Ukweli mtupu: Rais Magufuli anafanana sana kitabia na aliyekuwa Rais wa Kenya marehemu Daniel Arap Moi

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
12,505
Reaction score
40,002
Mimi nikimuangalia Rais Magufuli kitabia naona ni kama Moi alizaliwa upya kuitawala Tanzania. Wanafanana sana kitabia na hizi ni baadhi ya tabia zao kwa jumla zinazofanana.

1. Wanapenda sana wasifiwe. Enzi za Moi zilitungwa nyimbo nyingi kumsifia kitu kinachoonekana kwa Rais Magufuli pia.

2. Kupenda kuonekana kuwa wanajali wanyonge na watu wa hali ya chini. Hapa ndipo mzee Moi alipojichukulia umaarufu wa jina la "Mzee wa Nyayo"

3. Kuhodhi vyombo vya habari yani kila kitu wakifanya lazima kitangazwe sana na vyombo vya habari. Aisee ulikuwa ukisikiliza vyombo vya habari vya Kenya basi zaidi ya nusu ya habari ni ya mtukufu Rias Moi. Siku za jumapili kila saa saba habari ya kwanza utasikia "Mtukufu Rais Daniel Toroitich Arap Moi leo amewaongoza waumini wengine katika kanisa la "Moi Kabarak centre" Kwasababu hili kanisa lolitajwa kila jumapili basi nilifanikiwa kulifahamu jina lake nikiwa mdogo sijaanza hata darasa la kwanza. Leo nani asiyefahamu kanisa la pale Osterbay? Maana halijawahi kuachwa kutangazwa, hata lile la Chato nalifahamu. Aidha ilikuwa ni marufuku kuweka taarifa ya Rais baada ya wengine kwenye habari. Yeye ni lazima awe wa kwanza.

4. Enzi ya utawala wa Moi kukosoa ilikuwa ni sawa na kula sumu. Kupata umaarufu zaidi yake ilikuwa ni kosa kubwa. Enzi ya utawala wa Moi ndipo viongozi wakubwa wa kisiasa waliuawa hadharani tena kwa kupigwa risasi. Ndani ya utawala wa Magufuli hili nalo ni doa kubwa sana la wakosoaji kuandamwa kwa kila hali.
 
hapa sio kwamba unakataa hoja ya mtoa mada! yaan kama ingekua moto nadiriki kusema unachochoea kwa speed kubwa sana. kurahisha ni kwamba umekubali utawala huu unaua wenye mawazo tofaut
Hawa wehu sasa hivi wamepagawa wanaropoka yale ya sirini wanayaweka hadharani. Ile albdari iliyosomwa kule Muheza baada ya Lissu kupigwa risasi inaanza kutoa majibu. Mpaka October watakuwa wako uchi wa mnyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Mwalimu Nyerere enzi za Utawala wake alifit kwenye hizo sifa zako 1-4 tena na zaidi.
 
Nenda Mji Wa Serikali Mtumba Ukajionee 😏😏😏😏
 
G Sam, Siyo Moi tu, Magufuli anafanana sana na Madikteta kibao...kafanana sana na Mobutu Seseseko pia, Mobutu alijenga International Airport kijijini kwake Ggabolite na Magufuli pia kajenga International Airport Chato kijijini kwake..
Mobutu alijenga Hotel ya kifahari kijijini kwake Ggabolite na Magufuli pia kajenga Hotel Chato ya kwake.
Mobutu aliifanyia nchi yake ufisadi wa kutisha Bunge halikuwa na maamuzi na Magufuli naye ni hivyo hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nikimuangalia Rais Magufuli kitabia naona ni kama Moi alizaliwa upya kuitawala Tanzania. Wanafanana sana kitabia na hizi ni baadhi ya tabia zao kwa jumla zinazofanana.

1. Wanapenda sana wasifiwe. Enzi za Moi zilitungwa nyimbo nyingi kumsifia kitu kinachoonekana kwa Rais Magufuli pia.

2. Kupenda kuonekana kuwa wanajali wanyonge na watu wa hali ya chini. Hapa ndipo mzee Moi alipojichukulia umaarufu wa jina la "Mzee wa Nyayo"

3. Kuhodhi vyombo vya habari yani kila kitu wakifanya lazima kitangazwe sana na vyombo vya habari. Aisee ulikuwa ukisikiliza vyombo vya habari vya Kenya basi zaidi ya nusu ya habari ni ya mtukufu Rias Moi. Siku za jumapili kila saa saba habari ya kwanza utasikia "Mtukufu Rais Daniel Toroitich Arap Moi leo amewaongoza waumini wengine katika kanisa la "Moi Kabarak centre" Kwasababu hili kanisa lolitajwa kila jumapili basi nilifanikiwa kulifahamu jina lake nikiwa mdogo sijaanza hata darasa la kwanza. Leo nani asiyefahamu kanisa la pale Osterbay? Maana halijawahi kuachwa kutangazwa, hata lile la Chato nalifahamu. Aidha ilikuwa ni marufuku kuweka taarifa ya Rais baada ya wengine kwenye habari. Yeye ni lazima awe wa kwanza.

4. Enzi ya utawala wa Moi kukosoa ilikuwa ni sawa na kula sumu. Kupata umaarufu zaidi yake ilikuwa ni kosa kubwa. Enzi ya utawala wa Moi ndipo viongozi wakubwa wa kisiasa waliuawa hadharani tena kwa kupigwa risasi. Ndani ya utawala wa Magufuli hili nalo ni doa kubwa sana la wakosoaji kuandamwa kwa kila hali.
Wote ni walimu, madikiteta, moi alimuua Robert ouko,
 
  • Thanks
Reactions: prs
Huwezi mlinganisha Moi na huyu kamongo!! Ukumbuke Moi ameitendea makubwa sana Kenya na zaidi sana alihubiri umoja na mshikamano wa taifa!!

Kumlinganisha Moi na huyo mshamba unakosea sana, na ukumbuke Moi alikua shupavu hasa baada ya mapinduzi dhidi yake kushindikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana!
Kwangu Mimi kuna Tofauti ndogo kati ya JPM na

1. Iddi Amin Dada
2. Mobutu Seseko

hakuna tofauti kubwa kati ya mobutu na jiwe
1.mobutu alipenda kusifiwa
2.alienda kanisani kila jumapili na media
3.alipotoa pesa za maendeleo zilitajwa kua ni misaada ya rais
4.mobutu alikua hakosolewi
5.mobutu alitumbua tumbua hata kama huna kosa utatumbuliwa tu
tofauti yao kubwa ni kwamba mobutu alipendwa sana amekuja kuchukiwa akiwa ameshatawala zaidi ya miaka 20

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom