watoto, kwani tangu darasa la kwanza mpaka la saba wote tulisoma shule ya msingi ya kijijini Bisheke, tena bila viatu na wakati mwingine bila madaftari.
Mwaka 1994, watu wengi jamii ya Wanya-Rwanda walikuja kijijini kwetu, walikuwa ni wakimbizi jamii ya Watusi, baadae nilikuja kufahamu kwamba walikimbia Vita ya wenyewe kwa wenyewe miaka hiyo.
Binti Mmoja Mrembo (Dada Nshime) wa Kinya-Rwanda alipokelewa nyumbani kwetu na kupewa hifadhi na mama yetu akawa kama msaidizi wa Kazi. Binti yule alikaa kwetu kama ndugu, japo alikuwa anasaidia kazi za nyumbani na Shambani kwa malipo kidogo kila mwezi. Dada Nshime alitupenda sana, sikuwahi kujua kama sio dada yetu mpaka nilipopata ufahamu wa kiutu uzima. Mwaka mmoja baadae Dada Nshime alijifungua mtoto wa kike palepale nyumbani, baba wa mtoto huyo hatukuwahi kumfahamu mpaka dada Nshime alipo tuacha. Nakumbuka Dada Nshime Aliondoka nyumbani mwaka 1997, kwa kutoroka bila kuaga japo baadae sana tulikuja kujua kisa cha kuondoka kwake, na "ndio msingi wa simulizi hii ya maisha yangu."
Maisha yaliendelea, nilimaliza elimu ya sekondari (kidato cha 4) mwaka 2011, Katika shule ya Sekondari ya Mubunda, safari yangu ilikuwa ni ngumu sana kwani nililazimika kuhairisha masomo mara kadhaa, hivyo kuchelewa kumaliza kwa miaka miwili. Mungu si Athumani nilifaulu vizuri na kuchaguliwa kujiunga na Shule ya Advance Sekondari ya Ihungo Mjini Bukoba.
Mwezi January Mwaka 2012, Baba yetu ambaye alikuwa ni mlevi wa pombe na sigara sana, alianza kuumwa tumbo sana, tulimpeleka hospitali ya mission ya Rubya, wakagundua ana Kansa ya Inni, ambayo ilikuwa imesambaa sana. Baba alikaa kama wiki tatu hivi hospitalini na baadae ali aaga Dunia Mwezi wa Tatu mwaka huo huo nyumbani Bisheke.
Nilienda Advance Sec. kwa unyonge sana, kwani pamoja na ulevi uliopindukia wa baba, kitu kiomoja ambacho nitakikumbuka daima, ni upendo na kujali kwake familia na watoto wake.
Mungu alinisaidia, nikafaulu mtihani wangu wa NECTA wa advance, na kuchaguliwa katika chuo cha Uhandisi (COET) ktk Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Mwaka 2014. Nilifurahi sana, na kidogo nikaanza kuona ndoto zangu zinaenda kutimia.
Mwezi wa November, 2014 nilijiunga rasmi na chuo kikuu cha Dar Es Salaam na kupangiwa hostel main campus, hall 5, floor ya 6 chumba namba nimesahau. Kwa mara ya kwanza nilikanyaga Dar, sikuwahi kudhani kwamba mshamba mimi wa kijijini naweza kufika DSM.
Course niliyochagua ambayo ndio fani yangu mpaka sasa ilikuwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza 35 tu, kati ya hao wanaume 27 na wanawake 8 ambao miongoni mwao watano walikuwa wametoka Rwanda kwa ufadhili wa serikali yao. Hivyo basi Darasa letu lilikuwa na Wanya-rwanda watano wa jinsia ya kike.
Binti mmoja wa Kinya-Rwanda alijitambulisha jina lake kama Herrieth Shimeimana, binti huyu alikuwa ni mzuri sana, mrefu mwenye rangi ya maji ya kunde yaliyo pauka, umbo lake lilimvutia mpaka Tutorial Assistant wetu aliyemnyanyua na kutaka ajitambulishe alipokuwa anajibu Swali.
Baada ya Kipindi kwa kujikongoja na kujitaidi sana, nilijaribu kumsalimia Herrieth bila mafanikio kwani alikuwa na marafiki wengi wa kiume watoto wa mjini ambao pengine walikuwa na muonekano mzuri kuliko wangu.
Binti Herrieth sikuwahi kuongea naye hata neno moja kwa mwaka wa kwanza wote kwani vipindi vingi vilihusisha first years wa course zote za COET, hivyo ilikuwa ni ngumu kumpata, na isitoshe nijiona siko kwenye League yake. Binti alikwa mzuri haswa.....
Mwaka wa Pili ulianza kwa shida kidogo, kwani nilikosa hostel Main Campus na Mabibo Hostel. Nililazimika kupanga chumba kidogo sana Msewe, karibu na hospitali ya Masista kwa mama mmoja hivi ambaye alikuwa ni Nurse pale chuoni. Alikubali nimlipe kwa mwezi mmoja mmoja mpaka pale hali yangu itakapo tengamaa. Pia nilipata shida ya mkopo kwani jina langu halikuonekana kama nina stahili mkopo, kwa kifupi, semester ya kwanza mwaka wa pili ulianza vibaya sana kwangu.
