Ukweli wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar yakimuhusisha mtu asiye maarufu sana, John Okello

Leo katika mapumziko ya Mapinduzi Matukufu, sio vibaya kujikumbusha threads muhimu kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
P.
 
Taifa la Zanzibar limekulia na kudumaa katika uongo, ulaghai, ghiriba, vitisho Ifahamike na kueleweka kuwa bendera ya Taifa huru la Zanzibar ilipeperushwa tarehe 12 Disemba 1963.
Huu nao pia ni urongo!, Uhuru wa Zanzibar ni Desemba 10, 1963!. Ukiisha anza na factual error, you are very likely kujaza urongo mwingi humu, hivyo naomba kuwa mwangalifu sana na wewe usije kutulisha urongo!.

Huu pia ni urongo mwingine wa wazi wa mchana kweupe, Karume alijua kila kitu, ila ni kweli hakuwepo Zanzibar, sio kwa kuyakimbia Mapinduzi, bali kwa sababu hakukuwa na uhakika kama yatafanikiwa, Karume alisafiri kwa boti usiku ule akiwa na wanae, Amani na Ali kuja bara, mjane wake, Mdogo mtu amelithibitisha hili hapa
'Karume Hakuyakimbia Mapinduzi ya ZnZ'-Karume Jnr
Na mama mtu pia alithibitisha hapa
Mama Fatma Karume athibitisha Karume hakushiriki Mapinduzi ya Jan, 1964! TBC Live
Hivyo sii kweli kuwa Karume hakushiriki Mapinduzi, ndio mpangaji na mratibu na kuacha utekelezaji kwa wengine!.

Paskali
 

Tunaomba uthibitisho wa ushiriki wa karume ndani ya mapinduzi mkuu.
 
Akielezea mzee Mohamed said humu mnamwita muongo,mchonganishi,mdini na mshamba leo akiongea kamnda ndo mnaona ukweli
Na mseme who's behind 1961 independence na si nyerere tu
 
Historia ya Zanzibar imeandikwa na watu wengi,wengine wameandika historia ya ukweli wengine za uongo,wengine wameandika kwa sababu ya manufaa yao,wengine wameandika ili wapate kujulikana na mengi mengineo

Katika historia zote za mapinduzi ya Zanzibar ni kitabu cha "Kwaheri uhuru kwaheri ukoloni" ndio kitabu peke yake kilichozungumzia ukweli kuhusu mapinduzi ya Zanzibar

https://kwaheri.files.wordpress.com/2010/05/kwaheri-ukoloni-kwaheri-uhuru.pdf

Ukweli usiofichika wanzibari wengi wenye asili ya Mashariki ya kati na wahindi waliuliwa kinyama,yale yalikuwa sio mapinduzi yalikuwa mauaji ya kimbari (genocide).


Sababu hasa kilichowafanya wazanzibar wasiokuwa na asili ya Kiafrika kuuawa kichuki kama vile ni kuwa wale waliofanya yale mapinduzi walikuwa sio wazanzibar,walikuwa wageni,walikuwa watu ambao hawana hisia wala huruma na wazanzibari...

Zanzibar ni kisiwa,visiwa vyote duniani vina sifa moja,tabia ya wau kuchanganya(cosmopolitan),Tabu kumkuta mzanzibari halisi kuwa hachanganya damu na kabila au watu kutoka nchi nyengine...

Mndegereko kachanganya na muhindi,mwarabu kachanganya na mmanyema,mzigua kachanganya na mshirazi(wairani) nk......hiyo ndio sifa ya wazanzibari hiyo ndio sifa ya kisiwa chochoe duniani....

Hao wanaotawala sasa Zanzibar (CCM Zanzibar) ni mapandikizi ya watanganyika,mpaka mapandikizi yaishe ndio Zanzibar itaweza kujikwamua kutoka katika makucha ya wakoloni weusi

Hebu fikiri Miezi mitatu baada ya Mapinduzi,Zanzibar iliungana na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Zanzibar haijawahi kujitawala wazanizbari hawajafaidi matunda ya kuitawala wenyewe.......

