Ukweli Mchungu

Ukweli Mchungu

IMG-20221028-WA0011.jpg
 
 
Haiwezi kwenda dunia bila haramu kuwepo hata pig kitimoto mkuu wa meza anaitwa haramu na baadhi ya imani ila wanaokula hawapelekwi mahakamani hata siku moja

Haramu na iheshimiwe

Juzi nilikua kijiwe kimoja nimepoa na wadau, sasa kumbe mmoja wetu kwenye kijiwe hapo alikua na kiloba cha bangi mimi nilikua sijui maana ndio siku ya kwanza nmeenda kutulia niangalie wanavyocheza draft

Mara ghafla akaja kijana mmoja akaongea na yule jamaa mwenye kiloba, walichoongea mimi sikujua basi wakaelewana jamaa akaelekea kwenye kiloba akaanza kutoa bidhaa zimefungwa kwenye bahasha za kaki akampa

Jamaa akachukua ila hajakaa vizuri naona wametokea Jamaa wengine wawili wakiwa na pingu eeeh hatujakaa vizuri Jamaa katiwa pingu kawekwa chini kukaa sawa gari la polisi hili hapa

Wakamchukua mpaka central akawekwa huko wakaelewana na ilipofika jioni Jamaa akawa amerudi yupo kijiweni na kiloba chake cha bangi anauza pale pale km kawaida

Waliongea nini central wanakubariana nini mimi sijui ila itoshe kusema kwa kweli hakuna haramu ila wewe na Imani yako ndio inatafasiri ya hiki ni haramu na hiki sio haramu

Naweka karumu chini...
Swa my partner in crime
 
Back
Top Bottom