Ukweli ni kwamba hakuna mwanaCHADEMA aliyewahi kupambana na CHADEMA na akashinda, wengi wanaishia kudhalilika tu hata kama watapewa vyeo

Ukweli ni kwamba hakuna mwanaCHADEMA aliyewahi kupambana na CHADEMA na akashinda, wengi wanaishia kudhalilika tu hata kama watapewa vyeo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Huu ndio ukweli unaofahamika kila mahali, mifano ya waliokuwa wana CHADEMA na kusaliti chama chao waliodhalilika baada ya uamuzi wao huo ni mingi mno, hatuna haja ya kuirudia, ni kweli kwamba kuna waliopewa vyeo baada ya usaliti huo lakini heshima yao mbele ya jamii imepukutika mithili ya majivu kwenye upepo mkali.

Kwahiyo wanachopaswa kutambua wasaliti wapya na wajao ni kwamba usaliti wao utawagharimu heshima na utu wao mbele ya jamii kama ilivyowagharimu wasaliti waliopita ambao sasa wamepoteza kila kitu mbele ya Jamii, japo wamepata hela baada ya kununuliwa, hawaheshimiki na yeyote na wamedharauliwa moja kwa moja.

Muda utaongea...
 
Huu ndio ukweli unaofahamika kila mahali , Mifano ya waliokuwa wana Chadema na kusaliti chama chao waliodhalilika baada ya uamuzi wao huo ni mingi mno , hatuna haja ya kuirudia , ni kweli kwamba kuna waliopewa vyeo baada ya usaliti huo lakini heshima yao mbele ya jamii imepukutika mithili ya majivu kwenye upepo mkali...
Namalizia
"Mungu ibariki CHADEMA"

Hii sentensi huwa inanikosha sana kwenye nyuzi zako.
 
Kama chama kina jeuri kina jiamini kiwatimue tuu uanachama lakini pamoja na hayo wakidanya hivyo msaada kutoka nje nao watakosa maana kitakuwa hakina wawakilishi bungeni
 
Wacha Magugu yaende Mkuu...
Haya magugu chadema uwa hayaishi ninni? Sasa tutajuaje waliobaki kama siyo magugu. Yani kama mtu kama Halima naye kawa gugu duh! Kila mwaka mnasema magugu magugu yameondoka now CHADEMA iko stronger than ever mara kumbe kuna magugu mabaya zaidi kama hawa walinunuliwa kwa njama kama za Mossad
 
Inategemea, kuna watu utu na heshima yao kwa jamii si kitu mbele ya pesa. Hao hawapata hasara yoyote katika hilo bali 'faida'
 
Katiba ya Chadema imeweka wazi kabisa kuhusu adhabu ya wasaliti , maamuzi si yangu ni ya kamati kuu , na wala hayaangalii chochote zaidi ya kuwashughulikia wakosefu bila huruma yoyote , mtu pekee kwenye kundi lile anayeweza kunusurika ni Nusrat .
Ahaa basi tusubiri hiyo tarehe 27 kwenye kamati ya maadili tusikie wataambiwa nini
 
CHADEMA inabidi ing'olewe kutoka kwenye makucha ya viongozi wenye tamaa na wasio na maono na kuiwekewa kwa mikono ya wananchi kama taasisi. Mh. Aida Khenani Mbunge wa Nkasi, ameonyesha ukomavu wa kisiasa kuliko uongozi mzima wa CHADEMA
 
Wanaume wa CHADEMA mna roho mbaya kama mashetani au majini wabaya. Hao akina mama hawajaenda kuapishwa hivihivi.Kuna jambo ndani ya CHADEMA.Ukiona jibwa lipo kwenye mti kileleni juu uje kapandishwa huyo na mwenyewe yupo.Hata muimbe mgaregare chini hizo nafasi ni za wanawake.Waacheni hao !
 
Haya magugu chadema uwa hayaishi ninni? Sasa tutajuaje waliobaki kama siyo magugu. Yani kama mtu kama Halima naye kawa gugu duh! Kila mwaka mnasema magugu magugu yameondoka now CHADEMA iko stronger than ever mara kumbe kuna magugu mabaya zaidi kama hawa walinunuliwa kwa njama kama za Mossad
Magugu yapo na ngano zipo
michujo itaendelea mpaka tutakapotoa mfumo huu kandamizi... kama Gedion alianza na watu zaid ya 20 akabaki na Mia tatu tu na akashinda vita....
Tutabaki wachache lakin Mapambano yataendelea ni swala la muda tu
 
Kila ikikaribia Uchaguzi ndipo magugu yanaanza kuonekana na baada ya Uchaguzi. kama hawa waliokuwa makamabda wakuaminiwa frontline kabisa wana njaa za namna hii sijui wengine wana njaa kiasi gani
 
Back
Top Bottom