UKWELI MCHUNGU: Wakatoliki wenzangu Papa Francis ni mjumbe wa shetani ndani ya kanisa

Kama una amini ndiye huyu tu umeliwa.Since day one of the Catholic Church mlikuwa mmepigwa.Baada ya Shetani kushindwa msalabani,alibuni kwanza Kanisa la Roma na baadae Uislam.Kanisa la Roma ndicho kiti cha enzi cha Shetani mkuu.
Na wewe unaweza kusema umeandika kitu? Bure kabisa!
 
Kauli ya papa sio kauli yake bali ni kauli ya taasisi, hivo toa neno papa weka kanisa la roma
 
Sikio la kufa halisikii dawa,ila huo ndio ukweli whether you like it or not.
Ukweli huwa ukweli siyo kwa kusema kuwa ni ukweli, bali kwa kujisimamia wenyewe. Watu wengi wana mtazamo hasi na Kanisa Katoliki. Mtu akisikia tu maoni ya mwandishi wa BBC kuhusu papa au Kanisa Katoliki anaamini kana kwamba amesoma injili. Critical thinker cannot think that way. Lazima uwe na 'justification' ya unachokisema na siyo tu kusema kama watu wanavyoamini uchawi kwa sababu tu wamezaliwa kwenye jamii ambayo kila mtu anaamini hivyo na tukio lolote wanaloshindwa kuelewa chanzo chake wanaamini ni uchawi. Kanisa lina maadui wengi na kama limekosea katika mambo mnayodai kwa nini mhangaike nalo wakati nyie mko kwenye mstari? Ulishamwona Mkatoliki yeyote anayejitambua anahangaika na maisha ya mtu mwingine au dhehebu lolote la dini? Uwongo wenu mnaouzusha na msioweza kuuthibitisha isipokuwa kwa kuita ukweli hautawasaidia kitu. Ungeweza kuwasaidia kama mngeweza kuuthibitisha huo mnaodai ni ukweli mlio nao. Vinginevyo nitaendelea kuamini nyie ni wadau wa uwongo na mnaeneza huo uwongo kwa masilahi yenu na hautawasaidia. Hakuna pesa utakayoipata kwa kusema uwongo, na wala huwezi kupata kipato kizuri kwa kusema uwongo.
 
Umeandika ukweli mchungu! Hata mimi ninaanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu huyu Kiongozi wetu mkuu wa Kanisa. Sijui ni kwa sababu ametokea kwenye Shirika la Majesuit!!

Kiukweli hizi siku za karibuni amekuwa tofauti sana ukimlinganisha na watangulizi wake mfano Papa Yohane Paulo wa Pili, na pia Papa Benedict wa 16! Hakika akiendelea na huu mtazamo wake binafsi kuhusu kuwatambua mashoga, basi kuna kila dalili ya kuja kulivuruga kabisa Kanisa la Mungu.

Maana msimamo wa Kanisa uko wazi kabisa kuhusu masuala ya ushoga, ndoa za jinsia moja, utoaji mimba, nk. Kamwe Wahafidhina ndani ya Kanisa hatutakubali upuuzi kama huo kutokea.
 
Haipo sababu yeyote ya kuwa na msimamo hasi na dhebubu la Kikatoliki,it's just that we love you and we do not want you to suffer in eternal hell,ila kama mkishupaza shingo damu yenu hatudaiwi, tumetimiza wajibu wetu kama Mungu alivyotaka.

Ila inashangaza kuona kwamba hamuoni upotovu obvious na wa makusudi uliopo katika Dhehebu la Kikatoliki.Ila I know why,you are discouraged to read the Word of God ili muwe easy target for Satan's deception.

Anyway what is your opinion about the following clip,naye Pope Francis ana msimamo hasi kuhusu dhehebu ambalo yeye ndiye kiongozi mkuu?


View: https://youtu.be/lzmRVmlqGKU?si=-RPFTusLdQPxBquo
 
Hata yeye atapita na kuliacha kanisa..

Kanisa letu limepitia masahibu makuu kuliko hili
 
Tuambie twende wapi palipo pasafi saana, hebu tukusikilize pengine una hoja
 
Mdogo wangu kama mbingu isivyo rahisi na jehanamu sio rahisi kama unavyowaza, tatizo unawaza kishabiki saana na mawazo yako yapo kibinadamu mno..

Hebu toka nje ya box na uachana na mafundisho ya kibinafsi unayopewa na wachungaji wenu halafu uitafakari neema ya Mungu

Sijui kama unanielewa, sijui kwa kweli
 
So Jesus who established the church is a Satan, what a blasphemy!

Na Kama unabisha Yesu hakuanzisha kanisa KATOLIKI niambie ni Nani alilianzisha, au wafuasi wa Yesu waliutumia umoja upi hadi kulipigania kanisa kuweki vizazi hadi vizazi.


Mdogo wangu una shida kubwa sana yaani, kubwa mno. Ni kweli Kuna mabaya mengi sana yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wa kanisa lakina haihalalidhi mafarakano kama wakristu, hata kama Yuda iskarioti alimsaliti Yesu haiondoi ukweli ni kuwa alikuwa mtume mteule wa Kristu

Kwa kusema kanisa KATOLIKI limeanzishwa na shetani maanake YESU ndiye shetani mwenyewe na kitu ambacho ni kufuru na laana kubwa sana. Ni sawa na kusema Yuda alichaguliwa na shetani kuja kumsaliti Yesu, sijui kama mnafikiriaga ipaswavyo kama hamjaropoka kimihemko
 
Wewe unasali kanisa gani kwanza ndugu yangu
 
Kitendo cha kumtengua Askofu anayepinga hayo masuala ya ushoga na kutuita sisi wakatoliki tunaopinga hivyo vitendo kuwa tuna mawazo duni na ya kale na waraka unaowapa uhalali mashoga kuchafua sakramenti mbali mbali takatifu ni hatua mbaya sana kuwahi kufikiwa kwa karne hii, je bado unahitaji ushahidi zaidi?

Clip zipo tafuta utajionea, Paulo alimkemea Petro kwa kuwa mnafiki na Petro alitambua makosa take akajirudi. Je huyu papa ni mkuu kuliko Petro??

Je bado tutaendelea kukumbatia dhambia na uasi ndani ya kanisa chini ya kivuli cha "shutuma" na "uongo"??


Moja ya dhambi mbaya sana kwa mkristu ambayo itamfanya asirithi ufalme wa mbinguni ni UOGA (1 Kor 6:9-11)

Na sisi wakatoliki huwa tunaungama kwa mawazo, kwa matendo, maneno na KWA KUTOTIMIZA WAJIBU
 
Sawa asante

ila ningependa nami unipunguzie hizo akili ulizo nazo nimuelewe Fransisi
 
 
Mkuu hii clip ina ukweli?
 
Hawa ni wasabato ambao wanasem
Mkuu hii clip ina ukweli?
Ni kweli, ila hupaswi kuweka tumaini lako kwa mwanadamu

Neni la Mungu linasema "Bwana kama wewe ungehesabu maovu yetu, Nani angesimama.."

Tumaini letu ni Kristu tu achana na habari za papa hata yeye akikengeuka moto utamuhusu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…