Ukweli Mchungu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Tumia fursa hii kueleza lililoko moyoni mwako, iwe ni kwenye wigo wa siasa, michezo, dini, mapenzi na lolote lile. Nafasi ni yako.


Usimkashifu rais ni hatari kwa uhuru wako kitaa. Ukitaka kupendwa nyumbani, usikosoe, sifia kila kitu, hata ukiona buibui kachafua nyumba kwa utandu wake, weee sema, mama una baraka sana, na mkono wako umejaa neema tangu baba asafiri, kila kitu hapa ndani kina nawiri na kunenepa, hata mabuibui.
 
Hayupo mtu atakayekupenda kama mama yako mzazi.

2. Masikini siku zote hana rafiki.

3. Watu huheshimu pesa zako, hawakuheshimu wewe.

4. Yule unayempenda sana ndiye atayekuumiza sana.

5. Ukweli ni mwepesi,unapoanza kuuelezea unakuwa mzito.

7. Vitu viwili vinavyoweza kueleza maisha yako.
(i)Wakati huna kitu.
(ili)Wakati una kila kitu.

8. Watu hawakumbuki mazuri uliyowahi kutafanya, watahakikisha wanakumbuka mabaya uliyowahi kuyafanya.

9. Watu watakuuliza unafanya kazi gani ili kuishi, ili wakadirie kiasi cha heshima watakayokupa.

10. Watu wanapenda kukuona unateseka kwasababu matatizo yako yanawafanya wajiskie vizuri.

11. Unaweza kupenda mtu au watu, lakini isitegemee mtu au watu hao wakupende tena.

12 . Huwezi kuibadilisha hii dunia lakini dunia inaweza kuusikiliza utani wako.
 
ShetAni hana rafiki wa kudumu
 
Rafiki yangu mpendwa,

Kuna vitu waliofanikiwa sana wanavijua, lakini huwa hawaviweki wazi.

Wanafanya hivyo kwa sababu jamii huwa haielewi vitu vingi kuhusu mafanikio, na hivyo huishia kuwashambulia waliofanikiwa pale wanapojaribu kuwa wakweli.

Mara ngapi umesikia masikini wakiwasema matajiri kwamba ni freemason au wamepata utajiri wao kwa njia za giza?
Umewahi kumwona tajiri akibishana na masikini juu ya hilo?

Jibu ni hapana, tajiri anajua masikini hawezi kuelewa na hata kuamini mengi yaliyomsaidia yeye, hivyo anamuacha aamini anachochagua kuamini.

Leo nakupa siri kubwa, nakupa ukweli mchungu ambao ukiweza kuupokea na kuuishi, utaweza kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Ukweli huo ni kama unataka mafanikio makubwa, basi usiwe โ€˜fairโ€™. Neno fair yaani usawa limekuwa linatumika sana.
Wengi wamekuwa wanalalamika kwamba maisha hayapo fair, pamoja na juhudi wanazoweka bado hawapati wanachotaka.

Leo nakwenda kukushirikisha maeneo 10 ambayo upaswi kuwa โ€˜fairโ€™ kama unayataka mafanikio makubwa. Kwenye maeneo hayo, unapaswa kuwa tofauti kabisa na wengine walivyo ili uweze kupata matokeo ya tofauti.



Kama unataka mafanikio makubwa, usiwe fair kwenye maeneo haya 10.

1. Usiwe fair kwenye Kazi
Watu wengi wanafanya kazi kwa mazoea na kwa viwango vya chini sana. Wewe nenda kinyume nao, fanya kazi kwa juhudi kubwa na kwa viwango vya juu sana. Anza kwa kufanya kazi muda mrefu kuliko wengine. Kama wanaanza kazi saa mbili asubuhi na kumaliza saa 10 jioni, wewe anza saa moja asubuhi na kumaliza saa 12 jioni. Kila siku weka masaa 2 mpaka 4 ya ziada kwenye kazi unayofanya.
Na unapofanya kazi weka umakini wako wote kwenye kile unachofanya na usiruhusu usumbufu wowote ukuvuruge.

