SI KWELI Ulaji wa mayai wakati wa ujauzito husababisha kujifungua watoto wenye vichwa vikubwa au wasio na nywele

SI KWELI Ulaji wa mayai wakati wa ujauzito husababisha kujifungua watoto wenye vichwa vikubwa au wasio na nywele

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wanawake wajawazito hupewa tahadhari au hata hukatazwa kabisa kufanya baadhi ya mambo kwa lengo la kuwaepushia madhara yanayoweza kuhatarisha afya zao, pamoja na mtoto aliyeko tumboni.

9F0C925D-D2A2-4A5A-BE59-BEFC5DC32438.jpeg

Miongoni mwa mambo yaliyodumu kwa muda mrefu kwenye jamii zetu ni kuzuia wanawake wajawazito kutumia mayai ili kuwalinda watoto wasizaliwe wakiwa na vichwa vikubwa, au wakiwa hawana nywele.

Kisayansi, jambo hili lina ukweli kiasi gani?
 
Tunachokijua
Ujauzito huongeza uhitaji wa virutubisho kwa mama ili aweze kuutunza vizuri pasipo kuathiri ukuaji wa mtoto.

Nyongeza ya ziada ya virutubisho vyenye wingi wa nishati, protini, asidi ya foliki, omega 3, vitamini D pamoja na madini chuma, calcium, zinc hufaa sana wakati huu. Kumekuwapo na madai kuwa ulaji wa mayai kwa mwanamke mjamzito husababisha kuzaliwa kwa mtoto asiye na nywele.


Je ni upi uhalisia wa madai hayo?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa ulaji wa mayai wakati wa ujauzito hausababishi athari kwa mtoto hasa kuzaliwa bila nywele kama inavyoaminika na baadhi ya watu.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Mayai ya Australia, mayai ni chakula kizuri kinachofaa kwa afya ya mama mjamzito. Huwa na mjumuiko wa madini na vitamini 13 tofauti, mafuta mazuri ya omega 3, viondoa sumu pamoja na protini muhimu kwa ukuaji bora wa mtoto. Mayai yana protini kwa kiwango kikubwa na virutubisho muhimu, pia ni muhimu katika usaidia kukidhi mahitaji ya lishe na ukuaji mzuri wa mtoto wakati wa ujauzito.

Huwa pia na choline kirutubisho kinachotumiwa na mwili kwenye kutengeneza mfumo bora wa fahamu ukihusisha ubongo na uti wa mgongo. Kirutubisho hiki pamoja na asidi ya foliki husaidia pia kuzuia tatizo la mtoto kuzaliwa akiwa na mgongo wazi au kichwa kikubwa.

Faida nyingine ni uwepo wa vitamini A yenye faida kubwa katika kuboresha afya ya macho, ngozi pamoja na kuimarisha kinga ya mwili.

Mtoto kuzaliwa bila nywele kitaalamu hujulikana kama Congenital atrichia ambayo hurithiwa ambayo ni kutokuwepo kwa nywele kwenye mwili mzima wakati wa kuzaliwa, pia inaweza kuwa ya pekee au kuambatana na kasoro nyingine za mwili.

Tahadhari
Mayai mabichi pamoja na yale yasiyopikwa vizuri hubeba kiasi kikubwa cha bakteria jamii ya Salmonella ambao husababisha sumu ya chakula. Kwa mama mjamzito, wanaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo kuharibika kwa ujauzito. Hivyo, haishauriwi kutumia mayai mabichi.

Pia, kwa wanawake wenye kisukari cha ujauzito pamoja na kiasi kikubwa cha mafuta kwenye mishipa ya damu, wanashauriwa kutumia kiasi cha mayai yasiyozidi 7 kwa wiki ili kutokufanya matatizo haya yawe makubwa zaidi.

Kwa ujumla, mayai ni chakula salama kinachoweza kutumiwa na mama mjamzito wakati wote wa ujauzito ikiwa tu yatakuwa yameandaliwa katika hali ya usafi na kupikwa vizuri.​
Ulaji wa mayai ni muhimu sana kwa mama mjamzito kwani anahitaji virutubisho kwa ajili ya mtoto aliyeko tumboni, na hili la mtoto kuzaliwa bila nywele au kichwa kikubwa ni Imani potovu tu walizokua nazo wazee wa zamani.
 
Tetesi zilikua taboo za zamani. Wazee wa kiume walitaka vinono vyoote viwe vyao
 
Ulaji wa mayai ni muhimu sana kwa mama mjamzito kwani anahitaji virutubisho kwa ajili ya mtoto aliyeko tumboni, na hili la mtoto kuzaliwa bila nywele au kichwa kikubwa ni Imani potovu tu walizokua nazo wazee wa zamani.
Umenena vyema
 
Back
Top Bottom