Ukweli wa Tegeta Escrow!

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,423
Reaction score
3,297
Ndugu wanajukwaa, kwanza pongezi juu yenu wote kwa kukaribia kuuaga mwaka 2014.

Ndugu zangu nchi hii toka miaka ya 2000+ imepita katika kizazi cha Ulafi kisicho na huruma hata kidogo.
Tumeshuhudia Ufisadi wa kutisha usio na mfano wala kipimo kwa wale tuliowaamini na kuwapenda.

KWA NINI ESCROW?

Tumeaminishwa kuwa ni account iliyofunguliwa baada ya Mgogoro wa IPTL na Tanesco
Ili malipo yafanyikie hapo wakati mgogoro ukipatiwa uvumbuzi.

UKWELI WA TEGETA ESCROW

Hii account ilifunguliwa kwa kuwa IPTL si ya mtu mmoja ni kampuni yenye Wanahisa wengi ambao wengi ni VIONGOZI WAANDAMIZI SERIKALINI NA WENGINE NI VIONGOZI WALIOSTAAFU.

Kuna ambao HISA Zao walipitishia kwa Rugemarila akiwa kama Ngao yao na Wengine hasa Wale wenye HISA nyingi wakimtumia Seth kama Ngao yao pia.

Ndugu zangu Mafisadi hawa baada ya kuona kuwa Kugawana Faida za hisa zao italeta Mashaka ya kuwa kwa nini kila Vipindi fulani watu hao hupata fungu kutoka IPTL basi wakapendekeza ianzishwe Escrow ambayo kwayo Hakuna mtu yoyote angeweza kutoa fedha humo.

Kwa kuzingatia kuwa Wasingeweza kumwamini Singasinga na Rugemarila basi suluhisho ni kuzikusanya mahali ambapo ni salama.

Kumbukeni Muda wote huo wa miaka 7 kuzuia fedha za mwekezaji halali isingewezekana kabisa kwani ana mambo mengi ya uendesha yanayohitaji fedha.

Muda ulipowadia wa kugawana ndipo kila MWANAHISA ALIPOLIPWA SAWA NA HISA ALIZOPANDA NA IKUMBUKWE MWAKA 2015 NI WA UTAWALA MWINGINE NA HEKAHEKA NI NYINGI HIVYO KIBUBU KIKABIDI KIPASULIWE KILA MTU AJILIE VYAKE.

Hakuna cha Nani Wala nani IPTL ni ya Watz Kwa % 96.

Rais Mkapa Alisema--
Mtanikumbuka sana.

Na si kila king'aacho ni Dhahabu.

Jamani Akili Kumkichwa.

Waenagawana Share Walalahoi Wanajua ni Hongo ama Rushwa.

Ni maono tu.
 
Kikwete ndiye kinara wa wizi huu mkubwa uliolitikisa taifa na unaoendelea kwa kipindi hiki....

Watanzania tutaumizwa sana na Kikwete ambaye ni kinara wa magenge ya kifisadi hapa nchini...


Tumeambiwa Prof Tibaijuka pamoja na kuwajibishwa bado atakuwa na share kubwa na kulipwa malipo makubwa ili kumpunguzia machungu ya kuwajibishwa kwa jambo ambalo Kikwete ali-engineer mwenyewe
 
kwa mchezo ulikuwa haina shaka kuamin haya
 
Naam haya maneno. Waliopiga hii hela ni wengi engineer akiwa Raisi
 
Naam haya maneno. Waliopiga hii hela ni wengi engineer akiwa Raisi

Mkuu hao wanaitwa shareholders kwa lugha ya kibiashara ila kwa kiswahili cha madafu ni Washikadau.
 
Nini watanzania wafanye mkuu,chenge ameshastaafu u AG but bado anakula mafao ya IPTL na katiba katuandikia inayokidhi na kulinda masilahi yake na genge lake.same to Ngeleja and may be Jk baada ya muda wake.Tufanye nini ili kuondokana na huu ushenzi
 
kuna chembe chembe za ukweli tunaweza kuanzia hapo kuchimba zaidi
 
Raia Mwema: Turudi kwenye suala la Escrow. Hivi ile ripoti uliiona kabla haijatoka?

