Twin Tower
JF-Expert Member
- Jan 13, 2023
- 2,170
- 3,067
Naona taratibu wameanza kurudisha utawala wao. Kwa sasa wana timu 5 zinazo cheza hatua za nusu fainali.
Pale champions league kuna Ac Milan na Inter Milan. Hawa wanaenda kukipiga nusu fainali wao kwa wao. Napoli wametolewa na waitaliano wenzao, pengine nao wangekuwepo kama wangekipiga na timu ya nchi nyingine.
Europa pale unawakuta Juventus na Roma ambao pia wanaenda nusu fainali.
Ukimalizia conference league unamkuta Fiorentina nae anaenda kukiwasha nusu fainali.
Kaa tayari kushuhudia vikombe vyote vikienda Italia.
Ilikuwa ni bahati mbaya tu kwa timu yao taifa kushindwa kufudhu fainali za kombe la dunia kule Qatar.
Ila kiwango chao kwa sasa hakikamatiki.