Nimekutana na hii video jamaa akielezea kuwa ulaji wa maembe na maganda yake ni tiba ya asili ya Bawasiri. Msimu wa maembe ndio huu, kabla sijaenda nunua lumbesa ya maembe naomba kupata uhalisia wa taarifa, upotoshaji wa makusudi wa masuala ya Afya umeshamiri sana.
- Tunachokijua
- Embe kitaalamu hujulikana kama (Mangifera indica) ni tunda lenye utajiri wa Vitamin A, C na D na ni miongoni mwa matunda ambayo yanapatikana kwa urahisi katika maeneo mbalimbali.
Bawasiri ni uvimbe wa mishipa ya damu inayopatokana kwenye sehemu ya chini ya utumbo mpana pamoja na sehemu ya haja kubwa. Uvimbe huu mara nyingi husababisha maumivu makali na kuvuja kwa damu. Bawasiri inaweza kubakia ndani, au ikachomoza nje kwenye sehemu ya haja kubwa. Hali hii husababisha ugumu katika kujisaidia kutokana na aina ya maumivu ambayo hutengenezwa wakati huo.
Tovuti ya Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC wanaeleza kuwa mitindo ya maisha na mitindo ya chakula inaweza kuwa sababu ya mtu kupata ugonjwa wa Bawasiri, ulaji wa vyakula vya haraka (junks Food) kama kama pizza na aina nyingine, wapo kwenye hatari kubwa ya kupata bawasiri.
Kumekuwepo na taarifa zinazodai kuwa ulaji wa maembe husaidia kuzuia bawasiri na baadhi ya watu wamekuwa wakitumia katika kufanikisha jambo hili.
Uhalisia wa madai haya
JamiiCheck imepitia tafiti na makala za afya mbalimbali ambazo zimeonesha kuwa kuna baadhi ya matunda ikiwemo embe yana chembechembe ambazo zinaweza kuzuia Bawasiri. Tafiti zinabainisha kuwa maembe yana chembechembe zijulikanazo kama Mangiferin ambazo husaidia kupunguza uvimbe tumboni na kuimarisha mfumo wa kinga.
Chapisho lilichopashwa na Mayoclinic wanabainisha kuwa miongoni mwa njia ambazo zinaweza kutumika nyumbani kwa ajili ya kujilinda na kupunguza uvimbe wa bawasiri ni kwa kutumia vyakula vyenye kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi (high-fiber foods).
Tovuti ya Ds research center imebainisha pia kuwa kwa miongo mingi sasa maembe yametumika kutuliza tumbo kwa kuwa yana vimeng'enya vyenye uwezo wa kufanya hivyo. Embe lina nyuzinyuzi nyingi, kwa hivyo ikiwa unakula angalau embe moja kila siku, inaweza kupunguza changamoto ya kupata changamoto ya kupata haja kubwa, bawasiri, na dalili za ugonjwa wa tumbo.
Afyainfo wanaeleza kuwa kunywa maji ya kutosha kila siku, kuongeza ulaji wa matunda na mboga za majani pia kujihusisha na mazoezi mepesi ambavyo kwa ujumla huupunguzia mwili nafasi ya kupatwa na changamoto ya choo kigumu inaweza kutumika kama kinga ya Bawasiri.