Ukweli mchungu kwa Walokole wote duniani, hamtamuweza Shetani, mtazaliwa kuzeeka na kuondoka hamtamuweza na dunia itabaki

Acha longolongo nyingi.

Kwanza kabisa, thibitisha Shetani yupo kweli na habari za kuwepo kwake si hadithi za kutungwa na watu tu.
Shetani yupo watu wanaomfahamu ni wale waliokidhi sifa zake tu
 
Hujathibitisha yupo.

Acha longolongo nyingi.

Kwanza kabisa, thibitisha Shetani yupo kweli na habari za kuwepo kwake si hadithi za kutungwa na watu tu.
Narudia tena Shetani yupo yule ni dhahabu, dhahabu haiokotwi inachimbwa kumpata ni sawa na kuchimba dhahabu. Siongei kwa kubahatisha na mimi sio mwehu
 
Uzi mzuri, lakini niruhusu nikupe shule kidogo

1.KWAMBA tunapomwamini YESU kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha yetu tunapata upendeleo wa kuitwa WANA WA MUNGU, imagine heshima hii kubwa Shetani hatawahi kuipata.

2.KWAMBA tumezaliwa upya kwa mbegu ISIYOHARIBIKA, that being said Siyo sisi tunaoishi tena bali anaishi Yesu ndani yetu.

3.KWAMBA Shetani alinyang'anywa mamlaka yote Mbinguni na duniani, infact shetani hana mamlaka tena isipokuwa anaigiza kuwa nayo.

Soma biblia itakusaidia kujua uhalisia wako katika Kristo
 
Hujathibitisha yupo.

Acha longolongo nyingi.

Kwanza kabisa, thibitisha Shetani yupo kweli na habari za kuwepo kwake si hadithi za kutungwa na watu tu.
Sitafanya hivyo kwasababu katika article yangu nimesema hakuna kitu chochote anachohitaji kutoka kwa binadamu ni full package, hivyo kunitaka nikuthibitishie ni sawa na kumkosea adabu
 
Shetani na mungu ni marafiki huwa wanakutana mara kibao wanapiga story, mda mwingine huwa wanabet kabisa wanaweza kumchukua binadamu mmoja wakampa mateso ya kutosha ili waangalie nani mkeka wake utatiki
Ukisoma kitabu cha Ayubu alivyopata pata yale mateso,inafikirisha Sana!!!
Ilivyokua shetani na Mungu wanapiga stori

Mungu: unamuona mtumishi wangu Ayubu alivyo mwaminifu?

Shetani:aaaah Hana lolote huyo! Ni vile Tu umemzingira pande zote!!

Mungu:humuwezi huyo nakwambia!

Shetani:mwachilie uone!!
😀😀😀😀😀
 
Sitafanya hivyo kwasababu katika article yangu nimesema hakuna kitu chochote anachohitaji kutoka kwa binadamu ni full package, hivyo kunitaka nikuthibitishie ni sawa na kumkosea adabu
Hujathibitisha yupo.

Acha longolongo nyingi.

Kwanza kabisa, thibitisha Shetani yupo kweli na habari za kuwepo kwake si hadithi za kutungwa na watu tu.
 
Nyie Walokole sasa hizo nguvu zenu mlizo nazo ni zipi wakati ninyi ni miili hivi kweli umezaliwa Tanzania unasema unampiga Shetani? Are you serious au unakula bange mbichi? Kabla ya kufanya mzaha wa kumpigia kelele nenda kwanza kapigane na jeshi la Marekani ukishafanikiwa nitafute nikupeleke kwa vinyamkera na vibwengo, ukimalizana nao nikupeleke kwa majini ukiwamaliza wote nikupeleke daraja la tatu mpaka nakufikisha kwake skeleton ina afadhali
 
Duh! Umeamua kujitoa kwake na kuwa wakala wake mwaminifu.

Vv
 
Shetani anaogopa kifo sijapata Kuona, na anamuogopa YESU sijapata Kuona
29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?
Mathayo 8:29

31 Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe.
Mathayo 8:31

Muoga sana huyu kiumbe unae mmwagia Sifa........Nayaweza yote katika yeye anitiae nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…