Ukweli ni kwamba wapalestina hata wakiuwawa na waisrael pale sio kwao warudi walikotoka

Nimekupata mkuu, kwa hiyo kwa sababu hao wayahudi ni feki na hao ndugu zao ambao ni wapalestina ni feki pia?
 
Wakiwa na: nia, na nguvu ya kuwawezesha kurudi walipotoka na kuwashinda waliojimilikisha hapo mbona watarudi mapema tu?
Ila point yangu mkuu ni kuwa, hao niliowataja na hata hao uliowataja wewe, wengi wao waliwashinda waliokutwa hapo waka-settle na wote tunaona ni kawaida. Ila kuna kelele mno kuhusu wayahudi wakati trend ni ileile!
Unafiki huu upo pia ukiangalia majengo yaliyokuwa makanisa kule uturuki, yanatumika kama misikiti na hawa 'watetezi' wa haki hawasikiki kabisa kuliongelea hilo!
 

Kabla ya kuanzisha kwa taifa la "Israel" japo 1948, katika koloni la Muingereza la "Mandate of PalesrPal" walikuwa wakiishi waarabu na "wayahudi" bila chagizo zozote zile ....Soma historia .
Tukichukulia uhalali wa kitabu cha dini , basi Dunia inabidi iamini dini moja ili tuweze kuhukumiana ila kama hatuna dini moja, hoja ya dini inakosa mashine , kwa maana anaweza kuja mwengine akadai ye kaahidiwa Tanzania ya leo , tumor uhalali kutoka a na vitabu vyake ? Tusishabikie sábana dini bila ya kutumia akili.....
Kama ardhi ya ahadi , basi waanze mto Nile na wafike Hadi Euphrates kule Iraq , wasisite ili kwamba *ahadi yao waitimize* .....
 
Nimesema waarabu wa kiislamu walivamia eneo ambalo sio Lao


Kumbuka pia Kuna wakristo wa kipalestina ambapo nao hupata tabú Pía , kama unaamini Mungu wa Wayahudi ni wako Pía , basi elewa ya kuwa Wayahudi bado wanamsubiri Masía, kwani kwao Yesu ni nabii feki .....

Je leo watutsi na wamasai warudishwe Ethiopia ? Historia ipo wazi !!! Wangoni kule Afrika kusini ? Na Falasha basi poa wachukuliwe wote ili nao wafaidi "nchi ya ahadi" , Au ni mpango endelevu kwa wayahudi weupe tu ?? Weusi ulishakoma tokea miaka ya 90 ?? Na wale wa Zimbabwe nao vipi ? Au mweusi sio Myahudi ???
 
Hao ndio wanameza maandiko km yalivyo hawahoji huo ni upoyoyo, Wayahudi wanaajenda zao chafu za kutaka kutawala dunia.
Yesu kwao sio nabii ila kunakiumbe chao wanachokisubiri.
 
Nimekupata mkuu, kwa hiyo kwa sababu hao wayahudi ni feki na hao ndugu zao ambao ni wapalestina ni feki pia?
Yaani nachosema wapalestina wa sasa na wayahudi feki wana DNA moja haijalishi nani ni feki nani sio feki ila hoja ni kwamba kama mnashare chanzo kimoja hiyo hoja ya kusema huyu sio ardhi yake maana sisi tulipewa na mababu zetu inatoka wapi wakati babu yenu ni mmoja

Nachotaka msiweke undumila kuwili mtuambie kivp israel ana haki ya hapo kuliko palestina kwa muktadha huu nasubiri
 
Hao ndio wanameza maandiko km yalivyo hawahoji huo ni upoyoyo, Wayahudi wanaajenda zao chafu za kutaka kutawala dunia.
Yesu kwao sio nabii ila kunakiumbe chao wanachokisubiri.
Walishasema masiha wanaemsubiri ni binadamu sio mungu MTU,atazaliwa na watu na ndie ataliongoza taiga la Israel kuitawala dunia na kuwepo na serikali moja ikitawala toka jerusalem
 
na kwa kumuongezea tu swali jengine, je kama mungu ni wa wote, je hao waliotumwa kuja kupambana nao wao mungu wao alikua nani? Au hawakua na Mungu? Je Huyo Mungu ni wa wote?
 
Enzi hayo yanatokea dunia ilikuwa haiendeshwi kwa sheria zaidi ya kiimla kwenye falme nyingi ila miaka ya sasa kuna kitu kinaitwa sovereignty ambayo sheria za kimataifa linasimamia ndio maana hata urusi alipovamia crimea haikujalisha sababu ila ilipigiwa kelele na dunia nzima na hta kuwekewa vikwazo sasa nipe mfano wa nchi ambayo ilikaliwa kimabavu na dunia haijapiga kelele toka kuanzishwa kwa league of nations (mtangulizi wa UN) ili sasa ndio tuihalalishe israel kuwavamia palestina
 
Wakati abraham anatoka Uru kuianza safari alifika harani wakaweka kambi ya mapumziko hapo waliishi mda mrefu tu kabla hawajaamua kuondoka hapo kuendelea na safari yao kuelekea kanaan wakavuka mto huo unaoutaja hapo bado walikuwa hawajafika wakaweka kambi huko more sehemu iliyokuwa na miti mingi
Baadae wakaendelea na safari kupitia Syria ndipo wakafika walikokuwa wanaenda kanaan
 
Mimi sizungumzii habari za wakristo na waislamu hapa Bali ardhi ya waisrael
Waamini au wasiamini mimi hainihusu natetea umiliki wa ardhi yao waliyopewa milele
Cha msingi hao waarabu wa kiislamu wanaopigania ardhi isiyo yao wasepe au wakubali masharti ya Wenye ardhi
 
Huo ni upoyoyo, hawamuamini YESU hata kdg, wao wanamuamini Musa.
 
Daah mkuu, unahitaji ukombolewe kifikra.
 
Daah mkuu, unahitaji ukombolewe kifikra.

Huyo anaonekana Myahudi mweusi mwnye misimamo mikali,hasikii wala haambiwi kitu na hataki kuelewa kingine zaidi ya kile alichoaminishwa,kwa hiyo ndugu huo ukombozi unaotaka akombolewe sijui ni ukombozi wa aina gani utamkomboa.
 
Huyo anaonekana Myahudi mweusi mwnye misimamo mikali,hasikii wala haambiwi kitu na hataki kuelewa kingine zaidi ya kile alichoaminishwa,kwa hiyo ndugu huo ukombozi unaotaka akombolewe sijui ni ukombozi wa aina gani utamkomboa.
Anamuhuri tayari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…