Du yaani uzi mmoja umeufungua mara mbili, ila hivyi blue ivy, North West je unawasikia mpaka sasa eti au ina maana Jay z (album yake iliyotoka mwezi wa sita imegonga platnumz ndani ya wiki), beyonce (msanii aliyepiga ila ndefu kupitia tour yake mwaka jana kuliko msanii yoyote), Kanye West (anauza sana viatu) na Kim umarufu wao umeporomoka. Mimi ninachokushauri fanya shughuli zako, diamond platnumz kweli atashuka kimziki lkn sio kwa sasa, acha kulazimisha ndugu yangu, huyu jamaa bado sana, kama umaarufu wake umeshuka basi diamond karanga zingedoda, lkn ukitembea barabarani vipakti kibao vya diamond karanga na kama umaarufu wake ungeshuka marry me isingeshika no 1 wiki mbili mfululizo trace na kukaa ktk 5 bora zaidi ya wiki nne MTV na hivi sasa MTV fire inashika no 6 ktk chati za nyimbo za Africa, hapo bado hujaja ktk mikataba, kama umaarufu wake umeshuka coca cola, GSM mall, Vodacom (wanadhamini tour ya WCB mwaka huu mikoa 11) nk wasingempa mkataba na juzi juzi Kenya kaingia mkataba na Safaricom, sasa jiulize huyo msanii wako unayempenda ww kwa mwaka huu ana hit ngapi na mikataba mingapi, hata basi wa kampuni za pipi hana, hapo sijagusa YouTube (Kuna mdau alisema millard ayo anapiga ela ndefu je diamond platnumz atapiga sh ngapi wakati yy ndiye msanii mwenye view nyingi kuliko yoyote East Africa) ,hapo sijagusa wasafi.com. Sasa sikuelewi unavyosema umaarufu wake umeshuka alafu kaa ukijua huyo ni mtoto hata hao mastaa ulaya mwanzoni mwanzoni utawasikia watoto wao wakitrend lkn baada ya mwaka inakuwa kawaida. Ila kwa ushauri usimchukie diamond platnumz kwani ukimchukia utapunguza siku zako za kuishi, alafu moyo wako utakuwa umeufunga na chuki na mungu atashindwa kukubariki, alafu jamaa hashuki leo wala kesho.