 

Lakwanza ufahamu, Wakati hao waarabu unaowasema wanakuja hakukua na Tanganyika. NA Faham kua Big part ya Tanganyika ilikua ni Zanzibar.
 

CCM ndio wanaadhimisha mapinduzi ya Zanzibar.
Wananchi walio wengi hawana mpango nayo kabisa.
 
John Okello alikwenda Zanzibar kutokea Uganda kwa lengo la kujitafutia riziki kwa kufanya vibarua mbalimbali.
Wazanzibari ambao hawakuridhishwa na Uhuru uliotolewa na Waingereza kwa Chama Cha Sultan Jamshid, wakiwemo kina Seif Bakari, Abdallah Natepe na wenzao wengi wengine walipanga kufanya Mapinduzi.
Tatizo la Wanamapinduzi hao (kwa mujibu was maelezo ya Abdallah Natepe) walikuwa hawana jeshi la kuweza kupindua wala silaha za maana, wakati Sultani alikuwa na ghala la silaha.
Hivyo walipanga kuanza kuvamia ghala la silaha kwa kutumia silaha za kijadi, mapanga, mikuki, mishale, marungu n.k. Walipanga kumtisha Sultani na utawala wake kwa kuvamia kituo cha radio na kutangaza kuwa kuna majeshi ya kigeni yamevamia Zanzibar. Kukamilisha hilo waliazimia wapate mtu mwenye lafudhi ya kigeni. Wakampata John Okello, alikuwa na sauti yenye mamlaka na kafudhi ya kigeni, wakamtanguliza mbele, na kumpa jukumu la kutangaza Mapinduzi kwa kiswahili chake kibovu, watawala wakaamini kuwa wamevamiwa na majeshi ya kigeni, wakataharuki na kukimbia.
Baada ya Mapinduzi kufanikiwa, ilikuwa wamlipe ujira wake kwa kutekeleza vizuri jukumu walilompa kisha aende zake. Okello hakutaka hivyo, bali alijitangaza pia kuwa Mapinduzi yale ni yake na aliyapanga na kuyaongoza yeye, akataka na Serikali pia aipange yeye.
Ndipo alipopewa fedha za kutosha na kuamriwa kuondoka nchini, kwanza hakuwa raia wa Zanzibar wala Tanganyika.
Huo ndio ukweli kuhusu bwana huyo na Mapinduzi ya Zanzibar. Alichokiandika katika kitabu chake cha The Zanzibar Revolution, kuna baadhi ya maelezo yalikuwa ya kweli, lakini sehemu kubwa ya maelezo yake sio ya kweli, amejipamba sana ili aonewe huruma, ambayo hakuipata hata hivyo.
Laiti angetosheka na heshima aliyopewa ya kushiriki Mapinduzi na kutekeleza majukumu aliyopangiwa, angeandikwa vizuri kwenye Historia ya Mapinduzi hayo.
Ulaghai wake wa kutaka aonekane kuwa ni yeye peke yake ndie alikuwa steringi wa Mapinduzi hayo, ndio kumemponza. Alitaka kwenda Msumbiji kupigania Uhuru wakamkataa. Alienda Kenya na huko Kenyatta akamlundika gerezani, hatimae akatokomea kusikojulikana na kufia huko.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawatakia kumbukumbu njema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyovikomboa visiwa hivi.
P
 
John Okello alikuwa mwanaume wa Shoka.msema kweli mpenzi wa mungu.
 

Mkuu nisaidie kujibu haya maswali;
Katika hawa makamanda, Je kuna aliye hai mpaka sasa?
Je kuna watoto wao ambao wapo na bado wanaushawishi kwenye jamii mpaka sasa?
Je ni nini historia ya Okello baada ya kushuka Uganda mpaka leo.......?

Aksante kwa kutuelimisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…