Ukweli usioujua kuhusu biashara

Kwa buku 50 niliyonayo nitatoboa kweli, ngoja tu nikauze viepe mana havina kodi wala uhuni
 
Mimi namshukuru Mungu nimekula chumvi,nina uhakika na hili jambo nitakalo kuambia.....
UKWELI wafanya biashara baadhi huyafanya hayo.........lakini maisha yao yanakuwa ya mateso sana,mfano kama hatakuwa na mtoto teja,atasumbuliwa na maradhi au mitihani katika ndoa au mikosi na balaa za kila aina.
Kwa wale wanaofanya halali inakuwa ni kunyume chake......kwenye kodi hawaibi hata mia,hawadhulumu mtu,wanatoa sadaka,hutoa misaada sana na kamwe hawataki kutangazwa.
 
Kariakoo nimeuziwa jeans hilo ukivuta kidogo tu linatatuka daah
Hizo jeans zinakuwa zishaoza kwahiyo wanachofanya wanawapa wale wanangu wanaomwaga chini wapige mnada. Au wao wenyewe wanakuonesha jeans ya sample unaiona ipo fresh ila kwenye kufungiwa sasa ndo unapewa zilizooza.

Ilinikuta hiyo 2020 nikachukua mzigo wa duka wa kutosha, nilichokutana nacho sitokuja kusahau daima. Ndo maana siku hizi nikitaka kununua kiwalo dukani lazima nikikague kama vile kina kunguni
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hapo kwenye cement ni mwendo wa kupiga bomba kila mfuko unapunguzwa 5kg hadi 10kg

Kwenye nondo kuna nondo za kimagumashi kuanzia ubora mdogo na dimensions za uongo, utakuta nondo ya 12mm iko kama ya 10mm. Na zinauzwa bei sawa na zile zenyewe mafundi ndo huwa wanazitambua
 
Vitu feki feki na watu wanasifu hali hiyo
Hii yote lakn ni sabb ya jamii wengi ni wa kipato cha chini
 
Nyie biashara ni ngumu sana ndo maana statistics za mwaka jana ya sensa zinasema vijana waliomaliza chuo wengi wanasubiri ajira. Wengine wamejiajiri na wengine wamekataa kujiajiri wanasema liwalo na liwe.
Tatizo ni kwamba unakuta wengi hawana family background kuhusu biashara so unapoanza biashara huna background ni kama unaanza na sifuri sasa Kuna matatu, eidha upandishe hiyo sifuri au ubaki hapohapo au udondoke kwenye negatives.
Ndo maana usijaribu kitu chochote bila kujua risks zake.
Pia kitu jingine ukijifanya Mtakatifu sana kwenye biashara hutoboi, katafute ajira.
 
Kifupi unataka kutuambia kuwa kupigwa kwenye nchi zetu za dunia ya tatu hakukwepeki...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…