Ulaji wa mafuta upo wapi kwenye gari?

hapa hatupo kwaajili ya kubishana bali tupo kwa ajili ya kufundishana na kujuzana.

hivi gari kuwa na nguvu kubwa mfano kuwa na speed kubwa kunahusiana na cc??

Si ndio hapo mkuu, watu wanazungumza mengi wanacho sahau ni uhusiano wa horse power na engine displacement - specs hizo zinarandana sana na ulaji wa mafuta kwa engine ambazo ni natural aspiring lakini linapokuja suala la turbocharged engines compressed hewa inaingia kwa silinda ya engine kwa wingi hivyo fuel injectors zina tema mafuta kwa wingi ku maintain ratio ya 1:1 i.e fuel to air ratio ku support a complete combustion, sasa ulazimishaji wa hewa nyingi na mafuta mengine ufanya engine ya 2000 C.C ifikie power ya injini ya 4000 C.C huo ni ujanja wa ma designer wa internal cumbustion engines - engine ndogo power kubwa na ulaji mafuta mkubwa.

Mimi sioni logic ya kutaka kubadirisha ECM na sensors za gari ya 4000cc say na kuweka module ya 1800cc kisa? Kupunguza ulaji wa mafuta!!! Kitu cha kwanza engine performance itakuwa highly degraded kutokana na cylinder kujazwa mchanganyiko wa hewa na mafuta ambayo specs zake zili kuwa designed for an 1800cc engines na sio 4000cc torque itakayo kuwa generate na pistons kwenye crankshaft baada ya combustion itakuwa ni ndogo sana.
 
Habari wakuu,

Wataalamu wa magari naomba kujuzwa matumizi ya mafuta kwenye gari, gari inaongeza kiwango cha ulaji wa mafuta ikiwa katika mwendo wa speed ngapi gari za Automatic? Na mwendo mzuri wa economy ukiwa safari ni speed ngapi?
 
Ooh ahsante, sasa nikuulize lingine, unakuta mtu anakwambia hii gari inatumia mafuta lita 1 kl 10 mfano, huwa anachukulia wastani wa speed ngapi? Yaani ni katika over 110 au ni hiyo ya kati ya economy?
 
Magari yanatumia mafuta sana ukiendesha spidi ndogo chini ya 50km/h au yakienda spidi kubwa sana zaidi ya 120km/h. Optimal speed kwa magari ya petroli yanye injini sizozidi lita 3.6 ni 80km/h ambapo ndipo mafuta yanajichanganya sawasawa na oxygen na kuungua kikamilifu bila hata kutoa masizi yoyote. Iwapo unategemea kuwa unaendesha spidi za juu tu, yaani zaidi ya 110km/h muda mwingi, kuna ufundi wa kuprogram upya Engine Control Unit ya gari kusudi iruhusu injini kuvuta hewa nyingi muda wote, lakini utakuwa unatumia mafuta sana unapokuwa spidi za chini; vile vile kuendesha kwa muda mrefu katika spidi za chini kunaweza kusababisha injini kunoki. Watengeneza magari wengi wanaficha Engine control unit zao kusudi watu wasibadilishe program, lakini wajanja wanajua jinsi ya kupenyeza.
 
ni kweli mkuu hiyo kitu inaitwa mapping kama inavyofanyika kwenye magari ya mashindano sema balaa jingine ni kwenye speed ndogo itakutesa sana mda wote yatakiwa uwe mbio mbio tuu
 
sasa kama unaenda mbeya si utakeshaaa na hio speed kisa ubanie mafuta. Sometimes naonaga hakuna sababu ya kumiliki gari kama utaliendesha kwa masharti, hivi vitu tuwaachiege wazungu tu!
Wengine wanafungua madirisha wapigwe na vumbi, dah!!!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] sawa sawa mkuu hapo umenea.
 
Mkuu hukiishia juu juu tu kuhusu engine control unit utakuwa hujauetendea haki huu uzi...

