Ulevi ndiyo chanzo kikuu cha ndoa nyingi kuvunjika

Pengine limekutokea wewe ukajua ndio sababu kubwa. Kama huna takwimu basi haupo sahihi
 
Mwanamke hunyenyekea ndoa Hadi malengo yake yanapotimia baada ya hapo Huwa mbinafsi anaetaka kuishi nawatoto pekee bila mume!!

Ukitaka kudumu bae chelewesha malengo yake walau mtaishi miaka mingi!!

Swala la ulevi sio sababu kuu!!
 
Mkuu kwanza umeoa au unaongea tu?
Kwani zamani hakukuwa na pombe mbona ndoa zilikuwa zinadumu?

Au mbona kuna mamilioni ya watu wasio kunywa pombe na bado ndoa zao ni pasua kichwa na kuna mamilioni ya wanywa pombe na ndoa zao zimedumu?

Changamoto kubwa ndani ya ndoa za sasa ni uzinzi miongoni mwa wanandoa acheni kumungunya maneno ,yaani siku hizi jamii yetu imeendeka uzinzi na kuufanya kana kwamba ni kitu cha muhimu kwenye maisha ya kila siku si kwa wanaume wala wanawake, si kwa wanandoa na wala si kwa ambao hawajaingia kwenye ndoa.

Kwa sasa %99.9 ya ndoa za sasa ni kati ya wazinzi wawili walio amuwa kuishi pamoja, yaani uoe mwanamke ambaye ameshalala na wanaume kumi na ushenzi utegemee atatulia kwenye ndoa, au uolewe na mwanaume ambaye amesha tembea na wanawake 50 alafu utegemee atulie kwenye ndoa.?
 
Kwani Diamond PlatinumZ ni mlevi?
 
Bado
Bado
Bado
Nasema bado
Bado haujafanya utafiti, umesimuliwa, umeota au unasaikia.

Fanya utafiti au oa asiyekuwa mlevi.
 
Kwani tajiri namba moja duniani mzee wa DOGE ya Trump, Elon Musk na msaidizi wake kwa utajiri Jeff Bezos ni walevi?

Nasema bado, rudia utafiti wako.
 
Inategemea ni ulevi wa kitu gani, kama ni ulevi wa ngono sawa, ila siyo wa pombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…