Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
The world at large.. They were born/brought for the special purpose! Siri za hii dunia ni nyingi na nyingine zinatisha sana.. Hawa ndio wanaiendesha dunia N they are big minds. Very big minds! Wanacheza na nambari na wako mbele ya wakati
Very powerful 💪Uongo alimwambia Ukw eli, "Hebu tuoge pamoja, maji ya kisima ni mazuri sana.
Ukweli, akiwa bado na mashaka, alijaribu maji na kugundua kuwa ni mzuri. Basi wakavua wote nguo wakawa uchi na kuanza kuoga.
Lakini ghafla, muongo akaruka kutoka majini na kukimbia, akiwa amevaa nguo za Kweli.
Ukweli, kwa hasira, alitoka nje ya kisima na kumkimbiza uongo ili kuchukua nguo zake.
Lakini walimwengu, walipoona Ukweli ulio uchi, ulitazama pembeni, kwa hasira, dharau na aibu
Maskini Ukweli ulirudi kisimani na kutoweka milele, kuficha aibu yake.
Tangu wakati huo, Uongo unazunguka ulimwenguni kote, umevaa kama Ukweli, na jamii ina furaha sana..... kwa sababu ulimwengu hauna hamu ya kujua Ukweli ulio uchi.
Happy new year in advance.. The naked truth is gone forever
Hapo ndio mnaharibu kwa kujifichaficha ......By the way,leo Dec. 31, ni kati ya siku nne za Kalenda ambazo ni Sikukuu ya Shetani. Siku nyingine Sikukuu ya Shetani ni Mei Mosi yule jamaa,I forget his name,alipoanzisha Illuminati,yes, Adam Weishaupt.
kabisa,Pamoja na kwamba uzi unahusiana na ukweli lakini Mimi ni muumini mkubwa wa uhalisia kuliko ukweli
Truth is not that much pure than reality!
Truth is half empty and reality is empty half! Je tuko pamoja?
Mungu Ibariki Tanganyika.. Ndio nchi yetu ya asili... Tanzania ni uongo mwingine uliovaa nguo za ukweli😭kabisa,
hicho ndicho gentleman,
nilichojaribu kueleza kwenye reply yangu ya kwanza, ni mfano tu wa namna uongo unavyopewa kipaumbele kwenye masuala muhimu mbalimbali mathalani siasa, kuliko ukweli na uhalisia wa mambo.
ndio maana ndege ya abiria unaweza kudunguliwa makusudi, lakini uongo unaingilia kati na kuonekana jambo hilo ni bahati mbaya ni makosa ya kiufundi tu.
Au hospitali ya watoto yenye wagonjwa wasio jiweza, inaweza kulengwa na kulipuliwa makusudi, halafu uongo unaingizwa kwamba eti ni katika kujilinda hilo limetokea, eti wahalifu wamejificha humo.
Ama kwa hakika tangu ukweli ulivyo rudi kisimani na kutoweka milele kuficha aibu yake, na kisha nguo zake kuvaliwa na uongo,
hadaa na uzushi kupitia teknolojia vimeipumbaza dunia na kuwafanya walimwengu kushabikia na kufurahia uongo, kanakwamba ni kweli.🐒
Mungu Ibariki Tanzania