Ukweli mchungu kuhusu KINANA

Alistaafu jeshi mwaka 1972 akiwa ametumikia jeshi miaka 20 ! Cheo cha mwisho 'Kanali'. Kwa mantiki hiyo alipata ofisa kadeti (Luteni)1952 ! Hili lilikuwa jeshi gani ? .......KAR ? ...TPDF !? JWTZ !?

You have a point mkuu! tatizo watu wengine mapenzi yao binafsi kwa Kinana yanawafunika mpaka wapo tayari kutudanganya kama watoto wadogo ili mradi aonekane ni msafi.
 
acha ujinga kumfagilia JANGILI.. huwezi kusema huyu mtu ni makini wakati ameshindwa kutupa majibu ya kinagaubaga kuhusu ujangili wake, na matokeo yake amaekuwa mtu wa kuchenga kutoa majibu...
Hawezi kuepuka katika kashfa hii ya meli yake kukamatwa na PEMBE ZA NDOVU NCHINI KOREA...
JIBU NI KWAMBA WEWE PAMOJA NA KINANA NI WAHALIFU NA WAFUJA NYARA ZA SERIKALI....
ETI MELI NI YANGU LAKINI ALIYETUMA MZIGO HUO SIMFAHAMU???????????
DOES ITS MAKE SENSE?
HUWEZI FANYA INTERNATIONAL BUSINESS KAMA HIZI HALAFU USIJUE NI MTU WAAINA GANI UNAFANYA NAYE BIASHARA HII,
KINANA HAFAI.. ILA CCM WAENDELEE KUMKUMBATIA NA WAJUE FIKA WAO NDO MWISHO UMEWADIA WA KUSHIKA DOLA YA TANZANIA....
POLE SANA KIJANAA KWA MAWAZO YAKO FINYU KAMA VILE UPO KATIKA NDOTO...
 
Kei mkiendelea kumchekea maccm kufikia 2020 tembo wote kwisha habari yake atahamia kwa albino.
 
sikudhani kama kuna watu wana mawazo ya kizamani kwaninini msifikirie kumkwamua yule mkulima,mfanyakazi mwananchi wa kwaida wa mtaani kupunguza ugumu wa maisha yao wewe unafikiria kumweka mtu kupambana na wapinzani upuuziiii mkubwa jifunzeni china aheni upuuuzi huuuu tumieni akili zenu kutatua matatizo
 
Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na KUUPONGEZA AU KUUAHABIKIA uteuzi WA KIJINGA NA KIPUUZI uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.
 
Na wasifu wote huo Tembo wanaisha na sasa hasafirishi tena anasaga hapa hapa anasafirisha refined product

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
naloliga hurita unapaswa kuzingatia kwamba utendaji wa Kinana umekuwa ukiporomoka tangu alipokabidhiwa mikoba ya Mukama, ni kweli ana historia au rekodi nzuri ya kiutendaji lakini kulingana na mabadiliko ya kasi ya kisiasa na vuguvugu la mageuzi linalokolea kila kikicha rekodi yake imeanza kuingia dosari ambazo kiukweli hazirekebishiki.

Kama kweli wewe ni mchambuzi wa mambo sidhani kama ingekuwa ni busara kuacha kuzungumzia jinsi alivyojikuta kwenye mitego ya kisiasa inayomfanya ajikute akitoa majibu ya hovyo badala ya kuendelea kutetea rekodi yake kwa kupangua hoja kwa hoja, kule Morogoro vijijini aliulizwa na mwanakijiji mmoja kuhusu tuhuma dhidi yake za pembe za ndovu.. alihamaki na kujibu mbele ya umati uliohudhuria kuwa "umetumwa wewe".. sasa mchambuzi unaweza kupata picha anaelekea wapi.. kwakifupi kuna nguvu inayotawala siasa za mageuzi tz inayofanya wana ccm wachanganyikiwe.

Pia akiwa mjini Morogoro akihutubia wananchi alijikuta kwenye mtego wa kuzungumzia cdm muda wote wa hotuba kana kwamba cdm ndio chama tawala na yeye na ccm ni wapinzani.. huko ni kukosa mwelekeo na kuchanganywa na siasa za kisasa ambako naamini hakumpeleki kwema kama katibu mkuu, bali ni kuzidi kukiangamiza chama hiki kikongwe.
 

kwahiyo kwa mawazo yako ushamsafisha
haya kachukue posho yako
ukitaka kumjua vizur waulize tembo
 
Umakini wa Kinana utawezaje kwa sasa hivi kubadilisha na kuboresha maisha ya Watanzania? Ni jinsi gani umakini huo utaweza kuondoa shutma dhahiri dhidi ya ccm na kuweza kugeuza mtazamo wa wananchi kwa ccm, tofauti na ilivyo sasa?
Meli imeshatoboka tunasubiri mshindo mkuu punde usemi utachafuka wacha watimie kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…