2. Usiwe fair kwenye Muda
Watu wengi huwa wanachezea muda kama vile ni kitu ambacho hakina ukomo. Lakini muda una ukomo, kuna masaa 24 tu kwenye siku, ukishayatumia huwezi kupata tena mengine. Kuwa bahili sana wa muda wako, usikubali upotee hovyo kwa mambo yasiyo na tija. Kila siku unayoianza pangilia muda wako, weka vipaumbele vyako vya siku na vifuate hivyo. Kuwa na orodha ya mambo utakayoyafanya kwenye siku yako na ifuate hiyo. Usiruhusu usumbufu au mahitaji ya wengine yaingilie ratiba yako muhimu ya siku.

3. Usiwe fair kwenye Fedha
Watu wengi wakipata fedha huwa wanakimbilia kuzitumia mpaka ziishe na hata zikiisha hawaishii hapo, badala yake wanakopa ili waendelee kutumia zaidi. Wewe usiwe hivyo, unapopata fedha yoyote ile, tenga kwanza akiba kabla hujatumia. Usitumue kisha inayobaki ndiyo uweke akiba, fedha huwa haibaki. Badala yake weka akiba kwanza kisha inayobaki ndiyo utumie. Na akiba unayoweka, iwekeze mahali inapozalisha na kukua zaidi. Hiyo ndiyo njia ya uhakika ya kuondoka kwenye umasikini na kwenda kwenye utajiri.

4. Usiwe fair kwenye Kusudi
Watu wengi wanaishi maisha ya bendera kufuata upepo, hawalijui kusudi la maisha yao na hivyo ni rahisi kushawishiwa na chochote kinachopita mbele yao. Wewe usiwe na maisha ya aina hii, pambana ulijua kusudi la maisha yako na kuliishi kila siku. Jua kwa nini uko hapa duniani, maisha yako yanapaswa kuacha alama gani na jipe wajibu mkubwa unaokusukuma kuchukua hatua kila siku. Ukiwa na kusudi unakuwa na msimamo.

5. Usiwe fair kwenye Ndoto kubwa
Watu wengi hawana ndoto kubwa, wanaishi maisha ya mazoea, wanafanya shughuli zao, wanapata pesa ya kula na wabaridhika na hayo. Wewe usiwe mtu wa kuridhika na mambo madogo unayopata sasa. Kuwa na ndoto kubwa sana, ndoto ambazo wengine wakizisikia wanaona kama umechanganyikiwa na wanakuambia haiwezekani. Ni ndoto kubwa unazoziamini bila ya shaka zinazokusukuma kufanya makubwa zaidi kwenye maisha yako.

6. Usiwe fair kwenye Kujifunza
Watu wengi wakishahitimu shule, hawajifunzi tena vitu vipya wala kusoma vitabu. Watu hawasomi kabisa vitabu, wakiamini hakuna kipya wanachoweza kujifunza, tayari wanajua kila kitu. Wewe usiwe hivyo, kuwa mtu wa kujifunza vitu vipya kila siku. Kuwa mtu wa kusoma vitabu kila siku. Hakikisha kila mwezi unasoma angalau kitabu kimoja na kwa kila kitabu unachosoma chukua hatua za kuyabadili maisha yako. Hilo pekee linatosha kukupa fursa nyingi na kukuwezesha kupiga hatua kuliko wengine.

7. Usiwe fair kwenye Mahusiano
Walio wengi wanazungukwa na watu hasi, watu waliokata tamaa na wanaowakatisha tamaa pia. Mahusiano yao mengi yanakuwa kikwazo kwao kupiga hatua. Wewe kuwa makini sana na mahusiano yote uliyonayo, hakikisha yanakuwa mahusiano bora na yanayokusukuma uwe bora zaidi. Waepuke watu hasi na waliokata tamaa kama ukomo, usijenge ukaribu na watu wa aina hiyo, kwani watakuambukiza waliyonayo. Ulivyo ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka, chagua watano bora ambao watakusukuma upige hatua zaidi.

