Ukweli mchungu kwa timu Simba

Ukweli mchungu kwa timu Simba

Itovanilo

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2018
Posts
2,314
Reaction score
5,150
Najaribu kupitapita mitandao mbalimbali, naona kila mtu anasema Simba itatinga hatua ya robo fainali, huku wakikubali kuwa timu yao ni dhaifu lakini bado wanang'ang'ania eti watafika huko.

Mimi nakataa, namba za kiufundi zinanikatalia kabisa,

Ni hivi, huyu Simba kachukua points sita kwa mchovu Vipers, aliyewapoteza wachezaji wengi msimu huu kama Cesar Lobi Manzoki na Bobos.

Mechi ya kwanza kule Uganda Simba ilishinda kwa kudra za MUNGU tu huku mastraika na viungo washambuliaji wote wakishindwa kabisa kufanya kazi yao,

Tukirudi hapa kwetu kwa Mkapa ile juzi ukweli unadhihirika kuwa kuna wachezaji hawafai hata kuichezea klabu kubwa kama Simba huku likifungwa goli tamu na la kiufundi kwa jitihada za mchezaji mmoja mmoja na si timu.

Mechi inayofuata mnakabiliana na wagumu Horoya huku kiufundi Horoya akiwa anaimudu Simba kwa maeneo mengi, yaani kiufupi Simba anakufa hapa kwa Mkapa na kwenda kuzikwa kwa wababe na maanibiteni
Raja Club Athletic. Huku mkubwa Horoya akijihakikishia points zake Saba na kuwa na uhakika wa kuingia robo final kwani mwisho kabisa atamalizana na wabovu Vipers.

Kwa Yanga hii US Monastir hatoki kwa Mkapa
 
Najaribu kupitapita mitandao mbalimbali, naona kila mtu anasema Simba itatinga hatua ya robo fainali, huku wakikubali kuwa timu yao ni dhaifu lakini bado wanang'ang'ania eti watafika huko...
Utopolo ni lini mtakuwa na akili?

Ni lini Simba alifanya vizuri mkakataa kuukubali ukweli?

Kila Simba akishinda kimataifa inaonekana amekutana na timu mbovu.

Akifungwa simba inaonekana mbovu. Kweli Manara alikuwa sahihi wenye akili timamu kwenye ile timu ni wawili tu,wenginw wote mlipaswa kuwa Mirembe.

Kwa taarifa yako tunamuua huyo Horoya wako na tunakwenda robo fainali baki na wavu wako.
 
Kila la heri Simba. Haya sio mashindano ya wachovu. Hata akitoka, kuna tofauti ya kuwa mchovu katika washindi na kuwa mshindi katika wachovu.
 
Najaribu kupitapita mitandao mbalimbali, naona kila mtu anasema Simba itatinga hatua ya robo fainali, huku wakikubali kuwa timu yao ni dhaifu lakini bado wanang'ang'ania eti watafika huko...
Simba watamfunga Horoya bwashee
 
Kweli kabisa lakini ukweli mchungu timu yetu mbovu sana
Timu inatakiwa ishinde basi siku hizi duniani kote hakunaga mpira mtamu.wanaojaribu kucheza mpira mtamu unaona wanaongezewa muda na marefaree.

Unafuata mbinu unafunga unalinda ushindi, kikubwa ushindi.
 
Basi sawa. Tusubiri Horoya wataamua hii kesi
 
Najaribu kupitapita mitandao mbalimbali, naona kila mtu anasema Simba itatinga hatua ya robo fainali, huku wakikubali kuwa timu yao ni dhaifu lakini bado wanang'ang'ania eti watafika huko...

Uto na Kolo wote watashinda game zao za nyumbani March 18 & 19 na wote wataenda robo fainal……
 
Kolo FC safari yake imefika mwsho.. bila kukutana na hyo Timu mbovu ya Viper hizo point 6 angezisikia kwa Radio tu
Umesahau Viper ndio alimtoa Mazembe kwenye mabingwa ndio mkapangwa nae huko kwa waliofeli

Champions League hakuna timu mbovu, timu mbovu zote zilitolewa na kutupwa Shirikisho
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Umesahau Viper ndio alimtoa Mazembe kwenye mabingwa ndio mkapangwa nae huko kwa waliofeli

Champions League hakuna timu mbovu, timu mbovu zote zilitolewa na kutupwa Shirikisho
Nyie ni mabingwa wa ligi gani?
 
Waulize CAF kwa nini wakatuweka kwenye ligi ya mabingwa na nyie mkatupwa Shirikisho (kwa waliofeli)?
Ni utaratibu tu umewabeba lakini nyinyi sio mabingwa na hata mwaka huu hamtakuwa mabingwa. Sasa mnavyojivuna mtadhani kweli ni mabingwa. Halafu hilo kombe la waliofeli mmepambana mara ngapi kulibeba na lini mmewahi kulibeba?
 
Hatujabebwa, tulishinda dhidi hatu za awali za kufuzu mabingwa, nyie mkashindwa, hakuna cha kubebwa hapo
 
Mbona Horoya kashindwa kumfunga Vipers kama Simba alivyompiga. Ingekuwa mpira hesabu kama unavyosema basi Simba alitakiwa amfunge Horoya aliyeshindwa kumfunga Vipers.

Kwakuwa siyo yote yanawezekana..
Wakati akili zinagawiwa na Mungu wengine hawakuwepo.
 
Back
Top Bottom