Unajua kuna muda unawaza kizembe zembe tu..Mfano Iran,Korea kwa Kim Jo kule...Russia na Marekani mwenyewe si kila baada ya miaka minne wangekuwa wanabadilishana Kombe la dunia.
Na hata ligi zao pia zingekuwa bora mno..mana majeshi yao yana nguvu na wanafanya mission za kuogofya hapa duniani.
Niliposikia ile kauli sijui kama ni mimi ningeweka beki mwanajeshi.Nikajiuliza mbona JKT Uljoro na wale Polisi Dom,Moro si kila mwaka wangekuwa na makombe daraja la kwanza na Ligi kuu.
Akili ya kumeza meza mavitu darasani na ufahamu na utulivu na hekima zimetoweka miongoni mwetu kwa sasa.Na ndipo nilipoona sina haja ya kuishabikia timu ya namna ile japo nilikuwa nimeipenda sana.Tunaleta masimamngo na majivuno kuwa timu ya taifa ni ya kikundi flani.Waendelee watazidi kuona majibu yao taratibu.
Kama vipi watengeneze tu Timu ya jeshi na Polisi tuone matokeo ....mana hakuna cha ziada ya hapo...ndio ukomo wa fikra na tafakari za baadhi yao.