Ukweli mchungu: Mashabiki wa simba hawawezi kuwa na furaha timu yao kushiriki caf super cup, wakati hawana kombe (ndoo) lolote ndani ya kabati lao

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Na
NALIA NGWENA

Hakuna shabiki yoyote Yule duniani mwenye furaha yakushiriki michuano Fulani pasipo na mafanikio yoyote, Bali kila shabiki ana matamanio yakupata mafanikio haswa yakubeba kombe (ndoo) Hiyo ndiyo furaha kubwa ya shabiki yoyote wa mpira wa miguu duniani.

Hata kandarasi mpya anayopewa kocha kuja kufundisha timu huwa anapewa vipao mbele vya timu husika inaweza kuwa achukue kombe la ligi, fa mapinduzi Hadi ngao ya jamii, nimegusa zaidi hapa nchini kwetu.

Naona inatumika nguvu kubwa sana au danganya Toto kwa mashabiki wa simba kudanganyiwa habari za simba kushiriki caf super cup na umekwnda extra mile kabisa nakuwaambia mashabiki wa simba kuwa simba ni Bora sana kimataifa ndiyo maana imechaguliwa kushiriki caf super cup.

Sawa, Sasa furaha ya mashabiki ipo wapi hapo?? Kama timu haina hata kombe lakufutia jasho ndani ya kabati katika msimu uliopita na huu msimu uliopo ni tia maji kombe lililo baki ni fa na timu haina uhakika Kama italichukua maana competition ni kubwa.

Piga ua galagaza kushiriki caf super cup siyo furaha kwa mashabiki wa simba Bali mashabiki wanataka kuona timu yao ikitwaa makombe pamoja nankupata ushindi mbele ya mtani wao yanga Kama mwenyekiti alivyowaahidi wanasimba kwenye kampeni yake.

My take, kelele za kushiriki caf super cup ni kelele zisizo na mashiko Wala faida mbele ya mashabiki wa simba, maana timu itashiriki pasipo na faida yoyote ikiwa imepoteza makombe yote ya ndani.
Kujiita mkubwa wakati huna kitu ni sawa na kubwa jinga tu.
 
Na bado mtalia sana,


Tabula rasa FC
 
Ni CAF super league sio CAF super cup. Super cup ni shindano linalohusha bingwa wa CAF confederation cup dhidi ya bingwa wa CAF champions league
 
Ndugu yangu hizi lawama watupie wenyewe CAF wao ndio waliopanga vigezo sio simba. Na wala caf hawakuwauliza mashabiki wa simba kama wana furaha au hawana furaha. Na wewe pambana utajua kushiriki super ligi kuna furaha au uchungu.

Wivu ukikuzidi kajifungue hospitali.
 
Duh
 
Mashabiki wenzangu wa Yanga tunafungua threads kama vichaa kuifuatilia Simba huu ni umbumbumbu Pro Max tujadili ya kwetu tumefanya vizuri msimu mmoja midomo imekuwa mirefu kweli wenzetu wamefanya vizuri misimu mnne mfululizo tukae Kwa kutulia CAF kuwachagua siyo ngekewa jamaa wapo vyedi.
 
Sawa sawa....
 

Attachments

  • JamiiForums-696826148_378x430.jpg
    29.9 KB · Views: 6
Kama ulivyojifungua wewe
Ahsante kwa ushauri[emoji41]
 
Yanga hatuna shabiki wa hivi [emoji41]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…