Ukweli wa uwepo wa Mungu na Makazi yake upo hapa

God is Dead!
 
Mungu ni Matokeo ya Ujinga wa Binadamu Kushindwa Kung'amua Mazingira Yake na Vyanzo Vyake!
Alipoona Radi,Ujinga Wake Ukamtuma Kutafsiri Kuwa Mizimu/Mungu Amekasirika!
Mvua Ilipokata Kunyesha Aliamini Mizimu/Mungu Amekasirika,and the Only Way To Appease is By Sacrificing to Him!
Sayansi Ilipokua Ilimwezesha Mtu Kuondoa Imani Katika Kutafsiri Maana ya Vyanzo na Matokeo ya Vyote Vilivyotokea ktk Mazingira Yake!Iwe Mwanga,Jua,Uzazi,Kifo et al!
Badala ya Imani,Mtu Akaweza KUJUA!
Na Kujua Huku Kukaua Wazo la Mungu!
God is A Wishful Thought in The Man's Brain!
And That Thought was Killed By Human's Schence!
 
Sema ngoja nikimbie sina jibu.
Siwezi kukimbia nilikuwa natoka job naelekea home,
Mungu yupo ni roho tukufu inayoishi milele Mungu muumba wa vyote hakuna chochote ambacho hakijaumbwa na Mungu yeye amekuwepo milele yote
 
Mwaka 2006 tukiwa katika kitongoji bunj'ru
km 47 inje ya jiji la Yaoundé Cameroon kuna mtafiti tulikutana nae anaetafiti vitu vya kale raia wa Greece alikuwa akifanya uchunguzi katika bwawa la maji linalotumika na kijiji hicho kwanini hairuhusiwi kuchota Maji na chombo cha chuma, shaba, aluminium akiambiwa akigusisha chombo ktk Maji atanyanganywa na asichokijua na akiludia mda mwingine naye ataondoka, alichota akanyanganywa chombo hakikuonekana tena hakurudia Mara ya pili aliogopa watu wengi walipotea ktk mazingira tatanishi kwa ujinga wao!
WEWE UNAAMINI SHETANI YUPO?
UNAAMINI UCHAWI UPO?
UNAWAJUA BAKTERIA WASIOONEKANA KWA MACHO?
 
Siwezi kukimbia nilikuwa natoka job naelekea home,
Mungu yupo ni roho tukufu inayoishi milele Mungu muumba wa vyote hakuna chochote ambacho hakijaumbwa na Mungu yeye amekuwepo milele yote
Hujathibitisha hilo, umesema tu. Thibitisha.

Kama Mungu yupo, ndiye muumba yote, ni mjuzi wa yote, muweza yote na ana upendo wote, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kuwepo wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kufanyika?
 
Hewa mgandamizo ya aina mbalimbali na vipande vipande vya aina mbalimbali mlipuko ulipelekea kuundwa kwa sayari na nyota na vyote vilivyopo kwa ujumla wake ktk ulimwengu
Nini ilikuwa sababu ya huo mlipuko
 
Wewe unajua unachokisema?
Ndio!Mungu ni Wazo Lililo Kichwani Mwako,Tena Wazo Hilo ni Tokeo la Wewe Kushindwa Kuyajua Mazingira Yako!Ujinga Huu Kwa Kushindwa Kuujua na Kuuondoa,Umeupa Jina la "Mungu"!
Ukitaka Kuona,ebu Ona
a)Wahindu kwa Ujinga Wao Ulipewa Jina la Mungu Ng'ombe!
b)Wayahudi Ujinga Wao Waliupa Jina la Yehova
c)Wafilisti Ujinga Wao Waliupa Jina la Dagoni!
Mungu ni Ujinga Wako!
 
Mkuu naona kama unatumia hisia zaid nakuacha akili nyuma katika kutafakar jambo ili.Umeuliza hapo kua inakuaje Mungu aumbe dunia yenye matatizo meng.Uku nikuingilia maamuz yake binafsi kama ilivyo kwako unavyoweza kuamua kununua gar badala yakujenga nyumba.Dhana yakusema uwepo wa Mungu wetu unajichanganya izo bado niakili zakibinadamu kuwaza tusiyokua na uwezo nayo.Tulipewa akil zituraisishie maisha aya tuliyopewa sio kutaka kuwaza zaidi yajinsi aliyetuumba alituumba.kwaiyo lazima ujue uwezo wetu wakufikir una limit ndo maana kamwe huwez pata majibu ya uwepo wa Mungu kama unavyotaka.Kama ambavyo huwez jua mwenzako anawaza nin ndivyo jins ambavyo hatuwez kujua Mungu aliwaza nin kuumba ivyo ndo maana kukawa na dhana ya wenye busara ya KUAMINI.
 
