Ukweli mchungu: Simba tuliingia mechi ya leo tukiwa hatujiamini

Hujui mpira wewe.duh!,,,unatia aibu hii mada yako.
 
Ungeangalia odd za bet usingekuja na huu upuuzi kwani simba alikuwa anapewa nafasi kubwa
 
kwa wanaojua mpira wanakwambia Yanga walicheza kwa kuiheshimu SIMBA. Siyo kwamba hawakuwa na kasi yao.
 
kwa wanaojua mpira wanakwambia Yanga walicheza kwa kuiheshimu SIMBA. Siyo kwamba hawakuwa na kasi yao.
Simba iliidharau Yanga? Hata ile approach ya kukaa nyuma ni bado nidhamu.
 
Simba walipaki bus na bado manula alikua akipishana na mabeki wake kwa shughuli ya Mayele.
 
Mpira ni Mchezo wa wazi, Simba walijaribu kucheza kidogo dakika 10 za mwisho, Muda mwingi wakikaa nyuma shida ikawa wakipata mpira hawana mtu mwenye kasi ya kuwasumbua Yanga.
Oya umeangalia mpira au unaongea utopolo tu, kipindi chote cha pili simba waliikamata mechi, utopolo upepo ulikata.....
 
Mechi ya Leo mabeki wa Simba ndio walio cheza vizuri na bahati ilikua yao Ila hakukua na mchezaji yeyote wa mbele wa Simba aliye onekana tishio.
 
Hakuna kitu kama hicho,ninachosema kwamba huyu kocha ni mzuri sana,tofauti na Gomes ambae alikuwa bora liende.
Nakuhakikishia huyu kocha endapo atasajiri yeye kama yeye nakwambia Simba inarudi kuwa moto kuliko hata miaka iliyopita.Gomes aliwaua wachezaji wengi sana,na kufanya wengine kukosa muda wa kupumzika.


NB;YANGA WALIKUTANA NA KOCHA AMBAE ANAJUA KUANDAA KIKOSI.
 
Mpira ni Mchezo wa wazi, Simba walijaribu kucheza kidogo dakika 10 za mwisho, Muda mwingi wakikaa nyuma shida ikawa wakipata mpira hawana mtu mwenye kasi ya kuwasumbua Yanga.
Acha uongo kipindi Cha pili yanga mmecheza mpira kwa kupoteza sana mda na mkionyesha kuridhika na matokeo ya sare.wachezaji wa yanga walichelewesha sana mda.
 
Simba iliidharau Yanga? Hata ile approach ya kukaa nyuma ni bado nidhamu.
Kuna tofauti ya nidhamu na mbinu za mpira.

Ndiyo maana kipindi cha Kwanza mlicheza pasi nyingi zisizo na madhara mpaka mkawa mnajiga chenga wenyewe.

Kipindi cha pili mkapoteana ikabidi mzuie huku mkiomba mechi iishe haraka.

Huku mtaani kumetulia tuli. Yanga bora tuliiona Jana na Simba mbovu pia tuliiona.

Utopolo mnacheza mpira mdomoni.

Utopolo mnacheza mpira kwenye gazeti la champion , sports extra(tarimba abass) na mwanasport.

Simba tulishahama hizo enzi za Manara.
 
Mbinu ya mchezo mara zote hupangwa kulingana na sifa na uwezo wa timu pinzani. Kukaa nyuma tafsiri yake unataka mpira uchezwe zone yako zaidi. Hapo ni pale mpinzani wako ana sifa ya kupossess na kupress mpira zaidi yako. Huwezi kuniambia Simba icheze na Ruvu apack buss kisa approach ya game happy itakuwa ni plan mbaya kulingana na attributes za mpinzani wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…