Ukweli wa Tegeta Escrow!

Ukweli wa Tegeta Escrow!

Ndugu wanajukwaa, kwanza pongezi juu yenu wote kwa kukaribia kuuaga mwaka 2014.

Ndugu zangu nchi hii toka miaka ya 2000+ imepita katika kizazi cha Ulafi kisicho na huruma hata kidogo.
Tumeshuhudia Ufisadi wa kutisha usio na mfano wala kipimo kwa wale tuliowaamini na kuwapenda.

KWA NINI ESCROW?

Tumeaminishwa kuwa ni account iliyofunguliwa baada ya Mgogoro wa IPTL na Tanesco
Ili malipo yafanyikie hapo wakati mgogoro ukipatiwa uvumbuzi.

UKWELI WA TEGETA ESCROW

Hii account ilifunguliwa kwa kuwa IPTL si ya mtu mmoja ni kampuni yenye Wanahisa wengi ambao wengi ni VIONGOZI WAANDAMIZI SERIKALINI NA WENGINE NI VIONGOZI WALIOSTAAFU.
Kuna ambao HISA Zao walipitishia kwa Rugemarila akiwa kama Ngao yao na Wengine hasa Wale wenye HISA nyingi wakimtumia Sethi kama Ngao yao pia.
Ndugu zangu Mafisadi hawa baada ya kuona kuwa Kugawana Faida za hisa zao italeta Mashaka ya kuwa kwa nini kila Vipindi fulani watu hao hupata fungu kutoka IPTL basi wakapendekeza ianzishwe Escrow ambayo kwayo Hakuna mtu yoyote angeweza kutoa fedha humo.
Kwa kuzingatia kuwa Wasingeweza kumwamini Singasinga na Rugemarila basi suluhisho ni kuzikusanya mahali ambapo ni salama.

Kumbukeni Muda wote huo wa miaka 7 kuzuia fedha za mwekezaji halali isingewezekana kabisa kwani ana mambo mengi ya uendesha yanayohitaji fedha.

Muda ulipowadia wa kugawana ndipo kila MWANAHISA ALIPOLIPWA SAWA NA HISA ALIZOPANDA NA IKUMBUKWE MWAKA 2015 NI WA UTAWALA MWINGINE NA HEKAHEKA NI NYINGI HIVYO KIBUBU KIKABIDI KIPASULIWE KILA MTU AJILIE VYAKE.

Hakuna cha Nani Wala nani IPTL ni ya Watz Kwa % 96.

Rais Mkapa Alisema--
Mtanikumbuka sana.

Na si kila king'aacho ni Dhahabu.
Jamani Akili Kumkichwa.

Waenagawana Share Walalahoi Wanajua ni Hongo ama Rushwa.

Ni maono tu.

I see!....this makes alot of sense.
 
I see!....this makes alot of sense.

Mkuu wewe uwekeze hata kupikia shule halafu hela yako usilipwe miaka hata mi 4 tu huku ww unaendelea kununua mahitaji na kupika sijui kama ni rahisi khivyo.
Cha Ajabu kesi imeisha karibu na mwisho wa awamu ya 4!!!
Haihitaji akili kubwa kujua fumbo walilotufumba.
 
Mapendekezo
Mosi ccm imnyang'anye Kadi ya uanachama Mwenyekiti wake kwa kuipeleka nchi kuzimu.

Pili
Wote wanaoutafuta Urais kwa udi na Uvumba kama alivyofanya Kikwete na Lowasa kuanzia mwaka 1995 tuwakatae kabisa ni ccm Maslahi.

Tatu

Bunge limtimue Rais

Nne.
Kama 1, 2, 3 ni ngumu basi tufanye kama Bukinafaso yaani tumtoe mtu pale Magogoni.

Haiwezekani Majina ya wauza Sembe ukae nayo Majina ya Majangili upambie chumba na ya Stanbic bank pia?
Naunga Mkono mapendekezo yako ila naomba niongeze moja.Msajili wa vyama vya siasa aangalie uwezekano wa kukifuta chama cha mapinduzi kwani ndicho kichaka cha wahujumu uchumi wa Taifa letu
 
Hapo ndiko Prof. Muhongo anapopata ujasiri wa kusema "nikijiuzulu nchi itatikisika"!

Hii ndiyo TZ yaani mpaka muhongo anamficha JK mfukoni, sijawahi kuona

layoni=lion! !
 
Last edited by a moderator:
Ina maana chenge na mama tibaijuka walinunua hisa sawa? Maana wote walipewa kiasi sawa au siyo bana
 
Kumbe waligawana sawa?sasa mapovu ya nn?

Hahahaaa kweli tuna safari ndefu.
Kodi yetu vp?
Kumbuka wengine tutawalisha maisha yao yote.
Kama ni halali wafanye biashara kwa Uwazi kwa nn ubebe fedha kwa Sandarusi na Rumbesa?
Zimetimia kichwani kwako kweli?
 
Kuna jamaa Alishanitonya juu ya hili, that is explain whyChenge, Kimiti, Ngeleja, Daniel Yona wamepataje mgao, why mafanya biasharaagawe pesa kama njugu. Ukianzia na AlexStewart ilekampuni ya ukaguzi wa dhahabu, Atimus Gas ilekampuni iliyofilisikakule Mtwara, PAN AFRICAN ENERGT, Songas, simbion, na hata wanakuwa na masharekwenye migodi, Pesa za meremeta zilizokutwa kwenye account ya Chenge, Share zaStamico zilizopotea wakati Mgodi wa Bulyanhulu unauzwa kwa kutoka Suton kwendaBarrick na Buzwagi. Escrow imewaumbua hawa mafisadi.

Unajua ndugu lazma ujiulize viswali kuhusu wastaafu wanahongwa kwa lipi?
Kampuni ni ya Watanzania tena tuliowapa dhamana leo Wanatuangamiza mchana kweupe.
 
Kikwete ndiye kinara wa wizi huu mkubwa uliolitikisa taifa na unaoendelea kwa kipindi hiki....

Watanzania tutaumizwa sana na Kikwete ambaye ni kinara wa magenge ya kifisadi hapa nchini...

Tumeambiwa Prof Tibaijuka pamoja na kuwajibishwa bado atakuwa na share kubwa na kulipwa malipo makubwa ili kumpunguzia machungu ya kuwajibishwa kwa jambo ambalo Kikwete ali-engineer mwenyewe
 
Uko sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom