Ukweli mchungu: Wasanii wafuatao hawaji kuhit kama zamani waachane tu muziki

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2016
Posts
4,208
Reaction score
14,143
Penye ukweli lazima pasemwe,

Maisha ya muziki yamebadilika sana ni tofauti na ya zamani. Huwa nahuzunika naposikia Interview ya msanii fulani wa zamani akisema "sahizi nipo mbioni narudi nina ngoma yangu mpya ipo jikoni hivyo mashabiki wangu wajiandae" unatamani kama umshauri hiyo Pesa anayohangaikia kutolewa nyimbo mpya afanyie kitu kingine cha maana kwani hawezi kupokelewa kama zamani akubali tu muda wake umepita aketi chini atafute maisha mengine tofauti na mziki.

Hawa wafuatao kamwe hawaji kuhit kama walivyo hit zamani , kama wanafanya basi wanalazimisha tu ili wasipotee midomoni mwa watu na wenye akili waliolisoma "game" wameamua kukaa pembeni.

Q Chilla
Mr Nice
Afande Sele
TID
Ray C
Chid Benz
Inspector Haroun
Madee
.
.
.
.
Ongezea na wewe.
 
Ali Salehe Kiba......huyu naye kabebwa kwa lazima zaidi ya miaka 6 na Clouds yao ili kumpambanisha na Diamond na kumrudisha kwenye chati lakini bureeeee tupu wanaishia kumaliza nguvu zao ,alafu sasa kama vichawi yaani vinazidi kukomaa tu na kutengeneza vigisu lakini ngoma inaporomoka inaanza upya chini kabisa,yaani walichofanikiwa ni kulifanya jina lake liendelee kuzungumziwa mtaani ilhali muziki wake alishauzika mwenyewe,namshauri upande alioingia kibiashara una kila namna ya kumtoa na akawa mtu tofauti pasi kujivunjia heshima aliyowahi kujijengea kuliko kudanganyika na vivaa mlegezo vya pale wanapopaita Mjengoni,shavu la partnership alilolipata litoshe kumlelea familia yake na sio kushindana na wenye wakati wao.

Q chief kurudi kwenye umoto wake ni ndoto pia,ila atabaki anasikika na kupotea kana ilivyo kwa mwenzie TID ijapokuwa utofauti wao ni kwamba Q chief ana spirit ya music na TID anafanya kwa MOOD ya msimu,kwa sasa wote wajiandae haraka sana kuwekeza kabla hawajapotea kabisa ama kwenda kuomba kazi kwenye Music Band.
 
  • pnc
  • o ten
  • zay b
  • sister p
  • khasim mganga
  • temba
  • gigy money
  • enock yamoto band
 
Kwa TID hapana, jamaa akitoa ngoma inakuwa kubwa tuu uraiani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…