east36
JF-Expert Member
- Aug 4, 2013
- 1,352
- 610
Nauliza kwa dhati kabisa
Nauliza swali ambalo wengi wanaogopa kuliuliza waziwazi…
Hivi hawa machawa wa CCM wanaishi nchi hii hii tunayoiishi sisi, au wanaishi kwenye dunia yao?
Kwa sababu ukweli hauhitaji kupakwa rangi,
Mbaya zaidi, tunashuhudia matukio mazito hadi ya kupoteza maisha kama yale ya tarehe 29 Oktoba lakini kwao hilo halina uzito wowote. Kimya. Hakuna kuhoji. Hakuna kuwajibisha. Ni kusifia tu.
Sasa nauliza:
👉 Hawa watu hawaumizwi na hali hii?
👉 Au kuna maslahi binafsi yanayowafanya wawe vipofu kwa mateso ya wananchi wengine?
👉 Au tumefika mahali utu hauna maana tena?
👉 Kama wao hawapati madhara moja kwa moja je hawana wazazi au ndugu, jamaa na marafiki wanaoteseka?
👉 Je ni tamaa, ubinafsi na ulafi uliopindukia?
Kwa sababu haiwezekani mtu mwenye akili timamu, anayeishi na wananchi, akaona haya yote halafu bado akaamua kupiga makofi tu. Watu wanahoji anajibu kirahisi rahisi tu.
Kama kuna mtu anaona kila kitu kiko sawa, basi aseme wazi sisi wengine tunaona nchi iko pabaya sana na inaelekea kubaya zaidi.
Tujadiliane kwa hoja. Lakini ukweli lazima usemwe.

- Maisha yamekuwa magumu kupindukia
- Vijana hawana ajira
- Wananchi wanalia kila siku
- Mfumo unaendelea kuwaumiza wale wale wa chini
- Uongozi haueleweki