Kwa Tafsiri halali maana halisi ya uzalendo ni pamoja na kuongea ukweli ( Nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko ) , mficha maradhi mauti humuumbua , nimeanza na hili la uzalendo maana limetumika sana na mamluki ili kufifisha mijadala yenye tija , Uzalendo siyo Uzuzu au ubwege , uzalendo ni pamoja na kuhoji mambo mazuri au mabaya yanayoonekana kwenye jamii yetu , kuwa mzalendo haimaanishi kwamba wewe ni ndondocha uliyeng'olewa ubongo , ni lazima ifahamike humu jf na kwingineko kwamba kuhoji si kosa .
Ni dhahiri Watanzamia wamegawanyika kabisa kuhusiana na timu yao na mpaka sasa Haijafahamika sababu hasa ya watanzania kugawanyika kiasi hiki , uchunguzi wangu umebaini kwamba wanaoishangilia ni wachache mno kuliko wanaozomea , huo ndio ukweli ambao baadhi ya watu wanataka ufichwe , ni vema wadau wakajiuliza hali hii inatokana na nini , kujua sababu za hili ni nusu ya jawabu , toeni madukuduku yenu , sababu hasa ya kuitosa timu yenu ni nini ?