Ukweli mtupu "Simba na Yanga zinabebwa!!!"

mbwewe

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2014
Posts
3,267
Reaction score
3,404
LIGI YETU HAIKO FAIR.
Simba & Yanga ni team ambazo kuchukua ubingwa wa VPL zinabadilishana tu ukiwa na upenzi bila jicho la tatu utasema wana deserve na wanavikosi bora . Lakini kwa jicho la kiutaalam na la tatu ni team zenye ubingwa fake na waupendeleo mkubwa ndio maana kombe kama la azam confederation na Mapinduzi makombe yenye fair competition huwa wana struggle sana.

Turudi VPL Yanga na Simba huwa wanapata point 3 free kabla ya ligi kuanza, kwann na sema hvyo RUVU SHOOTING NA JKT RUVU ni team ambazo kwa miaka ya nyuma zilikuwa zinaandaliwa kuwapa point 6, Mechi za hao wanajeshi kwa team mbili tu yaani simba na Yanga wanatumia uwanja wa Taifa huku team nyingine zote zinazobakia zikifuata utaratbu wa nyumbani na Ugenini THIS IS NOT FAIR.
Team Zooote kwenye ligi zinacheza Mwadui complex,Manungu na Mabatini Simba na yanga hawagusi hvyo viwanja vibovu huku kichekesho wakiifuata Njombe mji (SABASABA NJOMBE) ukiuangalia uwanja wa sabasaba hauna tofauti kabsa na manungu, mabatini & Mwadui complex .

Kwa mambo yote hayo team gan yenye uwezo sawa na hzo team ikachukua ubingwa ikiwa wapinzani wenu wanapewa point 6 kabla ya kucheza (nasema point 6 nikimaanisha ukicheza na ruvu Taifa ni tofauti na ukikutana nao mabatini ndio maana simba&yanga wanashinda goli 7 na wanashinda tenA sababu wanacheza mechi za ugenini nyumban kirahsi huku AZAM FC NA SINGIDA WAKIENDA MABATINI,MWADUI & MANUNGU.

Kwa hzo fever leo simba na yanga wanaongoza point 6 wanapata wap kwa wapinzani wao kama sio zile fever nilizo zungumza ? Wawekezaji wanashindwa kuwekeza kwa raha sababu ubingwa ni ngumu sana kuchukua mbele ya hawa Ndugu na Shirikisho lililo unfair.
HII INAUDHI NADHANI NADHANI NDIO SABABU UONGOZI WA AZAM ULIAMUA KUBANA MATUMIZI BAADA YA KUONA UBINGWA ULIVYO NA MILOLONGO MINGI PAMOJA NA KUGHARIMIA SANA. Narudi kwako hili walionaje???

cc@mdau kutoka fb
 
Simba na yanga ndio zinafanya wadhamini Wawe wengi ahahah
Tuwe wapole tu


Ni ukweli Kuna favaur nying zinapata zikipeleka maombi tff zinasikilizwa haraka kuliko zingine
 
Sababu ya kutotumia viwanja hivyo ni mapato tuu na si zengine...timu zote hutegemea gemu zao na hao Vigogo wawili wapige hela. Sasa unategemea wacheze gemu zao viwanja vya fensi ya Bati. Wanahamishia viwanja vikubwa wajaze washabiki wapige hela. Tafta hoja ingine
 

hoja sio mapato hoja ni fairness ....hii ni sawa na mtoto wa maskini agongwe na gari la tajiri halafu tajiri atoe hela ili kuua soo ili kesi isiende mahakamani ,mwisho wa siku kesi inaweza isiende mahakamani lkn haki inakuwa haijatendeka na hii ndyo point ninayoizungumzia " kanuni za ligi yetu zinasema timu zote zitacheza nyumbani na ugenini" sasa kwanini simba na yanga baadhi ya mechi zao wanachezea zote nyumbani? haki ipo wapi hpo?
 
kwahiyo umeliona hilo mwaka huu tu kwakuwa yanga ndio bye bye au

Na hili ndyo tatizo kubwa kwa watanzania!! mada imezungumzia simba na yanga we umechagua upande unaoupenda na usioupenda umempa mleta mada
 
AC Na Inter Milan wanatumia uwanja mmoja wakikutana kuna mechi huyu anakuwa ugenini. Huyu anakuwa nyumbani
Hata UEFA wakikutana ni hivyo hivyo Na goal LA ugenini linahesabika.

Kwa hiyo Yanga awezacheza Taiga Na akawa ugenini.

Mechi yoyote duniani kuna Wa nyumbani Na ugenini. Hata za World Cup Russia kuna mechi Argentina awezajikuta Yuko nyumbani.

Wawezasema out of point Ila Elewa hivyo hivyo.
 
Simba au yanga ikicheza na mwadui uwanja wa taifa kwani hawafahani mapato?hata timu za mikoani zikicheZa dar zinapata hela nzuri kwasababu mapato wanagawana
 
umemung'unya maneno, ungesema simba, yanga, na azam ni mabingwa wa kununua mechi. Akina Bocco wanakiwa hawajui kuwa mechi zinanunuliwaga wanajiona tu hawapati timu ulaya!
 