Tatanishi?
Kwahiyo Ujinga wa Mgiriki Huyo Kushindwa Kujua Nini Chanzo cha Kuvutwa kwa Vifaa na Pia Imani ya Wanavijiji Pamoja na Wewe Kuwa Ujinga Wenu wa Kutokujua Ni Nini Kinachoendelea Kwenye Icho Kisima Tayari Mkaubatiza Jina la "Mungu"?
Mungu ni Ujinga Wako!
 
Kwani hayo unayoshangaa kutokea si sehemu ya kazi yake au unakosa maswali mengine zaidi ya hili la kwanini kaumba ulimwengu wenye mabaya?

Inaposemwa muumba wa yote hapa inagusa mazuri na mabaya na kayaweka kwa kusudio muaalum na yapo yote ili yawapate binadamu.

Jaribu kufuatilia kwanini kawaleta binadamu duniani na si sehemu nyingine?
 
Utasemaje naingilia maamuzi binafsi ya Mungu wakati hujathibitisha kama yupo?

Hivi unaelewa "logical consistency" ni nini?

Unaelewa kwamba mtu akikwambia pembetatu ni tofauti na duara, na duara haiwezi kuwa pembetatu katika Euclidean geometry, halafu akakwambia ametengeneza pembetatu ambayo ni duara, ukimuuliza ametengenezaje wakati alisema pembetatu haiwezi kuwa duara hujamuingilia maamuzi yake binafsi ila umehoji logical consistency yake?

Unafahamu logical consistency ni nini?

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Mbona hujajibu swali hili?

Unajua kwamba ukisema naingilia maamuzi yake binafsi unachosema ni kwamba hujui jibu la swali hili?

Unajua kwamba hujui jibu la swali hili kwa sababu hakuna jibu lililo logically consistent?

Unajua kwamba hakuna jibu hilo kwa sababu Mungu huyo hayupo?
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Hujajibu swali langu.

Unaniambiaje mimi ambaye nimekuuliza swali wewe - hilo tu ni kufuatilia- nijaribu kufuatilia?

Wewe ambaye umeshindwa kujibu swali langu ndiye umeshindwa kufuatilia.

Kama Mungu yupo, ndiye muumba yote, ni mjuzi wa yote, muweza yote na ana upendo wote, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kuwepo wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kufanyika?

Unaweza kujibu swali hili badala ya kulipiga danadana tu na kuniambia nijaribu kufuatilia?
 
Hivi kabla ya Mungu kuumba kulikuwa na nini?
St Augustine aliulizwa swali kama hili.

Aliulizwa kabla mungu kuumba dunia alikuwa anafanya nini?

Akashindwa kujibu.

Akasema Munguvalikuwa anaumba moto wa kuwachomea watakaouliza swali hili.

Hakuna anayejua jibu.

Kwa sababu Mungu huyu hayupo.
 
St Augustine aliulizwa swali kama hili.

Aliulizwa kabla mungu kuumba dunia alikuwa anafanya nini?

Akashindwa kujibu.

Akasema Munguvalikuwa anaumba moto wa kuwachomea watakaouliza swali hili.

Hakuna anayejua jibu.

Kwa sababu Mungu huyu hayupo.
hahaaa, na ukimuuliza creationist ni kitu gani kinaweza kubadili mawazo yake juu ya uwepo wa Mungu atakujibu "HAKUNA"! Inahitaji moyo wa barafu kudebate na hawa watu!
 
hahaaa, na ukimuuliza creationist ni kitu gani kinaweza kubadili mawazo yake juu ya uwepo wa Mungu atakujibu "HAKUNA"! Inahitaji moyo wa barafu kudebate na hawa watu!
Ni ujinga ambao kadiri siku zinavyoenda utapita tu.

Inaweza kuchukua mamia ya miaka, lakini kama watu tutaendelea kuwepo , kila mwaka unaopita ndio hii habari ya Mungu inavyozidi kuoneshwa kuwa ni uongo tu.
 
Kuna mtu kaweza kuthibitisha kwamba Mungu yupo?
 
Sababu za Mungu kuumba ulimwengu na yote yaliyomo mema na mabaya anazijua mwenyewe ni sawa na kukuta mhunzi aliweka alama ktk finyanzi yake huwezi fahamu kusudio lake
 
St Augustine aliulizwa swali kama hili.

Aliulizwa kabla mungu kuumba dunia alikuwa anafanya nini?

Akashindwa kujibu.

Akasema Munguvalikuwa anaumba moto wa kuwachomea watakaouliza swali hili.

Hakuna anayejua jibu.

Kwa sababu Mungu huyu hayupo.
Kuwepo kwa Mungu kunathibitishwa na uhai lakini wewe huna fact ya kuthibitisha kutokuwepo Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…