Masomo yalikuwa ni magumu kweli, group discussions nyingi nilikuwa nazikosa, muda mwingi nikishinda ofisi za bodi ya mikopo Mwenge kushughulikia issue yangu. Test za kwanza kwa ajili ya Course work nilifanya vibaya sana na nikajiona nisipokuwa makini mwaka huo sitoboi.
Siku moja Usiku, nikiwa nimechoka baada ya kushinda Bodi ya Mikopo, tena bila mafanikio, nilipokea wa sms kwenye simu yangu ya kitochi, " We need to meet tomorrow morning around 8:00AM, Vimbwetani COET, we have an assignment to attend together" sms hii niliipotezea na kuona ni ujinga kwani nilianza kukata tamaa na shule, kumbuka hapa bado sijalipa ada, na UE zinakuja, hivyo niliona ni kheri nipambanie mkopo kuliko kufanya assignments hivyo sikujibu chochote.
Saa 8:30 AM asubuhi nikiwa kwenye daladala kuelekea Mwenge (Bodi) nilipigiwa na simu ngeni, ilikuwa ni simu ya binti akiniuliza niko wapi, "Johannes where are you", nilimjibu "Wewe ni nani?" ..........."Its Herrieth, i sent you a text yesterday about our assignment, deadline is today around noon", kwa mara ya kwanza nilisahau kama nina matatizo ya mkopo na deni la mwenye nyumba, "Herrieth i`m on my way coming, give me 15 minutes" nilihamaki na ghafla nilishuka kwenye daladala na kukimbia COET kwani ndio kwanza tulikuwa tunatoka kituo cha Utawala.
Group discussion ilienda vizuri, japo kwa upande wangu bado nilikuwa na mawazo sana, naweza kusema wenzangu walifanya kwa niaba yangu. Kwa mara ya kwanza nilifanikiwa kuwa na ukaribu na Herrieth, binti alizidi kupendeza machoni mwangu, alikuwa faraja ya mateso na shuruba niliyopitia, kila nikimuona ninaomba hiyo ndoto ninayoiota iwe ni kweli. Maskini mimi, sikujuwa kwamba nilikuwa naota ndoto mchana tena nikiwa sijalala.
Wiki moja kabla ya Mtihani wetu wa mwisho yaani UE, bado mambo ya mikopo yalikuwa yameshindikana, nilifanya kila nililoweza bila mafanikio, ofisi ya Dean of Students walisema hawana budget hiyo, viongozi wa dini walisema wana request kama hizo nyingi, nikaanza kupata mawazo ya kuhairisha mwaka, nirudi nyumbani nifanye kazi nitafute ada, kwani Mama yangu alikuwa hajiwezi kabisa, ndugu zangu karibu wote wana matatizo yao na mdogo wangu yuko advance anategea kutunzwa.
"Ndugu zangu leo naomba niwaage", haya yalikuwa ni maneno yangu ya utangulizi kwa wanafunzi wenzangu baada ya kipindi nilipokuwa nawaaga kwani tayari nilishaandika barua ya kuhairisha mwaka. Niliwaeleza matatizo niliyopitia semester nzima, kwamba wakati wao wana hangaika na shule, mimi nilihangaika na daladala, kuingia na kutoka kwenye maofisi ya watu kutafuta msaada. Jumla ya Ada illyohitajika kwa Semester ile ni 750,000.00, hivyo hata kwa wanafunzi wenzangu ilikuwa ni changamoto.
Nikiwa mnyonge sana, tena niliyekata tamaa, nikielekea ofisi ya principal wa COET ku submit ile barua, nilipata simu kutoka kwa Herrieth "Johannes are you at COET?" nilijibu ndio nipo COET, kuna nini Herriet? "I heard from my friend that you are postponing a year because of school fees?, can we meet now?" yeye hakuwa darasani wakati naaga wengine!
Binti Herrieth alinipa kiasi cha shilingi million moja za kitanzania, akisema amenikopesha, kwamba siku ni sort mambo yangu nimrudishie. Kwanza sikuamni, kwamba nimepata ada, nimepata hela ya kodi, tena zimetoka kwa Herrieth, mwanamke wa ndoto zangu ambaye kila nikimuona natetemeka. "Herrieth why are you helping me?" nilihamaki kwa broken English yangu, alinijibu kwamba, wao wanapewa pocket money kila baada ya miezi mitatu, na alikuwa na balance ambayo alipanga kumtumia mama yake, lakini baada ya kusikia kwamba nina uhitaji ambao ungewa risk future ya masomo yangu akaona anisaidie.
Huu ndio ulikuwa Mwanzo wa ukaribu wangu na Malaika huyu wa duniani. Kwa Semester ile tulimalizia discussion na maandalizi ya UE kwa pamoja, alinisaidia sana pamoja na classmate wenzangu ku cover pale nilipo miss. Nashukuru Mungu Sikupata Supp, japo ufaulu wangu ulikuwa wa kawaida sana.
Fuatana na mimi kwenye simulizi hii halisi ya maisha yangu, je? ni nini kilitokea kati yangu na Herrieth kuanzia Semester ya Pili mwaka wa Pili? Ngoja niandae report ya Client then tutaendelea.............