Ludovick Utouh: Ni kweli kwamba mimi ndiye niliyeanza na suala hilo lakini sikulimaliza kwa vile nilikuwa nimestaafu tayari. Sitaweza kuwa msemaji mzuri kuhusu ripoti hiyo.

Raia Mwema: Kuna kitu kimoja kwenye ile ripoti ambacho kimechanganya watu wengi ni pale CAG anaposema fedha zilizokuwepo katika akaunti ya Escrow zinaweza kuwa za umma au zisiwe za umma. Kwanini ripoti haikwenda moja kwa moja kusema zile ni fedha za umma au si za umma?

Ludovick Utouh: Hilo swali lake lingeweza kujibiwa vizuri zsaidi na aliyekuwa Kaimu CAG ambaye ndiye aliyesaini ile ripoti. Yeye ndiye anayejua zaidi. Lakini naomba kusema yafuatayo.

Kama ulifuatilia mjadala ule wa bungeni, kitu cha kwanza ambacho kilisemwa na kipo kweli ni suala la kodi. Ndani ya fedha zilizokuwapo kwenye akaunti ya Escrow kulikuwa na kodi. Kodi ni mali ya umma. Hivyo kwenye eneo hilo la kodi, fedha za umma zipo.

Jambo la pili lipo kwenye historia ya kuanzishwa kwa akaunti hiyo. IPTL na Tanesco walikuwa na mzozo kuhusu malipo ya capacity charge. Mgogoro ulikuwa mkubwa na wakaamua kuweka fedha za malipo hayo kwenye akaunti ya Escrow huku wakisubiri shauri lao kutoka katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro.

Sasa, nizungumze kama mfano tu, kwa kufikiria kwamba IPTL walikuwa wanaichaji Tanesco shilingi 30 kwa siku. Tanesco wakaona kwamba wanalaliwa kwa gharama hizo. Wanalipa zaidi ya wanavyotakiwa kulipa.

Wakaenda mahakamani kushitaki. Uamuzi uliotoka ni kwamba, ni kweli Tanesco wamebambikiwa hizo gharama. Inabidi gharama za capacity charge zikokotolewe upya. Sasa ofisi ya CAG haina mamlaka ya kufanya ukokotoaji huo.

Kwa hiyo, kama ukokotoaji ungefanyika, labda tuseme IPTL ingetakiwa kutoza shilingi 20 kwa siku, maana yake ile tofauti ya shilingi 30 inayotozwa na shilingi 20 inayotakiwa kutozwa, yaani shilingi 10, ingekuwa ya Tanesco.

Hii maana yake ni kwamba, katika kila shilingi 30 iliyokuwepo katika Escrow, ukiondoa zile za kodi, shilingi 20 zilikuwa za IPTL kwa sababu ya umeme wake iliyouza na shilingi kumi zilikuwa za Tanesco ambayo ni taasisi ya umma.

Ndiyo maana, nafikiri, Kaimu CAG katika ripoti yake akasema kwamba ndani ya akaunti ile kulikuwa na fedha za umma na pia kulikuwa na fedha zisizo za umma.

Raia Mwema: Kama leo wewe ungekuwa CAG na Mheshimiwa Rais akakuuliza achukue hatua gani kwa wahusika wa Escrow wewe ungemshauri nini?

Ludovick Utouh: Unajua jambo ambalo napenda watu wajue hapa ni kwamba ripoti ya CAG haichunguzi jinai. Sisi kazi yetu na kukagua mahesabu na kutoa maoni yetu kuhusu tulichokiona.

Ndiyo maana, mwaka 2010, tulifanya marekebisho kwenye Sheria ya Ukaguzi wa Umma kifungu cha 27 ambapo CAG aliruhusiwa kupeleka taarifa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa ajili ya uchunguzi wa jinai kama zipo kwenye ukaguzi uliofanyika.

Kama Rais angenitaka ushauri, ningemwambia Mheshimiwa Rais naomba utumie vyombo vyako. Atumie Takukuru, DCI na vyombo vyake vingine kuchunguza kujua nini hasa kilifanyika nyuma ya pazia. Hii si kazi ya CAG. No, Thank You.