8. Usiwe fair kwenye Kujiamini
Watu wengi hawajiamini, wanaweza kuwa na ndoto kubwa ila wanapowaambia wengine na wakawakatisha tamaa, wanawasikiliza na kukubaliana nao. Ndiyo maana kundi kubwa la watu kwenye jamii hawawi na maisha wanayoyataka, maana hawajiamini kiasi cha kuwashinda wale wanaowakatisha tamaa. Wewe jiamini kupitiliza, amini ndoto kubwa ulizonazo utaweza kuzifikia bila ya kujali unaanzia wapi sasa. Hata kama wengine wanakuambia haiwezekani, hata kama wanakuonesha na mifano kabisa, usiwaamini zaidi ya unavyojiamini wewe. Jifunze yote muhimu na endelea kusimama kwenye ndoto zako kubwa.

9. Usiwe fair kwenye Ungโ€™angโ€™anizi
Ili ufanikiwe lazima uwe kingโ€™angโ€™anizi sana, ujitoe kweli kweli na ukomae mpaka upate kile unachotaka. Utakutana na magumu, vikwazo na kushindwa, lakini usiruhush hayo kuwa mwisho wa safari yako. Jipe kiapo kwamba utapata kile unachotaka au utakufa ukiwa unakipambania, hakuna mbadala wa hilo.

10. Usiwe fair kwenye kutoa Kafara
Ili upate kile ambacho hujawahi kupata, lazima uwe tayari kupoteza kile ambacho tayari unacho sasa. Kuna vitu vizuri unavyo sasa lakini ni kikwazo kwako kupata mafanikio makubwa unayotaka. Wengi wanataka mafanikio lakini hawapo tayari kutoa kafara, kuachana na vile vizuri walivyonavyo sasa ili kupata vilivyo bora zaidi. Ukiweza kuvuka hilo, utaweza kupata makubwa.

Ukiondoa usawa kwenye maeneo haya 10 muhimu, utakuwa na maisha ya tofauti kabisa na utaweza kufanya makubwa sana.
Lakini utakapokua na maisha ya tofauti wengi watakushambulia, hivyo utakuwa kama mpweke katikati ya kundi kubwa la watu.

Nakukaribisha ujiunge kwenye jamii ya tofauti, jamii ambayo utakutana na wanaoishi maisha haya ya tofauti na kukupa nguvu ya kuendelea kuyaishi pia. Jamii hiyo inaitwa KISIMA CHA MAARIFA, kama bado hujawa kwenye jamii hiyo, wasiliana nami sasa kwa wasap namba 0717 396 253 nikupe utaratibu wa kupata nafasi kwenye jamii hii ya kipekee.

Usikubali tena kuendelea kuwa fair kwenye mambo yanayokurudisha nyuma.

Chagua kushika hatamu ya maisha yako ili uweze kufanya makubwa.

Rafiki yako anayekupenda sana,
 
Nimejifunza sana hapa yaan
 
Rafiki yangu mpendwa,

Kuna vitu waliofanikiwa sana wanavijua, lakini huwa hawaviweki wazi.

Wanafanya hivyo kwa sababu jamii huwa haielewi vitu vingi kuhusu mafanikio, na hivyo huishia kuwashambulia waliofanikiwa
Madini adimu haya, food for thought
 
Kuna watu wanajikita miungu watu hapa duniani. Na bado hawataki kujifunza kuwa tuko safarini. Dhamana walizonazo wanavuna laana kwa familia zao ndo mana mie Huwa sihangaiki whatever goes around come around and remember karma is bitch. .
Mbaya sana, familia za kiafrika zina miungu watu, mtu akiwa na tupesa kidogo tu anataka awatese ukoo mzima mum mumwabudu yeye
 
Watu wengi tunatamani Sana kufanikiwa kimaisha Ila Kuna Jambo lipo nyuma ya pazia ambalo hilo ndio kikwazo cha watu wengi kuishia kulalamika maisha ni magumu.

