Ukweli wa dhati wa mwanadamu: Mume/Mke uliyenaye unaweza kuta wewe wala siyo chaguo lake

Tman900

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
589
Reaction score
1,897
Katika Dunia, kuna mengi ila mume/mke ulie nae, unaeza kuta katika ukweli wa ndani wa moyo wake wala wewe ulie nae sio chaguo lake, ila yuko na wewe ili mladi tu maisha yaende.

Yaani unaeza kuta mwanaume/mwanamke yuko katika uhusiano lakini hisia zake na upendo wake wa dhati uko kwa mwingine kabisa.

Miyoyo ya wanadamu imebeba mengi, ikitokea ukapata nafasi ya kuujua ukweli wa mwenza uliyenae ndio utajua binadamu wanasiri katika nafsi zao.

Nanuukuu kauli, "Kweli nimeolewa unadhani mimi nampenda mume wangu, wala hayuko Moyoni mwangu!"

Yaani kwa hii kauli ilinibidi nikae kwenye kiti nikatafakari sana, kwa jinsi Binadamu tulivyo.

Tembea ujionee mengi, zungumza na watu usikie zaidi na zaidi.
 
Title ya uzi na uzi wenyewe ni vitu viwili tofauti kabisa.
 
= ili mradi
 
Mbona kawaida kwa mioyo ya binadamu Mungu pekee ndiye anayejua.

Nikuulize tu kwani kazi unayoifanya ndiyo uliyokuwa unaipenda tokea utotoni mwako. Maisha unayoyaoshi ndio chaguo lako, kula yako, vaa yako, ishi yako eneo, nchi,lala, nyumba, eneo, gari lako hivi vyote viko sahihi kulingana unavyotamani ama matamanio yako yanakidhiwa.
Mie nashangaa jamii imejikita katika mahusiano pekee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…