Sasa akipata taarifa zote, ya CAG, Takukuru na DCI, hapo anaweza kuwa amejipa taarifa za kutosha kuhusu suala hili. Kama ataona kuna jinai yoyote, basi achukue hatua ya kuwasimamisha kazi wahusika na kuwapeleka mahakamani ili mkondo wa kisheria uchukue nafasi yake.

Raia Mwema: Kuna maneno yameenea kwamba maazimio ya Bunge kuhusu suala la Escrow yalikuwa yametawaliwa na mihemuko ya kisiasa zaidi kuhusu ukweli. Wewe una maoni gani kuhusu mawazo hayo?

Ludovick Utouh: Kwanza niseme kwamba ukiangalia tulikotoka miaka minane iliyopita na sasa kwenye eneo la usimamizi wa mapato na matumizi ya umma utaona kwamba tumepiga hatua kubwa. Bado hatujafika mwisho wa safari lakini tumesogea.

La pili niseme kwamba linapokuja suala la usimamizi wa mapato na matumizi ya mali na rasilimali za umma, mambo ya itikadi ya kisiasa yanatakiwa kuwekwa pembeni.

Maendeleo tuliyoyapata katika maeneo ya mapato na matumizi yanapaswa kuchagizwa kwa kuongeza zaidi wigo wa mapato ambayo yanaweza kukusanywa.

Naipongeza sana Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kazi kubwa ya kukusanya mapato ambayo wameifanya. Ukiangalia ni kiasi gani ukusanyaji wa mapato umeongezeka tangu enzi ya Rais Benjamin Mkapa hadi sasa utaona ni kiwango kikubwa sana.

Lakini bado watu wengi hawalipi kodi inayotakiwa. Hapa Dar es Salaam kuna watu wanauza maziwa au mayai na wanapata fedha ambazo ni mara tano ya mishahara wanayopata. Sasa wanakatwa kodi kwenye mishahara yao lakini hawakatwi kodi yoyote kwenye mapato haya ya nje. Ziko biashara nyingi sana ambazo hazilipiwi kodi na zingeweza kuongeza mapato ya serikali kwa kiasi kikubwa.

Ningetoa ushauri kwa TRA kuhakikisha kwamba wanatumia vema fursa hii ya kuwapo kwa vitambulisho vya Taifa vya NIDA ili kuweza kubaini watu walipo na kuwatoza kodi stahiki kwenye shughuli zao.

Kuna pia umuhimu mkubwa wa kuziba mianya iliyopo kwenye mfumo wetu wa utawala ili kuhakikisha Taifa linakingwa na matukio ya kifisadi kama yalivyokuwa kwenye EPA na hii Escrow. Ni lazima tufanye jitihada kuziba hiyo mianya ya ufisadi kwenye mfumo wetu.
 
Hii inadhihirisha Ikulu imehusika ktk uchotwaji fedha za escrow.
 
Tukifanikiwa kuchukua nchi lazima tuwanyonge viongozi kadhaa bila huruma kabisa, just a matter of time
 
Mashaka makubwa ni kuwa kwa nn hawa viongozi hata ile hela ya Kodi wameweka kwenye share zao?
 

Ok. Kwa hiyo nini kifanyike? Toa mapendekezo yako maana yale yaliotolewa na Bunge kwa Serikali ya Kikwete hayatekelezeki.
 
Ok. Kwa hiyo nini kifanyike? Toa mapendekezo yako maana yale yaliotolewa na Bunge kwa Serikali ya Kikwete hayatekelezeki.

Mapendekezo
Mosi ccm imnyang'anye Kadi ya uanachama Mwenyekiti wake kwa kuipeleka nchi kuzimu.

Pili
Wote wanaoutafuta Urais kwa udi na Uvumba kama alivyofanya Kikwete na Lowasa kuanzia mwaka 1995 tuwakatae kabisa ni ccm Maslahi.

Tatu

Bunge limtimue Rais

Nne.
Kama 1, 2, 3 ni ngumu basi tufanye kama Bukinafaso yaani tumtoe mtu pale Magogoni.

Haiwezekani Majina ya wauza Sembe ukae nayo Majina ya Majangili upambie chumba na ya Stanbic bank pia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…