Kwa miaka mingi tumekua tukihubiriwa kuhusu kufanya kazi kwa bidii, kutunza pesa, kuwa na mikakati mizuri nk

Ninaamin hayo yote watu huwa wanayatimiza.

Kila mtu ameshawahi kufanya kaz kwa bidii Ila matokeo yake hakuna alichopata Ila bado anaendelea kupambana tu na unawezakuta had uhai unakuishia utakua bado hujafanikiwa.

Mafanikio yamejificha kwenye IMANI
Mungu/Yesu
Mtume Mohammed/alha
Mizimu
Waganga
Uchawi

Tafuta dunia nzima hakuna mtu ambaye amefanikiwa kimaisha bila kusaidiwa na kimoja Kati ya hvyo vitu nilivyoorodhesha hapo juu

Najua ni ukweli MCHUNGU hasa kwa wale walokole lazma wataanza kukemea baada ya kuona nimeweka mizimu na waganga.

Ni kweli suala la mizimu lipo na linafanya kazi.

Kuna watu hawafanikiwi kwasababu mizimu yao haipo sawa yaan wewe upo upo tu hata hela haikai mkononi Ila bado unajipa moyo one day yes utatoboa, my friend your wrong.

Ila Kuna watu wengine mizimu yao imewakubali hata asipo fanya kitu yeye pesa anazikamata tu yaan anakua na bahati Sana huwa tunawaita Wana kismati cha hela Ila ukweli ni mizimu yao ndiyo inayowasimamia.

Kuna wengine Iman zao zipo kwenye dini, hawa mafanikio yao ni mwenyezi mungu mwenyewe ndio anatoa baraka kwao na mtu huyu huwa anafanikiwa Sana kwenye mambo yake.

Waganga,. Hapa wapo matajiri wengi sana ambao wamefanikiwa kwa kutumia njia hii, Hawa wapo ambao wameuza nafsi zao au ambao wametoa kafara ya kitu fulani ili wajipatie utajiri.

Hapa bila shaka wale ndugu zangu wa kule Njombe hawana ubishi.

Uchawi, hapa sasa ni mtu binafsi anashiriki uchawi wa kimaendeleo, kwa mfano kumroga mtu ili upandishwe cheo, kuroga wateja wawe wanakuja kwako nk.

Ndugu zangu tunajitahidi sana kupambana na maisha Ila hapa kwenye imani wengi tunachemka. Chagua kimoja ukomae nacho utatoboa. Mimi nipo kwa Yesu๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿคช Ila msiniulize kama tayari nimefanikiwa kimaisha au la, ila nimeamua kuwafungulia code ambazo matajiri wengi hawazifungui wao wataishia kwenye:

Fanya kazi kwa bidii
Kuwa na kauli nzuri
Waheshimu watu
Jitume
Lipa kodi
Usifanye biashara haramu (japo wao wanafanya)

Mwenye akili aelewe na mwenye ubongo afunguke
 
Mbaya sana, familia za kiafrika zina miungu watu, mtu akiwa na tupesa kidogo tu anataka awatese ukoo mzima mum mumwabudu yeye
Unajua ukiwa na dhamana kubwa ukumbuke walio kuwa nyuma yako. Imagine unapata Hela ya kula ila Kuna watu wanateseka acheni tu. Hata sabuni hakuna. Yan hata kasukari kwenye chai Hawana. Ila Kuna watu wanakula na kutupa, laana watazipata kwa vizazi vyao sio ndogo. .

Mara nyingi angalia watu wanavyokifa ndo utajua kwa nini amekufa kifo Cha mateso na kibaya sana. Utakuja pata majibu. .
 
Acha kumsengenya shangazi yangu. Anatoa milioni tano sadaka ya ujenzi, wewe huna ada ya law school, ukimwomba anasema umechelewa kidogo tu, jana nimetoa hela ya ujenzi wa kanisa mil tano. Sina hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