Ukweli usemwe, Yanga wametuacha Mbali sana upande wa Jezi

Simba lunyasi

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2022
Posts
385
Reaction score
840
Hivi Uongozi wa Simba kwanini usitoe masharti kwa Vunja bei yenye kumfanya atengeneze jezi zenye viwango vyao klabu kama Simba? Yaani kitendo cha kumpa mkataba ambao haumbani ndio kinachofanya tuletewe haya madekio ambayo hata sokoni yataenda kudoda.

Jezi hazina ubunifu wowote, jezi hazina ubora wowote yaani ni Bora liende tu. Kwa kuwa mtani kazindua jezi eti nayeye vunja bei ili asionekane yupo nyuma nayeye kaleta matambala yake sokoni..

Kiufupi vunjabei anapaswa ajitafakali maana jezi za hii miaka miwili ya udhamini wake ni takataka sana[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
 
Yaani hayo madaso yanauzwa elf35? Kweli mbumbu FC ni shamba la Bibi!
 
W ni guluguja kweli, watu wanawaza malengo makubwa ya kufika mbali zaidi kimafanikio w unaongelea mambo ayo hayakupeleki kokote....ngoja tusubir utopolo kama hyo jezi itawasadia kufunga magoli. W ni utopolo bila kupepesa macho.
 
Jersey zenye thamani duniani zinaonekana hivyo kutokana na ubora na mafanikio ya timu husika. Kuna jerseys nyingi tu duniani ziko very simple lakini zina thamani.

Italy ambapo madesigner wakubwa wa nguo duniani wanatokea, jezi zao za national team hazijawahi kubadilika sana na ziko simple mnoo. Real Madrid wanavaa all white, jezi hazina mbwembwe ila uwanjani mziki wao unajulikana. Liverpool, France....

Hivyo hivyo kwenye masuala ya Logo. Wanasema "simplicity is the ultimate sophistication".
 
Mtani wetu kachemka kwenye jezi. Ila kwa kuwa anamwambia MTU WA NJE KWAMBA AJE A-VISIT TANZANIA, sio mbaya sana. Ila VUNJA BEI ANAWAZINGUA.

Na kwa kujua kwmba jamaa anawazingua, ni pale NAE ANAPOAMUA KUJITANGAZA KWENYE JEZI YA SIMBA…!!!

Sijaona SHERIA NGOWI AKIJITANGAZA KWENYE JEZI YA YANGA…!!! Amefanya kazi yake VIZURI na AMEACHA YANGA IMTANGAZE KWA KAZI YAKE NZURI…!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…