Ukweli Usiosemwa: Hakuna Chama cha siasa wala Mwanasiasa anaeipenda katiba ya Warioba

Ukweli Usiosemwa: Hakuna Chama cha siasa wala Mwanasiasa anaeipenda katiba ya Warioba

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
19,629
Reaction score
34,199
Wanasiasa wote nia yao ni moja: Pesa na Madaraka.

Kwenye pesa na madaraka kikweli haijalishi ni chama gani, mtauana.

Hizi kelele za katiba zinapigwa na watu wasionufaika na katiba iliyopo, ila ikitokea na wao wakapata madaraka ndani ya katiba hii hii, msitegemee tena katiba ya Warioba. Sahauni kabisa.

Suluhisho kamili ni namna ya kuwafanya wanasiasa waheshimu matakwa ya wananchi.

Katiba haipaswi kuwa jambo la mwanasiasa kwasababu siku zote anajiangalia yeye tu namna anavyowrza kunufaika.

Wananchi tupambanie mamlaka ydtu kwa uangalifu, ila tuhakikishe hayaanguki mikononi mwa chama cha siasa tena.
 
Huyo mwananchi naye akipata madaraka atajiangalie yeye kwanzA....africans tumelaaniwa aisee..atajifanya mtoto wa masikini..kumbe ndio anakusanya tamu zote za nnchi.

Kama nakudanganya mwambie Mpango aliyejiita mtoto wa masikini..na anajua shida za watanzania..atoe posho zake zote na apunguze nusu ya mshahara wake uwasaidie masikini wenzake..
 
Huyo mwananchi naye akipata madaraka atajiangalie yeye kwanzA....africans tumelaaniwa aisee..atajifanya mtoto wa masikini..kumbe ndio anakusanya tamu zote za nnchi ...
Target ya mwananchi siyo madaraka. Ni ubora wa maisha yake.

Mahitaji makubwa ya watu ni Ajira, biashara, Uhuru, usalama, haki, masoko ya bidhaa, bima n.k
 
Back
Top Bottom