Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Sasa hivi mitandaoni ni kilio cha tozo na hii ni kwasababu tozo imetugusa wote na si kundi moja katika jamii, otherwise kilio kingekuwa si kikubwa kiasi hiki na huu ndio ujinga mkubwa wa sisi watanzania.
Kwanini nasema hivi?
Wakati wa Mwendazake, watumishi ambao walikuwa ni wafaidika wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, waliongezewa makato karibu mara mbili na walipolalamika, baadhi ya watanzania wenzao waliwabeza na kuwaambia walipe hizo hela ili na wengine wasome na maneno mengine mengi ya kejeli.
Si hivyo tu, watumishi wa umma walipokaa miaka sita bila kuongezewa mishahara, wako watanzania waliwakejeli na kuwaambia kama hawaridhiki na mishahara yao waache kazi.
Halikadhalika, watumishi wanapolalamika kuwa PAYE ni kubwa mno, wako watanzania wanaowaona kama walalamishi na kuwaambia wanapaswa kulipa kodi ya serikali.
Mbali na yote hayo, mwezi uliopita watumishi walipolalamikiwa kuongezewa shilingi 12.000, 20,000 n.k, kuna watanzania waliwabeza na kuwaambia kama nyongeza hiyo wanaiona ni ndogo, basi waache kazi na maneno mengine ya aina hiyo.
Funny enough, baadhi ya watanzania waliowataka watumishi wa umma waacha kazi kama wanaona mshahara ni mdogo, ndio hao hao leo hii wanamlaumu Mwigulu kwa kuwataka watanzania wanaolalamikia tozo wahamie Burundi.
Wamasai huko Ngorongoro wanaohamishwa na kupelekwa Tanga wanapolalamikia, kuna watanzania wanawabeza na kuwataka wasipinge uamuzi halali wa serikali lakini ndio hao hao leo hii wanapinga uamuzi wa serikali kuongeza tozo kwenye miamala ya mabenki, n.k.
Mifano ya aina hii iko mingi sana ila yote inadhihirisha jambo moja kubwa kuwa watanzania ni watu wasioweza kuungana kupinga uonevu wa serikali dhidi ya kundi fulani katika jamii au hata pale ukandamizaji huo utapogusa watanzania wote kama ilivyo kwenye hili swala la tozo linalotugusa watanzania karibu wote.
Sasa watanzania tujiulize, kama hatuwezi kuungana kupinga kwa nguvu uonevu au ukandamizaji unaofanywa na serikali dhidi yetu, watawala wana hofu gani ya kuendelea kutukandamiza?
Jibu rahisi ni kwamba, wakulamiwa kwa haya yanayoendelea hapa nchini si watawala tena, bali ni sisi watanzania wenyewe kwa kukosa umoja katika kupinga mambo tunayoamini sio ya haki yanayofanywa na watawala, hivyo tuendelee kuvuna tulichopanda pasipo kulalamika kwani mtu huvuna kile alichopanda na kamwe si vinginevyo.
Kama vipi, Mwigulu njoo na tozo ya kulalamika ili tukae kimya kabisa.