BC: Wapenzi wengi wa muziki, tukiwemo sisi hapa BongoCelebrity, tungependa sana kujua, je wimbo wenu ujulikanao kama Dingi ni kisa cha kweli au utunzi tu? Nani alitunga wimbo huu?
DOMOKAYA : Nyimbo hiyo ya “Dingi”
nimeitunga mimi mwenyewe hapa. Mimi kama Domo,lakini pia wakati natunga, nilikuwepo na mwenzangu
ManDojo. Ila kisa chenyewe kinanihusu mimi zaidi. Maisha yangu pamoja na nilivyoishi na baba yangu. Lakini kuna vitu venginie kidogo tumetunga kama vionjo vile ili verse itoshe na ili uweze kusikiliza. Lakini part kubwa ya lyrics ni true story. Yaani hata mama na kina mamdogo huko wanapousikia huu mwimbo
wanaona kabisa ‘huyu kamwimba baba yake huyu’ kama nilivyokwambia sisi tukitunga nyimbo tunajaribu kutunga kitu kile kile ambacho kinatokea katika maisha ya kila mtu, kama mimi yamenikuta yale yalionikuta mimi na baba yangu, kuna watu wengine yamewakuta mabaya zaidi na baba zao kuliko yalionikuta mimi ,unaona? Kwahiyo kila unapoandika na unapowakilisha wengi sana yanawagusa pia.