Ulevi ni msingi wa maendeleo?

Ulevi ni msingi wa maendeleo?

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Nimewaza sana kuhusu umuhimu wa ulevi wa pombe na sigara kwa walevi nikagundua kwamba ulevi huu hauna umuhimu wowote kwa wahusika, uwe wa kiafya au kiuchumi. Madhara ya pombe na sigara kwa mtumiaji yanajulikana kwa kila mtu mwenye akili timamu.

Pombe humfanya mnywaji ashindwe kufanya maamuzi sahihi na kumdhuru kiafya. Ina madhara kwa ini na viungo vingine muhimu. Hii ni sehemu tu ya madhara yatokanayo na unywaji pombe.
Sigara husababisha kansa ya mdomo, koo au mapafu.

Kila siku tunasikia serikali ikiwaita wawekezaji kujenga viwanda vya pombe kila mkoa katika nchi hii. Na uwekezaji kwenye pombe unalipa sana kwa sababu ya uwepo wa soko la uhakika (walevi) nchini.

Siku ya maadhimisho ya uvutaji sigara, utawaona serikali wanawaasa raia waache kuvuta sigara. Siku inayofuata utasikia wanapeleka tani kadhaa za mbolea kwa wakulima wa tumbaku huko Ruvuma na Tabora.

Ni kweli kwamba pombe na sigara huuingizia serikali fedha nyingi za kigeni. Lakini je, tutaendelea kudhuru afya za watanzania mpaka lini?
Tafakari!
 
unamzungumziaje doctor ambaye hawezi kufanya operation bila kunywa pombe je aache pombe?!
 
unamzungumziaje doctor ambaye hawezi kufanya operation bila kunywa pombe je aache pombe?!

kwani pombe ni stimulant ya madaktari wanaofanya operation? bila pombe operation hazifanyiki?

mimi concern yangu ni wale watu wanaodhuriwa afya zao kwa pombe na sigara kwa kigezo kwamba makampuni ya pombe na sigara huchangia uchumi wa nchi. hakuna theory yoyote ya ujenzi wa uchumi inayo-support uharibifu wa afya za wananchi kwa kisingizio cha kuongeza mapato ya serikali.
 
Back
Top Bottom