Ulaya kwa sasa Serie A ndo ligi bora 2022/2023

Twin Tower

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2023
Posts
2,170
Reaction score
3,067
Naona taratibu wameanza kurudisha utawala wao. Kwa sasa wana timu 5 zinazo cheza hatua za nusu fainali.

Pale champions league kuna Ac Milan na Inter Milan. Hawa wanaenda kukipiga nusu fainali wao kwa wao. Napoli wametolewa na waitaliano wenzao, pengine nao wangekuwepo kama wangekipiga na timu ya nchi nyingine.

Europa pale unawakuta Juventus na Roma ambao pia wanaenda nusu fainali.

Ukimalizia conference league unamkuta Fiorentina nae anaenda kukiwasha nusu fainali.

Kaa tayari kushuhudia vikombe vyote vikienda Italia.

Ilikuwa ni bahati mbaya tu kwa timu yao taifa kushindwa kufudhu fainali za kombe la dunia kule Qatar.
Ila kiwango chao kwa sasa hakikamatiki.
 
Labda mmuue Madrid,ucl inaenda Spain
 
UCL ni man cty
 
Kwenye Europa league kuna Sevilla wenye kombe lao hao hivyo Roma na Juve wajipange haswa kuchukua kombe kwa Sevilla ni shughuli pevu.
Kwenye champions league nako kuna Real madrid wenye kombe lao. Inter/ Ac Milan wakomae haswa sio rahisi hiyo fainali hata kama watakutana na Man city
 
VYOVYOTE VILE ITAKAVOKUA BINGWA WA UEFA CHAMPION LEAGUE NI MANCHESTER CITY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…