Ukweli tuuweke hapa kuhusu Kassim Mganga!

Kwanza, Kibongo bongo Kassim Mganga ameshatoka kitambo lakini hii si dunia ya kutegemea kazi ulizofanya mwaka mmoja uliopita! Hata kama umetoa ngoma kali namna gani, baada ya muda mfupi watu wataisahau kv wana access ya kuisikia/kuiona wimbo wako hata mara 100 kwa siku kiasi cha kufikia kukifu!

Katika mazingira kama hayo LAZIMA uwe active... uwe unatoa ngoma mara kwa mara jambo ambalo Kassim hafanyi!

Kutoka nje ya mipaka ya Tanzania, kwa staili yake ni ngumu kidogo! Ngoma nyingi za Kassim ni radio version kwahiyo ku-attract attention ya watu wasiofahamu lugha husika inakuwa mtihani hadi iwe tayari una hiyo audience (of non Swahili speakers)!
 
Jamaa yuko vizuri , ni msanii pekee aliyeyoka Tiptop na still anaendelea kutoa ngoma kali
 
juzi kati nilibahatika kushuhudia show yake huku sumbawanga kwa kwel jamaa ni noumaa
 
Tatizo lake Mwinyi mno yule Mdigo....ila kuhusu mziki wake jamaa ni mkali mno
Mzaramo,
Sina la kuongeza sentensi fupi lakini umeonesha ''udhaifu'' wa nguli huyu wa mistari. Inabidi Cassim Mganga hii tabia ya umwinyi aiache ama sivyo ataishia kualikwa ktk shughuli za harusi.

Maana umwinyi humfanya mtu kutofanya makubwa zaidi na kutosheka kwa umaarufu wa "mitaa ya kwao" wakati kuna kila dalili anaweza "kutoboa" kikanda na kimataifa.
 
Ofcoz kasssim ana imba vizur lakin kabweteka utafikili mziki Unataka ivo amuulize Mwenzake kiba Asaivi kashituka Nini afanye Ili awe juu ila kassim anasauti Poa sana
 
kweli ase kassim yupo vur sana,kwa kwel mana ana mashair mazur meskiza ngoma yake manuari' ni nzur anjua sana mziki.
 
Kuwa na kipaji na kuwa mbunifu kwenye biashara ya muziki ni vitu viwili tofauti
 
Kassimu anajua kuimba sana,
Japo mi mashairi ya kiswahili sana huwa siyafagilii kivilee no wonder sio msikilizaji wa taarabu.
Mie ni mpenzi wa mashairi fulani hivi yakihuni huni & Swaggz kibao (Mtu mzima ninayependa uhuni). [emoji85]
 
Sasa kama Kassim ni Icon ya bongo je Diamond Platnumz baba tifah Dangote mtoto wa tandale young bilioner, icon ya africa mashariki na kati na mashariki ya mbali a.k.a Simba, Kifaru, atakuwa nani sasa?
Mahaba yakizidi muone daktari[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Msanii pekee anayefanya vizuri baada ya kuondoka Tip top wengine wote chali [emoji12]
 
  1. Nitakutunzia penzi manuari
  2. Chini nipige mbizi kwa safari
  3. Kukuangusha siwezi ni hodari
  4. Nitalilinda na kulienzi kila hali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…