Ukweli mtupu: Vijana wanasoma ili wakaibe

Ukweli mtupu: Vijana wanasoma ili wakaibe

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hello!

It's like a joke lakini ndio ukweli wenyewe.

Nchi hii wizi mbaya ni ule wa kuchukua mahindi mabichi shambani, kuiba kuku, kuiba simu , kuiba karanga , korosho, pipi na vitu vingine. Ila tukija kwenye wizi wa kisomi, wizi wa kwenye makaratasi huo wananchi hawana shida nao.

Mtumishi wa umma masaa 12 yuko kazini, hana biashara kando mshahara wake laki 5 lakini anaagiza gari Japani la milioni 20, kazini ana miaka 3 tu na hajakopa benki yoyote. Hana wasiwasi anaendesha kwenda na kurudi kazini. Aliyepaswa kumhoji na kumkagua naye ana hotel ya Billioni 1.5 huku mshahara wake ni sh. 2.5 ml. Na ana duka la viatu Kariakoo ambalo ndo kwanza lina miaka 3 tu.

Karibu Watanzania wote ni wezi sema chance watu hawajazipata.

Nani atalibadili hili Taifa?
 
Ajionavyo mtu ndivyo anavyodhani na wengine wapo.

Swali je unaamini watu wote ni waovu isipokuwa kwa sababu fulani? Au unaamini kuwa watu wote ni wema isipokuwa kwa sababu fulani?
 
Back
Top Bottom