Darrasa ametoa wakati sahihi ila tatizo album haukupewa promo,ila album yake kali.
Si unajua siku hizi radio promo wanawapa Ali Kiba na Konde wakiamini wanawakomoa WCB,hili bonge moja la mistake na inawaumiza sana wasanii wasiokuwa kwenye makundi.
We si unaona promo aliyopewa Konde alivyo zindua album,imerushwa live na media mbili Clouds na EFm,imepewa promo zaidi ya mwezi.Kiba wakati anatoa Mvumo wa radi alipewa promo siku nzima kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa tano usiku hii haijawahi kutokea kwa msanii yoyote zaidi ya Kiba.
Beef la Clouds,Efm,EATV,Harmonize na Kiba against Diamond na Wasafi lina waumiza sana wasanii wasio husika huku Harmonize,Kiba na label zao wakipata promo na airtime ya kutosha kuliko wasanii wengine.
Wewe Barnaba mtoto wa CMG katoa album juzi lkn hajapewa promo ya kutosha,Young D naye hivyo hivyo,hata Jux nae,Navy Kenzo nk hawa wote hawakupewa airtime ya kutosha kabisa.
Hili beef lina faida kwa Diamond,Harmonize na Kiba na si kwamba labda ni wasanii wakali kuliko wenzao bali ni watu waliokuwa pamoja baadae wakafarakana.