Ulevi ulitaka kuniponza

The topnotch

Member
Joined
Nov 14, 2018
Posts
6
Reaction score
4
Sehemu ya kwanza
Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2019, kipindi hicho niko chuo mkoa wa Mbeya katika harakati zangu za hapa na pale. Mimi nilikuwa ni mtu wa kwenda sana klabu kupata mbili tatu za hapa na pale, sasa siku moja nikaenda klabu moja maarufu sasa jijini Mbeya

Katika hapa na pale, si unaelewa tena ukishapiga vitu lazma akili ikutume uwe na mtoto mkali wa kwenda kupumika naye na mambo mengine yaendelee pakuche, sasa nikiwa hapo napiga vitu mishale kama ya saa nane hivi klub imebamba balaa akapita mrembo fulani hivi, ameshona balaa [emoji41] daah!

Nikasema na hili baridi simuachi, basi nikahama meza...............
 
 

Attachments

  • cup-of-tea-teapot.gif
    157.7 KB · Views: 11
Hebu tupe mbinu(mbuni) sisi wanachuo ambao pamoja na kutokwenda club ili kusave pesa bado tunashindia mihogo na hatuna kitu

We really need your 2019 tactics mkuu🙏🙏
 
Kuchoshana tu hakuna jipya chini ya jua we ungehadithiwa walevi walivyoruka na mashoga club asubuhi anaamka kashatunukiwa na jicho si ungedata
 
Hebu tupe mbinu(mbuni) sisi wanachuo ambao pamoja na kutokwenda club ili kusave pesa bado tunashindia mihogo na hatuna kitu

We really need your 2019 tactics mkuu[emoji120][emoji120]
Masikini watoto wa wakulima mnawaiga watoto wa vibopa kuishi ?

Ishi maisha yako achana na mambo ya eti lazima niwe na code kali

Achana na simu za gharama ukiwa na PC basi kiswaswadu ndiyo habari ya mjini.

Oya wewe bado huna hela hizo laki tano na kumi zisikutoe akili kwa hiyo miezi miwili unayoipokea achana na habari za kupanga chumba eti unajipanga na maisha .Maisha gani hayo ? Wakati mkimaliza vitu mnauza ili mpate nauli kurudi vijijini kwenu?

Pambana upate hosteli ili uwe na uhakika wa kulala kwani wamama wauza vyakula vya buku huwajui ? Kale huko achana na habari za chipsi yai maana hata kwenu hukuwahi kula hivyo.

Oya dogo , laki mbili ni kubwa sana kwa wewe kula miezi miwili kabla ya bumu lingine na pia kulipia hizo hosteli kila mwezi elfu thelathini ambavyo mkishare ni kumi na tano

Dogo wewe mjini ni wa kuja hivyo tuliza akili achana na motivational speaker et tafuta biashara uanza wewe dogo pambana kutunza hicho kidogo kwanza mpaka kiwe kikubwa walau.

Dogo najua una hamu ya kugegedana , bwana mdogo achana na ushenzi wa kuwa na maslay queen tafuta kabinti kashamba kama wewe ambako mtaendana hata siku ukikatoa out basi elfu mbili iwatoshe kunywa soda na kurudi magetoni akupe mzigo.

Dogo hapo ni shule sio kwenye ajira ule upuuzi wako wa kuwatumia ndugu zako hela acha mara moja , Maana bumu likikata hawajawahi kukutumia hata nusu ya ulichowahi kutuma.

Bwana mdogo sio kila mwanafunz ni mwanafunzi hivyo acha shobo na usiowajua sio kila mtu awe rafiki yako .

Dogo ulikuja kusoma au kushindana kuvaa na kwenda bar au Play station Games?
Piga kitabu bwana mdogo kilichokuleta ni hicho tu sio hayo maigizo.

Dogo mambo ni mengi mda ni mchache niache nikawachome sindano wanakijiji ila nikusisitize ukitakata ufanikishe lengo la kuitunza hela anza na kutizama majengo mazuri yote mjini jiulize ni nani pale kwenu analo ikiwa hamna basi jua kwenu ni masikini wa kutupwa acha kuiga pambana uondoe laana ya ukoo wenu.

Pole nimeandika haraka niko na wamama labour na pia nisamehe kwa lugha ngumu ni haraka tu ila mimi ni mstaarabu.

Natanguliza shukrani.
 
Halafu mbona wengine tunamega pis kali sana pasipo kutumia hela au ni swala la nyota
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…