Point ya Simba na Yanga kubadilishana ubingwa sio hoja ya kusema wanabebwa.
Ebu angalia LA LIGA ni Barcelona na REAL MADRID.
Angalia GERMANY ni BUYERN tu. FRANCE ni PSG na ITALY ni JUVENTUS Je wanabebwa?
Jana umeona MAN U amepigwa na West brom tena OLD TRAFORD.. Kwani hao Mwadui wakishinda hapo TAIFA wananyimwa Point au.
 

umetoka nje ya mada hebu rudia kusoma tena!!........ni lini madrid wamecheza mechi dhidi ya levante au leganes zote santiago bernabeu yaani wasiende kucheza ugenini zote wachezee nyumbani?. singida na azam wanaenda kucheza uwanja wa mabatini wa ruvu shooting wenye pitch mbovu mno na wana struggle sana kupata matokeo wakati simba na yanga hawaendi mabatini mechi zote wanachezea taifa kwenye pitch nzuri .sasa hapo haki ipo wapi?
 
Ujinga mtupu, umekazana fever fever hujui ata ina maana gani, kwani umeskia hizo timu za jkt hazipendi kucheza kwenye kiwanja kizuri? Au wao wakishinda wana nyang'anywa ushindi?

Kwa taarifa yako tu kuwa hao wenyewe wanafurahi kucheza taifa
1. MAPATO wakicheza taifa watazamaji wanakuwa wengi hivo kupelekea na hizo team kupata mgao ambao unawasaidia kwenye mambo yao tofaut na wakicheza kwao hakuna majukwaa ya kukaa watu wengi

2. UBOVU WA VIWANJA, sijui unaongea tu au na mpira unaangaliaga, uliangalia mpira kati ya Azam na hao jkt kule mabatini? Match imehailishwa siku nzima kisa maji kujaa uwanjani, je unaongelea vp ubora wa ule uwanja?

Badala ya kuja na hoja useme ata TFF wahakikishe timu zilizopo VPL ziwe na viwanja vinavyokizi ubora unakuja na ngonjera za kitoto kwa watu wazima, hivi unazani matatizo yanazoeleka? Hao wenyewe wanapenda kucheza taifa na uhuru maana hali ya viwanja ni hovyo na vinahatarisha ata afya ya wachezaji
 

jkt wana rasilimali watu na vifaa wanashindwa vipi kuwa na uwanja wenye pitch nzuri na majukwaa? na unatakiwa ujue kuwa hpo kuna interest ya vitu viwili fairness na mapato na kinachopaswa kutangulia hpo ni fairness hatuwezi kuwa na league kila timu inatka kuchagua uwanja kwa interest zao huku tukiharibu dhana nzima ya ushindani na haki kwenye ligi
 
Mkuu tatizo lako unaongea sana alafu huna point, naomba nikuulize swali, umewahi kuskia wao wakilalamika juu ya hili? Kama hujawahi kuona, unazani wao ni wajinga alafu wewe ndio mwerevu sana?

I short hizi team zinajipatia kipato kizuri pale tu ambapo zikiwa zinacheza na either Simba au Yanga, hivo kwao kucheza taifa ni fursa, ila wewe umekazana kubwabwaja tu hapa,

Fairness gani unayoongelea wewe kwani ukicheza ugenini hurusiwi kushinda? Mfano ni team ngapi ambazo zimecheza na Simba na Yanga katika viwanja vyao ila still wamefungwa tena magoli mengi tu na sometimes zinakuja kupata draw au kushinda taifa?

We jamaa kweli hamnazo, kwamba unaposema kuwa jkt wana rasilimali watu na vifaa ila wameshindwa kujenga kiwanja kizuri kwahiyo unamaanisha hawana kiwanja kizuri ili wawe wanaenda kucheza taifa? Unajua kagera imeachukua miaka mingapi hadi kujenga ule uwanja wao? Kati ya kagera na hao jkt nani yuko vizuri? Kwanini club kama simba na yanga hadi leo hii hawana viwanja?

Mkuu mpira sio mambo yako achana nayo tu, huwezi kujua kila kitu ila ni vizuri kujua mambo mengi ila kwenye mpira ndugu yangu acha likupite tu utajua ata vingine
 
Umempa makavu live na kama akibisha ni kwakuwa ni mbishi tu au ana stres za timu yke mwakani haitaweza kupanda pipa
 
Kumbe unajua shida ni Pitch... hawalazimishwi wakigoma watasikilizwa.
 

we ni shabiki mandazi unanabwawaja km umekatwa kichwa, km ishu ni mapato basi ligi ichezewe dar es laam peke yake mi naandika for sake ya ligi yetu kuwa fair ili tupate bingwa halali na sio mambo ya ujanja ujanja ambayo mwisho wa siku tukienda kucheza kimataifa tunageuka kituko....we! umekalia ushabiki tu wa kuangalia maslahi ya timu unayoipenda bila kuangalia maslahi ya mpira wetu km nchi , kwenye kombe la fa kulikuwa na fair ground uliona kilichowatokea hao simba na yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…