Ulaji wa Mafuta wa Subari impreza ninayomiliki

Jemsi

Senior Member
Joined
Mar 22, 2012
Posts
149
Reaction score
19
Habari wakuu, samahani naomba msaada nina subaru impreza ya 2008 cc1490, 70,000km. Kwenye dashboard inaonyesha ulaji wa mafuta ni 8.6km/l na pia nikicalculate manually range inaangukia kwenye 8 kwa safari za mjini na highway, lakini wadau wenye haya magari wanasema ni 10km/l kwa mjini na 14-15km/l highway, wajuzi naomba kujua tatizo lipo wapi
 
Uendeshaji wako ndo shida kama kwel gari ako iko proper kila kitu
 
Kwa gari ya cc1490 inabidi upate zaidi ya 10km/l iwe mjini au highway.
 
Mi my next car ni rumion kwa sasa naendesha passo tena ni ya pili baada ya ya mwanzo iufikisha 160000km nikaiuza, nikanunua mpya ina 34000km na sasa ina 67000 km napiga nayo safari nyingi tu toka kanda ya ziwa hadi dar
 
Hata mimi nina Passo ina km 66500... lakini rumion achana nalo halina muonekano mzuri.... nunua angalau runx au allex zipo powa sana... ilaa kwa mimi natamani baadae ninunue toyota Belta nimeipenda sana
 
Swali la langu ni je unaweka engine oil recommended by manufacture? utakapokosea aina ya oil kwenye engine itakupelekea kwenye ulaji mkubwa wa mafuta mfano unatakiwa uweke 5W30 wewe unaweka 20W50 hiyo gari lazima itumie mafuta mengi, kingine je unafanya service kwa wakati? kama hufanyi hivyo anza kufanya sasa utaona mabadiliko makubwa
 
Hata mimi nina Passo ina km 66500... lakini rumion achana nalo halina muonekano mzuri.... nunua angalau runx au allex zipo powa sana... ilaa kwa mimi natamani baadae ninunue toyota Belta nimeipenda sana
Mkuu mm huwa naangalia engine, spares mwonekano kwangu unakuja mwisho kabisa. Honda crossroad kwangu naipenda sababu ya mwonekano ila nimeambiwa ikiloga spea hadi uagize nje
 
Tatizo lipo kwenye gari lenyewe ni Subaru!
 
kwa cc hzo ilitakiwa ile 13-16 km kwa lita kama ni Impreza XV,kama haili hivyo kuna shida mahali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…