Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Weekend hii nilikuwa na mzee mmoja mserikali àliyestaafu mambo ya uongozi. Katika mazungumzo yetu tukajikuta katika mjadala mkali kuhusu maliasili na rasilimali za wananchi.
Nikamwambia madini, maziwa, Gesi wanyama na maliasili zingine mali za wananchi wa taifa hili. Mzee yule akatabasamu kisha akaniambia
"Taikon nakujua kwa ubishi wako lakini nisikie, mwananchi hamiliki Maliasili. Maliasili sio mali ya wananchi isipokuwa mali za wanasiasa, watawala kwa kile kiitwacho serikali"
" Kitu pekee ambacho mwananchi anaweza kumiliki ni nyumba yake,gari na mambo yote yanayoundwa na wanadamu. Hayo ni yake na nidhuluma kuyachukua kutoka kwake. Ikitokea unayachukua lazima umpe fidia kwa sababu ni yake"
"Lakini hakunaga dhambi kwa watawala kuchukua au kutumia maliasili vile watakavyo. Kwa sababu maliasili ni mali halali ya watawala na wanasiasa"
Mwisho wa kunukuu!
Sasa Taikon kwa ubishi wangu niliachana na yule mzee kwa kinyongo baada ya kunichana. Ingawaje ni rafiki yangu lakini hoja yake hii imenipa mtazamo mpya.
Sasa nimelileta huku tujadili.
Je ni kweli Maliasili sio mali za wananchi. Bali mali za watawala au wanasiasa kwa jina lao waliitalo serikali?
Yaani bahari, madini, gesi, mbuga, maziwa,ardhi miongoni mwa maliasili zingine.
Kwenu wanazengo.
Robèrt Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam