Subira the princess
JF-Expert Member
- Mar 3, 2018
- 3,474
- 3,744
Wasalaam.
Nimesikitishwa na maamuzi ya kamati kuu ya ccm kutaka jeshi la police lichunguzwe kwa sababu eti wananchi wamepoteza imani nalo. Najiuliza hivi kweli serikali ya ccm haijui matatizo ya jeshi lao sikivu na tiifu kwao? Hivi kweli serikali ya CCM haijui kwanini tumefika hapa?
Jeshi la police limefanya maovu mengi ili tu ccm waendelee kutawala na kujinufaisha wao na vizazi vyao. CCM wamejineemesha wenyewe na kuwasahau Police katika ukata mkubwa kiasi cha kuwa wahalifu kwa kupora wananchi mali zao, kuwabambika kesi na kisha kuwadai rushwa unagemea wananchi watakuwa na imani?
Police wametelekezwa na serikali wakiwa na matatizo ya kutosha kama vile;
1. Mishahara duni.
2. Makazi duni.
3. Mavazi wanajinunulia.
4. Lishe duni.
5. Mazingira magumu kazini.
6. Vitendea kazi duni n.k.
Hapo unategemea police wafanye nini zaidi ya kujitafutie riziki kwa njia haramu za kuwaumiza wananchi. Angalia jinsi police walivyompora pesa na kisha kumuua mfanyabiashara mtwara, angalia tukio la hamza n.k unategemea wananchi watawapenda? Ccm na jeshi la police mnachukiwa sana na raia msidanganye mnapendwa, siku mkipitisha katiba mpya ndo mwisho wenu mnatawala kwa mabavu.