Funguka ili tupate kujua zaidi...
 
mwendo mzur ni kujua wap injin yako ina tengeneza max torque yake mfano mdogo nikupe kweny piki pik aina ya boxer max torque ni 12.26nm @ 5500rpm hvy tafuta spid itakayo kuwepo kwa gia ya mwisho as boxer ina gia 4 piga ratio ya gia zake utapata spid 66kph hvo ukiwa spid hyo kwa boxa ndo inakuwa inakula mafuta kidogo kuliko spid yeyote ile...........hvo kwa mweny gar cha kufanya ni kujua wap injin yake inaproduce max torque
 
We
Unajua mengi aisee ila ungefanya tukajua hiyo max torgue inatafutwaje. Mfano mi natumia lexus gs300. Inasoma 260km/h max. Sasa nitaijuaje? Au narud kugoogle specifications!
 
sasa kama unaenda mbeya si utakeshaaa na hio speed kisa ubanie mafuta. Sometimes naonaga hakuna sababu ya kumiliki gari kama utaliendesha kwa masharti, hivi vitu tuwaachiege wazungu tu!
Wengine wanafungua madirisha wapigwe na vumbi, dah!!!

Speed ya 110 sio ndogo hata kidogo hata kama unakwenda wapi.
 
Ili usitumie mafuta zaidi ya kiwango;
1. Cheki upepo wa matairi yako usiwe kidogo.
2. Usikanyage accelerator kwa nguvu sana.
3. Mwendo uanzie 40kph to 110kph
Mengine wadau wataingezea......
 
kasampaida mm nijuavyo ulaji wa mafuta unategemea vitu vingi hasa kwenye hizi barabara zetu
maana hujasema km ni Diesel au Petrol
ni barabara ya vumbi au lami
gia zitakazotumika katika vumbi nitofauti kabisa na kwenye lami (na hasa kwa Auto)
haya mambo ya Torque (zunguko wa crankshaft kuwa na ratui ya 1:1 (kwa gear no4) au uruke overdrive tuyaache kwanza kwa hizi barabara zetu.hakikisha upepo mbele 30 na nyuma 35ps pump (fuel pemp ni nzima, service ya engine fanya km mileage imekaribia, halafu uwena Corolla 110 Petrol na LandCruiser VX G8Diesel tuseme ni gari za mwaka 2000 matumizi yake yatapishana
Mfano unatumia gari ndogo
ya chini ya cc1500 eg Corolla yenye 1490cc Dodoma to Dar 450km Corolla hutumia lita 25 unaingia Dar kwa bei ya 50,000/ ukigawa kwa bei ya 1,950/ ni sawa na lita moja km 18
sasa hapo kuna Bumps, kuna vibao vya 50 kwenye makazi ya watu ni lazuma ushuke mpaka gia no 3 au 2 na speed unapiga mpaka 150km/h​
Ukija Diesel Dom mpaka Dar ni zaidi ya Lita 70 zitateketea, na hizi gari zinafumuka kula mafuta na mwendi ukishavuka speedometer110 na ni njia hiyo hiyo ya bumps na limit speed
sasa ndio njoo na swali lako ni gari gani ya petrol au diesel ni Lorry au IST inayotimia vvti
 
Speed ya 110 sio ndogo hata kidogo hata kama unakwenda wapi.
Loh sasa chukulia una Land Cruiser Vx V8 yenye max 260km/hr on dash unautafuta mkoa. Utaendeshea 110km/hr safari nzima ikiwa ni mkandamizo wa ndani ya sekunde 8 tu? Je, 110km/hr hapo utasema ni speed kubwa bado.
 
sasa kama unaenda mbeya si utakeshaaa na hio speed kisa ubanie mafuta. Sometimes naonaga hakuna sababu ya kumiliki gari kama utaliendesha kwa masharti, hivi vitu tuwaachiege wazungu tu!
Wengine wanafungua madirisha wapigwe na vumbi, dah!!!
Si kila ukienda Mbeya ni safari ndefu, inategemea unatokea wapi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…